Mzee wangu simuelewi kabisaaaaa. Mwaka wa 4 huu amekuwa akinisisitiza nitafute mwanamke mwenye sifa zifuatazo :-
- Awe na elimu isiyopungua form six, na kama ana six awe na mpango wa kusoma zaid ya hapo
- Asiwe mzungu, mhindi wala mchina
- Awe anaingiza kipato kama kazi au biashara
- Asiwe "mtoto wa mjini"
Na mbaya zaidi atataka amu-interview kama ana uwezo wa kujieleza, kabla hajaamua kumkubali. Ninacho shangaa, hajawahi kunieleza kama mapenzi ni muhimu au sio muhimu. Na kali zaidi mke wake mwenyewe (maza) kaishia la 7. Naona kama kuna mbinu za kunitafutia mke hivi . . . .
Kwanza kuna kitu waswahili wamesema "msema pweke hakosi"
Hivi unaamini kuwa baba yake kamwambia ende akamu interview? Naamini hakuambiwa hivyo.
Usikute kaambiwa "mlete tumuone mapema, tuzungumze nae, tuone kama tunaelewana kwa kuwa ndoa si ya wawili tu kwa mila ya kwetu"
Naona kuna watu hawajanielewa, au hawaniamin kwa vile haijawahi kuwakuta. Pengine mnadhan wazazi wote wako sawa kifikra. MZEE KANIAMBIA LIVE UMLETE HAPA HUYO BINTI NA NITAMUULIZA UMESOMA HADI WAPI NA UMESOMEA NINI. Na mbaya zaidi mzee anajitapa kwamba anajua kila kitu, so hata kama kasomea udaktari au uandishi wa habari (wakat yeye ni engineer) atamgundua tu. Sasa hiyo ndo sawa na kusema MLETE NIMUONE??
Msema pweke hakosi ina maana anaehadithia kitu peke yake huwa hawezi kujuulikana kama kakosea kwa kuwa hakuna hadithi kutoka upande wapili.
Yeye kamchora baba yake hivyo na sisi tunaamini kwa kuwa ni msema pweke ndo hakosei 🙁
Soma maoni ya watu uone alivyomtukanisha kwa kuwa tu yeye mwenyewe hakuonyesha kumuheshimu.
Sasa hiyo ndo kumu interview?
Na unaposema anajitapa hivi, anajitapa wapi?
Kaka mbona unaonekana kaa husikilizani na baba yako au kuna cha ziada tusichokijua?
Kwani ulishaona wapi baba mkwe analazimika kujua elimu ya mchumba wa mtoto wake kabla ya kukubaliwa? Kwanini asiulize cha msingi ambacho ni upendo wa kweli??? Elimu itanisaidia nini kama mwanamke hana upendo??
Roselyne hahaaaaaaaa....hakuna mzazi asiyependa mazuri kwa mwanae...inawezekana baba yako hataki ufanye makosa aliyopitia..kumsaili mtu ni kumjua kama anafaa kuwa na wewe au hapana....ila honest mie ningempotezea baba yako,ningehakikisha namletea mkwe na mimba juu...kwi kwii
Anaoa yeye lakini chaguo la baba yake!Unaoa wewe au baba yako?
Pole jaba. Mzee wako anakupenda na anakutakia mema. Ameshaona madhaifu ya mama yako ambae ameishia la saba.
Lakini suala la interview tena jamani!!
Zungumza nae muelewane.
Gaijin lakini asuse kivipi? Huyo baba atakuwa na lake jambo basi!
Wazee wa style hiyo wapo. Madhali vigezo vyake havikufatwa ataona kadharauliwa na atasusa lakini mwisho wa siku ataelewa kuwa uchaguzi wa mke wa mwanawe si wake na I hope atajirudi