Mwongozo tafadhali

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,522
Reaction score
14,007
Habari zenu wakuu!
Nina binti yangu amemaliza kidato cha sita 2019
Matokeo yake:
General Studies E,Geography D,Chemistry E,Biology E na BAM E. DIV III point 14.
Naomba kujua je anaweza kupata nafasi ya kusoma chuo kikuu na akapata mkopo?
Je anaweza kupata nafasi ya chuo kikuu kwa udhamini binafsi?
Kama hataweza kupata nafasi ya kusoma chuo kikuu ni kozi gani anaweza kusoma kwa ufaulu huo?
Naomba kujuzwa maana mm sijasoma sana nimeishia darasa la saba la zamani.
Asanteni.
 
Mkuu tafuta mtu mwenye kitabu guide ya TCU au ingia kwa website ya TCU unaweza kipata ukadownload, kisha soma humo namna ya ku-calculate cutting points kutokea kwenye matokeo ya huyo binti yako huku unalinganisha na faculty tofauti tofauti ambazo zitamfaa/zinasoko/anazipenda tukota vyuo tofauti tofauti.

Ila kwa kuanzia ni kwanba anaweza kupata chuo, ila kuhusu mkopo sijui.
 
Mtoto mpaka anafika form 6 maswali yako mengi anaweza kuyajibu, isipo kuwa hayo ya mkopo hakuna mwenye majibu yake hata humu sidhani. Ila hayo anaweza kusoma kozi gani chuo, mwanao atakuwa na clue
 
Kama uko Dsm kuanzia wiki ijayo kama sikosei, Vyuo vikuu vitafanyq maonyesho pale viwanja vya Mnazi 1, kijana aende then afike kwenye kila banda la chuo anachotaka atajua kila kitu.

Swala la mkopo ni je alisoma shule binafsi au za uma?
 
Kama uko Dsm kuanzia wiki ijayo kama sikosei, Vyuo vikuu vitafanyq maonyesho pale viwanja vya Mnazi 1, kijana aende then afike kwenye kila banda la chuo anachotaka atajua kila kitu.
Swala la mkopo ni je alisoma shule binafsi au za uma?
Alisoma ya private kidato cha tano na sita,O level ya serikali pamoja na msingi pia.
Mm nipo kijijini Koromije,sipo Dar.
Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…