Mwl Nyerere alifuta demokrasia ili alete maendeleo haraka,akashindwa,JPM pia atashindwa!

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,012
20,685
Moja kati ya sababu za mzee nyerere kufuta demokrasia ya vyama vingi ilikuwa ni kuharakisha maendeleo ya nchi

Nchi ikawa inaenda kwa amri moja na kudumisha fikra za mwenyekiti wa chama

Lakini,mwisho wa siku,mzee nyerere aliiacha nchi ikiwa hoi taabani

Nchi zilizokuwa zinafata matakwa ya kidemokrasia katika kila mambo yake, zimechanja mbuga na sasa ziko mbali sana

Maendeleo yanayoambatana na demokrasia huleta "sense of ownership" yaani mwananchi amekaa akajadili na akakubaliana na wenzie nini wafanye

Maendeleo yanaanzia na mwananchi mwenyewe

Je awamu hii itafanikiwa kuleta Maendeleo bila demokrasia?
 
Nadhan hafuti demokrasia Bali anaonesha mipaka ya demokrasia. China hamna hata huu Uhuru wa kutoa comments lakini ni nchi inayokaribia kushika usukani kwenye uchumi wa dunia, Russia inaheshimika sasa dunian kwa nguvu zake lakini jamaa Purtin ni zaid ya diktator..! Sasa hofu yako ni nini au ndio ule msemo mbaaz ikikosa maua husingizia jua?
Miaka 10 ya demokrasia nzurr ya JK imeipeleka Tz hatua ngap mbele?
 
Waafrika sijui mna matatizo gani hamueleweki mnataka maendeleo au demokrasia,maana tumekuwa tunalazimishana kuaminishana kwamba maendeleo huendana na demokrasia wakati huo huo kuna nchi ambazo zina madikteta au zilikuwa na madikteta lakini zilikuwa na maendeleo.

Tunapozungumzia maendeleo basi tuzungumzia maendeleo na tunapozungumzia demokrasia basi tuzungumzie demokrasia,na sio kuanza kuaminishana kwamba maendeleo huendana na demokrasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ashindwe mara ngap?, alipokurupukaga kwenye sukar, wajanja tukawa tumejua MUNGU katupa jinamizi lingne.

Hapa hapa tuliopinga upuuzi wake wa sukari tukaitwa vibaraka.

Mashabiki wake mpaka leo wanasubiri sukari ya bure.
 
  • Thanks
Reactions: F9T
Leo wametaifisha almasi. Tunarudi kule kule kwa njia zile zile na watu wanashangilia.
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, mfumo huria ulipoingia,utaifishaji ulipigwa marufuku,

Sheria iliingiza due process,lodge malalamiko yako mahakamani/tribunal/kwa arbitrator ili awasikilize,upate haki yako

Hii kampuni inamilikiwa na serikali pamoja na muwekezaji,huwezi kama serikali ukasema ulidanganywa wakati una wawakilishi wako kama mwanahisa,bora useme wote mliingia chaka(serikali na muwekezaji) kama ni chaka,taratibu ni kuomba ulichopunjwa tu,basi may be na other legal penalties,sio uchukue kila kitu

Hawa jamaa utawasikia wako uswisi mahakama za kimataifa
 
Hapa hapa tuliopinga upuuzi wake wa sukari tukaitwa vibaraka.

Mashabiki wake mpaka leo wanasubiri sukari ya bure.
hahaha sio sukari tu, mkuu umesahau na noah, yaan wanasubiri wawe wanaendesha noah huku wanaramba sukariguru, hahaha lumumba ni shidaa aisee.
 
Nadhan hafuti demokrasia Bali anaonesha mipaka ya demokrasia. China hamna hata huu Uhuru wa kutoa comments lakini ni nchi inayokaribia kushika usukani kwenye uchumi wa dunia, Russia inaheshimika sasa dunian kwa nguvu zake lakini jamaa Purtin ni zaid ya diktator..! Sasa hofu yako ni nini au ndio ule msemo mbaaz ikikosa maua husingizia jua?
Miaka 10 ya demokrasia nzurr ya JK imeipeleka Tz hatua ngap mbele?
Kwanini huwa mnapojenga hoja za kuhalalisha hoja zenu huwa mnatumia mifano ya nchi ambazo zimewapiga gap sana hasa ukizingatia sie hata kutengeneza "toothpick" hatuwezi alafu unajifananisha na china...kwanini usijifananishe na Kenya, Msumbiji, Rwanda, Ghana na nchi zingine za Afrika
 
hahaha sio sukari tu, mkuu umesahau na noah, yaan wanasubiri wawe wanaendesha noah huku wanaramba sukariguru, hahaha lumumba ni shidaa aisee.
Anasema ataruhusu wachimbaji wadogo wavamie migodi wakachimbe

Hajui hii dunia imevuka huko
 
Back
Top Bottom