Mzee Mkapa achambua utendaji wa Rais Magufuli

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,887
7,670
RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, ameunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli; hasa katika maeneo ambayo kumekuwa na utata kuhusu namna utekelezaji wake unavyokwenda.

Katika mazungumzo yake na Shirika la Habari la Ujerumani (DW) yaliyofanyika hivi karibuni, Mkapa aliulizwa maswali kuhusu maeneo makubwa manne; utawala wa Magufuli, uhuru wa vyombo vya habari, mgogoro wa Burundi na athari za ukoloni katika maendeleo ya kiuchumi ya Afrika.

Kuhusu Magufuli, Mkapa alimpongeza kwa kufanikisha zoezi la kuondoa wafanyakazi hewa na wasio na vyeti halali vya kazi, na akasema anasikitika tu kwamba kwa nini yeye hakufanya hivyo wakati wa utawala wake.

“Hawa waliofukuzwa ni watu waliotakiwa kuwa wamestaafu lakini bado wanalipwa mishahara. Hawafanyi kazi lakini wanalipwa. Hili ni zoezi ambalo ilikuwa lazima lifanyike.

“Masikitiko yangu pekee ni kwamba kwa nini sikufanya uhakiki huu wakati nikiwa madarakani. Labda nilikuwa na mambo mengine makubwa zaidi niliyotakiwa kuyafanya lakini kwa hili alilofanya Magufuli namuunga mkono kabisa,” alisema Mkapa.

Kwenye eneo la uhuru wa vyombo vya habari ambao unaonekana kuminywa na serikali ya Magufuli, Mkapa alisema kinachofanyika ni kupunguza tu idadi ya vyombo alivyoviita vya “umbea” ili vibaki vichache vilivyo makini.

“Ukiangalia ubanwaji wa uhuru wa vyombo vya habari unaofanyika, mara nyingi ni ule wa kwenye mitandao ya kijamii ambayo mara nyingi imejaa habari za umbea tu ambazo hazina uhusiano wowote na masuala ya maendeleo.

“ Tatizo moja kubwa la vyombo vya habari vya nchi za Afrika hasa hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara ni kwamba nyingi ya habari zinazopewa kipaumbele ni zile za kisiasa na zinazohusu nani ni nani na kafanya nini.

“ Kuna upungufu mkubwa wa habari za kiuchumi na maendeleo zilizofanyiwa utafiti wa kina na zinazochochea. Kuna habari kidogo sana za utetezi wa kimaendeleo na kujipanga ili tupige hatua.

“ Kwa hiyo, huo uhuru wa vyombo vya habari unaosema unabanwa unahusu kundi la vyombo vya habari ambavyo havina mchango wowote katika uchambuzi wa masuala ya kiuchumi, utetezi wa maendeleo wala kujipanga kwenye kujitafutia maendeleo. Nasi ni taifa masikini linalohitaji kuendelea. Nadhani ni uamuzi sahihi,” alisema.

Tangu Rais Magufuli aingie madarakani takribani mwaka mmoja na nusu uliopita, kumekuwa na magazeti yaliyofungiwa na wapo watu waliofikishwa mahakamani kwa sababu ya kuandika maneno yasiyopendeza kumhusu Magufuli mwenyewe au serikali yake.

Katika mahojiano yake hayo yaliyotangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkapa alisema kwamba kwa sababu ya vyombo vya habari vya Tanzania ‘kukalia politiki’, hata mafanikio ambayo utawala wake unasifika huko nje kwa kurekebisha uchumi na kufutiwa madeni, hayapewi umuhimu huo hapa nchini.

Mkapa anakuwa rais wa kwanza mstaafu wa Tanzania kuzungumzia hadharani utendaji wa Magufuli ambaye alichukua nafasi ya Jakaya Kikwete baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Kuhusu mgogoro wa Burundi ambao Rais Yoweri Museveni wa Uganda amempa Mkapa kazi ya kuzipatanisha pande hasimu katika mgogoro huo, Rais huyo wa Awamu ya Tatu alisema tatizo kubwa ni kwamba wahusika hawataki kukaa pamoja na kuzungumza matatizo yao.

“ Tulipofika kwa sasa siwezi kusema kwamba tuko kwenye mkwamo, hapana. Hatujakwama bado. Tatizo lililopo ni kwamba tunakwenda kwa kasi ndogo sana na hii ni kwa sababu wahusika hawataki kukaa chini kwa pamoja na kuzungumza. Hili ndilo tatizo kubwa,” alisema Mkapa.

Kuhusu uhusiano kati ya ukoloni na kudumaa kwa uchumi wa Afrika, Mkapa alisema tatizo kubwa lililokuwepo ni kwamba kizazi cha kwanza cha viongozi waliodai Uhuru kilijikita sana katika kujikwamua kisiasa na hakukuwa na mipango thabiti ya kujikwamua kiuchumi.
 
Nimependa hiki alichokisema mzee Ben

Kuhusu uhusiano kati ya ukoloni na kudumaa kwa uchumi wa Afrika

, Mkapa alisema "tatizo kubwa lililokuwepo ni kwamba kizazi cha kwanza cha viongozi waliodai Uhuru kilijikita sana katika kujikwamua kisiasa na hakukuwa na mipango thabiti ya kujikwamua kiuchumi"

Huo ndio ukweli na mpaka sasa bado tupo hapa
 
Na ndio maana yeye alikomaa sana na mambo ya uchumi. Nadhani pia ndo mshauri mkubwa wa Magufuli
 
Kuhusu uhusiano kati ya ukoloni na kudumaa kwa uchumi wa Afrika, Mkapa alisema tatizo kubwa lililokuwepo ni kwamba kizazi cha kwanza cha viongozi waliodai Uhuru kilijikita sana katika kujikwamua kisiasa na hakukuwa na mipango thabiti ya kujikwamua kiuchumi.[/QUOTE]

Hapa anamaanisha kwa Mw hakufanya kitu kiuchumi maana sijaelewa vizuri
 
RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, ameunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli; hasa katika maeneo ambayo kumekuwa na utata kuhusu namna utekelezaji wake unavyokwenda.

Katika mazungumzo yake na Shirika la Habari la Ujerumani (DW) yaliyofanyika hivi karibuni, Mkapa aliulizwa maswali kuhusu maeneo makubwa manne; utawala wa Magufuli, uhuru wa vyombo vya habari, mgogoro wa Burundi na athari za ukoloni katika maendeleo ya kiuchumi ya Afrika.

Kuhusu Magufuli, Mkapa alimpongeza kwa kufanikisha zoezi la kuondoa wafanyakazi hewa na wasio na vyeti halali vya kazi, na akasema anasikitika tu kwamba kwa nini yeye hakufanya hivyo wakati wa utawala wake.

“Hawa waliofukuzwa ni watu waliotakiwa kuwa wamestaafu lakini bado wanalipwa mishahara. Hawafanyi kazi lakini wanalipwa. Hili ni zoezi ambalo ilikuwa lazima lifanyike.

“Masikitiko yangu pekee ni kwamba kwa nini sikufanya uhakiki huu wakati nikiwa madarakani. Labda nilikuwa na mambo mengine makubwa zaidi niliyotakiwa kuyafanya lakini kwa hili alilofanya Magufuli namuunga mkono kabisa,” alisema Mkapa.

Kwenye eneo la uhuru wa vyombo vya habari ambao unaonekana kuminywa na serikali ya Magufuli, Mkapa alisema kinachofanyika ni kupunguza tu idadi ya vyombo alivyoviita vya “umbea” ili vibaki vichache vilivyo makini.

“Ukiangalia ubanwaji wa uhuru wa vyombo vya habari unaofanyika, mara nyingi ni ule wa kwenye mitandao ya kijamii ambayo mara nyingi imejaa habari za umbea tu ambazo hazina uhusiano wowote na masuala ya maendeleo.

“ Tatizo moja kubwa la vyombo vya habari vya nchi za Afrika hasa hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara ni kwamba nyingi ya habari zinazopewa kipaumbele ni zile za kisiasa na zinazohusu nani ni nani na kafanya nini.

“ Kuna upungufu mkubwa wa habari za kiuchumi na maendeleo zilizofanyiwa utafiti wa kina na zinazochochea. Kuna habari kidogo sana za utetezi wa kimaendeleo na kujipanga ili tupige hatua.

