Mzanzibar ni aliezaliwa Zanzibar au alizaliwa nje ya Zanzibar na kupewa Uraia wa Zanzibar.
kila siku tunasikia "wazanzibari" wanadai hiki na kile, hususani kwenye katiba mpya, je wazanzibari ni kina nani hasa? Tuzingatie mifano kama: Rais ali hasan mwinyi kazaliwa bagamoyo lakini ni mzanzibari, Dr shein mzaliwa wa pemba ni mzanzibari, Mmasai, mchaga au "mbara" yoyote atayehamia zanzibar na kukaa miaka kadhaa naye anapewa uzanzibari (kama rais mwinyi).
Hivi mpemba aliyezaliwa bara na kukulia bara anaweza kuwa mzanzibari automatically tu kwa sababu babu yake alizaliwa zanzibar? au yeye atakuwa mbara?
Na je mbara aliyehamia zanzibar akawa mzanzibari (kisheria), akirudi bara na kuzaa watoto, hawa "wanyamwezi" nao watakuwa wazanzibari vile vile? Naomba tusaidiane.
Hapo umetaja wakazi wa visiwa viwili tu Unguja na Pemba ,vipi kisiwa cha Tumbatu,wale sio wazanzibari?au kisiwa cha kojani wale pia nao sio wazanzibari?Au hujui kuwa Zanzibar ni muunganiko(archipelago) wa visiwa takriban 50 na kati ya hivyo kuna zaidi ya 5 ni makazi ya watu?Mpemba+muunguja. Sijui kama kuna mwingine
Mzanzibari ni mtu aliezaliwa katika visiwa vya zanzibar au alieishi kisheria zanzibar kwa miaka kumu mfululizo au mmoja ya wazaziwake ni mzanzibari wa kuzaliwa.
Zanzibar ni Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vidogo vilivyo zunguka visiwa vya Unguja na Pemba
Kama vile visiwa vya tumbatu kojani mtambwe.nk.
Hivi visiwa ni shida tupu. Kuna kiongozi kutoka Zanzibar aliwahi kuwaambia Wazanzibar kuwa 'vichwa/akili kama samaki'. Hiyo kauli naikumbuka,aliyesema nimemsahau.