Mzozo wa Marekani na Korea ya Kaskazini si kitu cha mzaha

Junior Ayo

Member
Aug 3, 2016
6
6
Mzozo wa N.Korea na Marekani unaonekana na kama ni kitu cha kawaida sana na kuna baadhi ya watu wanashabikia kama mpira wa miguu Man U na Chelsea lakini sivyo. Mzozo huu ambao sababu yake kubwa ni umilika na vitisho vya Korea ya kaskazini sasa umepamba moto. Kwani Korea ya kaskazini imesema itandelea na mpango wake huo wa kujaribu silaha zake za nyuklia.

Maamuzi haya yamefikia baada ya Taifa za Marekani kama msimamizi wa usalama kupeleka manuari zake na Meli kubwa ambayo ndege zinaweka kupaa na kutua juu yake. Pamoja na silaha hizo korea ya kaskazini haishtushwa na imesema itandelea kila wiki kila mwenzi kufanya majaribio ya silaha hizo ambazo ni kali zaidi. Huku Uhusiano wa Marekani na Korea ya Kusini ukiimarika zaidi ili kuweza kuidhibiti Korea ya Kaskazini.

Duru za habari zinasema kuwa Taifa ya Russia ambalo juzi lilizozona na Marekani dhiti ya hatua ya Trump Kushambulia Syria limeamua kusogeza silaha zake kali za kivita ambapo lipo tayari kukabilia na uchochezi wowote toka kwa korea ya Kaskazini. Hatua hii imefikiwa na rais wa Russio Putin baada ya vitisho vya Korea ya kasikazini kuendelea.

Duru na wataalamu mbali mbali wanasema taifa ya Marekani lina silaha kubwa sana za kuishambulia taifa hilo za Korea ya kaskazini ila tatizo je raia watakuwa katika hali gani. Hata hivyo china ambayo ni mshikirika wa karibu sana wa Korea ya kasikazini naye amesema kuwa atahakikisha mzozo huwa unatatuliwa kwa kutumia diplomasia, na kusema itaiwekea vikwazo vya kiuchumi mshirika wake huyo kwa kukiuka sheria za usalama wa umoja wa mataifa.

WITO WANGU

Wale wanaofurahia haya wasidhani kuwa watapona kama likitokea na kutokea vita yoyote ni mbaya sana. Endapo diplomasia itashindikana na wakapigana basi ujue kuwa Korea inaweza kuzidiwa na Marekani(Mtazamo wangu) ila gharama ambazo Marekani itatumia katika vita hivi itasababisha mdororo mkubwa sana wa kiuchumi ambapo mataifa yote machanga kama Tanzania yataathirika kwa Kiwango kikubwa sana.
 
Back
Top Bottom