Mzee wa Upako: Weka muziki acha maneno ndio yenyewe

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Mzee wa upako amesema kamatia chini imechuja na sasa hv ni Weka muziki acha maneno.Amesisitiza yeye sio mchungaji wa kizamani kama wengine.Pia katika mahubiri hayo amekiri anakunywa pombe.Namwangali hapa Chanel ten muda huu.

Mzee wa Upako aichambua Muziki ya Darassa

TUESDAY , 21ST FEB , 2017
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako' ameichambua ngoma wa msanii wa bongo fleva, Darassa inayokwenda kwa jina la Muziki, na kusema kuwa msanii huyo ameimba vitu vya maana sana kwenye ngoma hiyo.




Mzee%20wa%20upako%20bongo%20fleva.jpg

Mchungaji Lusekelo ambaye amewahi kunukuliwa akitumia maneno ya wimbo huo na nyingine kadhaa za bongo fleva katika mahubiri yake, alikumbana na maswali katika kipindi cha KIKAANGONI cha EATV, ambapo watu walitaka kujua ni kwanini anatumia muziki wa kidunia katika mahubiri yake, badala ya nyimbo za injili.

Akijibu maswali hayo, Mzee wa Upako amesema yeye kama mwanajamii, anaishi duniani pamoja na wana jamii wengine, hivyo ni lazima ajue matatizo yanayowazunguka watu wake ili aweze kuwasaidia na ndiyo maana anajaribu kufuatilia mambo yanayopendwa na watanzanie ikiwemo muziki wa kidunia.

"Muziki ni muziki, hakuna wa kanisani wala duaniani, cha msingi ni ujumbe tu... Sasa ukisema wacha maneno weka muziki, kuna shida shida gani? Ule muziki mi naupenda sana, anasema hakuna jambo gumu kama kumfundisha chizi, na pia ni ujinga sana kusubiri embe chini ya mnazi. Mimi nina nyimbo nyingi hata za kihindi nasikilizaga sana" Alisema

Mzee%20wa%20upako%20Navy%20.jpg


Mbali na ngoma ya Darassa, pia ametoa ufafanuzi wa maamuzi yake ya kuimba wimbo wa Navy Kenzo unaokwenda kwa jina la 'Kamatia Chini', huku akishauri wasanii wa bongo fleva kuimba nyimbo zenye mafunzo badala ya nyimbo za mapenzi pekee.

"Wasiimbe nyimbo za mapenzi tu, walipe pia sadaka kwa taifa... wakati mwingine waimbe na nyimbo ambazo zinaasa maadili"

Kuhusu Diamond na Alikiba, Mzee wa Upako amesita kusema ni yupi anayemkubali zaidi, na kusema kuwa wote ni wa Mungu, na vipaji vyao vimetoka kwa Mungu.

Huyu hapa Mzee wa Upako, akiimba ngoma ya Muziki, Kamatia chini, pamoja na nyimbo kadhaa za zamani
 
Mzee wa upako amesema kamatia chini imechuja na sasa hv ni Weka muziki acha maneno.Amesisitiza yeye sio mchungaji wa kizamani kama wengine.Pia katika mahubiri hayo amekiri anakunywa pombe.Namwangali hapa Chanel ten muda huu.
Kama ni kweli nampongeza sana huyo mzee wa upako maana maandiko Matakatifu yameandikwa wajinga ndio waliowao na watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
Mzee wa upako amesema kamatia chini imechuja na sasa hv ni Weka muziki acha maneno.Amesisitiza yeye sio mchungaji wa kizamani kama wengine.Pia katika mahubiri hayo amekiri anakunywa pombe.Namwangali hapa Chanel ten muda huu.
Hakuna mahali amesema anakunywa pombe, Mimi pia nimemuangalia na kumsikiliza vizuri sana, usiongeze maneno Ili Uzi wako uonekane wa maana.
 
Waafrica zamani tuliwategemea waganga wa kienyeji
siku hizi ndo kama hivi

Labda ndo tunapiga hatua....
Bongo watu wamevurugwa sana Moshi huwezi kutana na haya makitu yaani utahamishwa mpaka kijiji kuna walingia ingia huko vijijini tunawaangalitunawaangali kwa jicho la tatu
 
Nimemuona hapa, kadhoofika sana pombe imemmaliza mpaka sura imekuwa ya kilevi namna ile! Sijui anakunywa unywaji gani huyu!
Pia amesema anasoma sana mitandao na kuona watu wanavyo muandama kwa kumwambia ni tapeli, anahoji je, kupokea sadaka ni kosa?

Panda mbegu ni utapeli kwani Mungu alitoa karama bure na yeye ni kutoa bure.Mungu haongwi kwa pesa ya panda mbegu.
 
Back
Top Bottom