Mwisho wa mwisho wa CCM

Last emperor

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2015
Posts
10,346
Reaction score
9,881
Kwa heshima nawasalimia wana jukwaa la Jamii forum!

Wakati akifunga mkutano wa 8 wa CCM, tarehe 13/11/ 2012 Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, alisema" Nataka mfahamu ndugu zangu tukiishi kwa kutegemea jeshi la polisi kufanikisha mambo yetu, tutakwisha na tutakwisha kweli". Hiyo ilikuwa ni takribani miaka 9 iliyopita. Kipindi kile kilikuwa ni mwanzo wa mwisho (The beginning of the end) wa CCM. Nchi ndo kwanza ilikuwa imetoka kwenye uchaguzi ambao Mh Kikwete alitoka kupambana na Dr. Slaa. Kikwete ambae muhula wake wa kwanza ambao alikuwa ameshinda kwa wastani wa 80% ya kura zote za uchaguzi, uchaguzi wa pili uliompambanisha na Dr. Slaa alishinda takribani 60% za "mashaka", upinzani ukiwa na nguvu sana, nchi ilianza kuona matumizi makubwa sana ya dola. Wapinzani wakipigwa, kuvunjwa na kukamatwa kila siku... CCM ikaanza kujificha kwenye kichaka cha polisi.

Miaka mitatu baada ya Kikwete kutoa kauli hiyo, nchi iliingia tena kwenye uchaguzi, safari hii CCM wakimsimamisha Magufuli, bahati mbaya huyu hakuona aibu kabisa CCM kutegemea polisi katika kufanya shuguli za kisiasa. Mikutano ya kisiasa ikapigwa marufuku, wapinzani wakapigwa risasi hadharani, wengine wakavunjwa miguu, wengine wakapewa kesi za uhujumu uchumi na wengine wakapewa kesi za mauaji. Tanzania ikawa police state. Kukawa hakuna tena siasa, ikawa nchi inaendeshwa kidikteta. CCM wakaipenda hiyo, maana wakawa wanashinda chaguzi kwa kupita "bila kupingwa". CCM ikajisahau na kuacha kufanya siasa na kunadi ambayo serikali ya chama Chao imeweza kuyatelekeza, chama kikawa kinategemea dola kiwaziwazi. Hadi kupelekea katibu mkuu wake akasema " