Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
MWENYEKITI wa chama cha United Democratic (UDP), John Cheyo, ameibua mpya baada ya kudaiwa kuahirisha Mkutano Mkuu wa chama hicho uliopangwa kufanyika wiki iliyopita kutokana na yeye kuugua katika siku ya mkutano huo, Raia Mwema limeambiwa.
Mkutano Mkuu huo ulikuwa umeitishwa jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, ulipanga kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa chama hicho katika ngazi ya taifa kwa mujibu wa Katiba ya UDP.
Kwa mara ya mwisho, UDP ilifanya uchaguzi wake mwaka 2011 na ilitarajiwa kuwa mkutano huo uliotakiwa kufanyika mwaka 2016 lakini haukufanyika kutokana na kukosekana kwa fedha, ungefanyika na kuhitimisha hitaji hilo la kikatiba.
Hata hivyo, wakati wajumbe wanaokadiriwa kufikia takribani 400 wa UDP kutoka mikoa yote ya Tanzania wakiwa tayari ukumbini, ililetwa taarifa kwamba Cheyo hajisikii vizuri na kwamba mkutano huo umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena.
Aliyetoa taarifa hiyo alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa UDP Taifa, Ausi Likundasy, ambaye aliwataka wajumbe hao kupiga kura ya kukubali kuahirisha mkutano huo hadi itakapotangazwa baadaye. Uamuzi huo unaelezwa kukubaliwa na sehemu kubwa ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo.
“ Ulipofika muda wa kuanza kwa mkutano, Mwenyekiti (Cheyo) alikuwa hajafika ukumbini. Simu yake ikawa haipatikani na kwa kweli ikawa taharuki kidogo. Tukawa tunajiuliza kama amekumbwa na tatizo lolote.
“ Ndipo baada ya muda mfupi akaja Makamu Mwenyekiti na kututangazia kwamba Mwenyekiti ameugua ghafla na daktari amemzuia asitoke hospitali. Kwa sababu hiyo, Makamu Mwenyekiti akaomba wajumbe wapige kura kuruhusu Mkutano Mkuu uhairishwe hadi utakapoitishwa hapo baadaye.
“ Kwa namna alivyokuwa anazungumza, halikuwa suala la kujadiliana bali huo ndiyo uamuzi. Kura yenyewe ilikuwa ya kusema kwa sauti. Sasa hatujafanya mkutano tangu mwaka 2011 na hata muda wa uongozi uliopo madarakani umemalizika. Cha ajabu mkutano wote unaahirishwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa mtu mmoja. Hiki kwa kweli ni kituko cha mwaka,” Raia Mwema limeelezwa na baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo waliozungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina yao.
Gazeti hili limeambiwa na wajumbe waliohudhuria mkutano huo kwamba uamuzi huo wa Cheyo unasikitisha kwa sababu chama kina hali mbaya kifedha na kuwa sasa kitajiingiza kwenye gharama nyingine bila sababu.
“ Hebu fikiria, tumetembeza bakuli kwa marafiki mbalimbali hadi kufanikiwa kukusanya kiasi kinachotakiwa kwa ajili ya kuwaleta wajumbe hapa Dar es Salaam. Watu wamekuja na badala yake wanaambiwa mkutano umeahirishwa kwa sababu mtu mmoja anaumwa.
“ Katiba yetu inaruhusu Makamu Mwenyekiti kuendesha Mkutano Mkuu kama Mwenyekiti hayupo. Sasa Makamu yupo lakini badala ya kuendesha mkutano yeye ndiyo kwanza anauahirisha. Sasa tutapata wapi fedha nyingine za kuendesha huu mkutano?” mmoja wa wajumbe wakongwe wa mkutano huo aliliambia gazeti hili.
Katika mazungumzo yake na Raia Mwema, Cheyo alisema uamuzi wa kuahirisha mkutano huo ulifanywa na wanachama wenyewe kwa kuzingatia umuhimu wa mkutano wenyewe.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu walipitisha kwa kauli moja suala la kuahirishwa kwa mkutano ule. Mkutano Mkuu ni muhimu kwa chama na usingeweza kufanyika bila ya kuwepo kwa Mwenyekiti, alisema Cheyo.
Alipoulizwa ni lini mkutano huo umepangwa kufanyika tena, Cheyo alisema tarehe nyingine itapangwa na itatangazwa na kuwa hakuna tatizo lolote kwa sababu uliofanyika ulikuwa ni uamuzi wa wanachama wote.
“ Najua kwamba kuna watu wasioitakia mema UDP wataamua kuleta matatizo kwa sababu zao lakini huu ni uamuzi ulioungwa mkono na wajumbe wote wa Mkutano Mkuu na hata rekodi za mkutano zinaonyesha hivyo. Sasa anayepinga maamuzi ya wajumbe ni nani,” alihoji.
Ingawa mkutano huo ulipangwa kufanyika Mei 27 mwaka huu, hakukuwa na taarifa zozote zilizotoka kuuhusu, zaidi ya taarifa iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari kuhusu kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Godluck ole Medeye, ambayo ilitoka siku iliyofuata.
Katika taarifa hiyo, Medeye ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, hakutoa sababu za msingi za kuchukua uamuzi huo zaidi ya kusema apate muda wa kupumzika na kufanya mambo mengine.
Taarifa hiyo ndiyo iliyozua maswali katika duru za kisiasa hapa nchini, kwa sababu wakati anajiunga na UDP akitokea katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Medeye alisema anakwenda kupigania mabadiliko ya kweli hapa nchini.
Raia Mwema linafahamu kwamba mwanasiasa huyo alikuwa amejitoa vya kutosha katika uendelezaji wa chama hicho; ikiwamo kukubali kutoa ofisi kwa ajili ya matumizi ya chama hicho.
Katika mazungumzo yake na gazeti hili wiki hii, Medeye alikataa kuzungumza lolote kwa maelezo kwamba alikuwa kwenye msiba wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Moshi Mjini kwa miaka 15, Philemon Ndesamburo, aliyefariki dunia wiki iliyopita.
“ Sina cha kusema zaidi ya ile taarifa yangu mliyoiona. Kwa sasa naelekea kwenye msiba wa mzee Ndesamburo mjini Moshi na sina cha zaidi cha kueleza,” kiongozi huyo aliliambia gazeti hili.
Gazeti hili lina taarifa kwamba baadhi ya wanachama wa UDP wamekwenda kwenye Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa kwa lengo la kutoeleza kufurahishwa kwao na uamuzi huo wa kiongozi wao huyo wa chama.
Hata hivyo, katika mazungumzo yake na gazeti hili, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, hakukana wala kukubali kupokea malalamiko hayo ya wanachama hao wa UDP.
“ Labda niseme kwamba kwa sasa sitajibu maswali yako. Kama hao wanachama wamekwambia kwamba walikuja ofisini kwangu kwa ajili ya suala hilo, kwanini wamekuja na kwako?
“ Mimi ni mtu ambaye ninapenda suala moja litatuliwa na ofisi au taasisi moja tu. Kama leo likiwa huku na kesho ukalisikia kule maana yake ni kuwa baadaye mambo madogo tu yanaweza kufanywa kuwa makubwa.
“ Mimi nakuheshimu sana wewe mwandishi na gazeti lako lakini kwa sasa ningeomba nisiseme chochote kwa sababu ambazo tayari nimekueleza,” alisema Jaji Mutungi.
John Momose Cheyo amekuwa Mwenyekiti wa UDP tangu kuanzishwa zaidi ya miaka 20 iliyopita na amewahi kuwa mgombea urais wa chama hicho na mbunge kwa vipindi vine.
Kulikuwa na fununu, kabla ya mkutano huo wa Mei 27, kwamba Cheyo angeachia ngazi ya Uenyekiti na kubaki kuwa mjumbe wa heshima wa Kamati Kuu ya chama hicho ambacho yeye ni mwasisi wake.
Kutokana na matukio ya mkutano huo, Cheyo sasa ataendelea kuwa Mwenyekiti wa UDP hadi hapo mkutano mwingine wa uchaguzi utakapoitishwa.