“ Kwa hiyo, huo uhuru wa vyombo vya habari unaosema unabanwa unahusu kundi la vyombo vya habari ambavyo havina mchango wowote katika uchambuzi wa masuala ya kiuchumi, utetezi wa maendeleo wala kujipanga kwenye kujitafutia maendeleo. Nasi ni taifa masikini linalohitaji kuendelea. Nadhani ni uamuzi sahihi,” alisema.

Tangu Rais Magufuli aingie madarakani takribani mwaka mmoja na nusu uliopita, kumekuwa na magazeti yaliyofungiwa na wapo watu waliofikishwa mahakamani kwa sababu ya kuandika maneno yasiyopendeza kumhusu Magufuli mwenyewe au serikali yake.

Katika mahojiano yake hayo yaliyotangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkapa alisema kwamba kwa sababu ya vyombo vya habari vya Tanzania ‘kukalia politiki’, hata mafanikio ambayo utawala wake unasifika huko nje kwa kurekebisha uchumi na kufutiwa madeni, hayapewi umuhimu huo hapa nchini.

Mkapa anakuwa rais wa kwanza mstaafu wa Tanzania kuzungumzia hadharani utendaji wa Magufuli ambaye alichukua nafasi ya Jakaya Kikwete baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Kuhusu mgogoro wa Burundi ambao Rais Yoweri Museveni wa Uganda amempa Mkapa kazi ya kuzipatanisha pande hasimu katika mgogoro huo, Rais huyo wa Awamu ya Tatu alisema tatizo kubwa ni kwamba wahusika hawataki kukaa pamoja na kuzungumza matatizo yao.

“ Tulipofika kwa sasa siwezi kusema kwamba tuko kwenye mkwamo, hapana. Hatujakwama bado. Tatizo lililopo ni kwamba tunakwenda kwa kasi ndogo sana na hii ni kwa sababu wahusika hawataki kukaa chini kwa pamoja na kuzungumza. Hili ndilo tatizo kubwa,” alisema Mkapa.

Kuhusu uhusiano kati ya ukoloni na kudumaa kwa uchumi wa Afrika, Mkapa alisema tatizo kubwa lililokuwepo ni kwamba kizazi cha kwanza cha viongozi waliodai Uhuru kilijikita sana katika kujikwamua kisiasa na hakukuwa na mipango thabiti ya kujikwamua kiuchumi.

Mwizi lazima.amtetee mwizi mwenzake.Haki ya msingi ya RAIA kuongea hata kama anauona UMBEA tua he tuongee.Vyombo vya habari ndivyo vilivyotoa wizi wote uliofanyika kwenye awamu yake,awamu ya JK na ndiyo vyombo hivyo hivyo vinatumika kuandika wizi wa awamu ya TANO.

Shida ukweli hatupendi kusikia.Tunapenda kusifia tu.Media zinapoongelea wizi wa raslimali za Umma unaziita umbea Bali waongelee Uchumi wa nchi,Bali wasiongelee wabadhirifu wa Mali za umma sababu ni wao wenyewe kwa hilo nalikubali.Ukiwa unakula hatutakiwi kuongea.

Nasubiria Tanzania ya Vi-wonder
 
Mkapa na Magufuli ni watu ambao hawajawahi kuelewa falsafa za MEDIA za Afrika

#Ni media ambazo hata ukijenga reli wao watakuwa wanautumia kupiga siasa tu

Afrika ni siasa 24/7 maana ndo ajira
 
RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, ameunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli; hasa katika maeneo ambayo kumekuwa na utata kuhusu namna utekelezaji wake unavyokwenda.

Ni maoni yake MzeeMkapa, ni haki yake kutoa maoni.

Lakini maoni yake hayabadili ukweli wa hali halisi tunayoiona na kuijua. Ukiyaweka kwenye mizani ya haki na ukweli unaona chembechembe za u-CCM, na Mh Mkapa ni kada mashuhuri tu CCM hivyo hilo ni jambo la kawaida kabisa kutokea.
 
Anakumbuka shuka kumekucha...

Back
Top Bottom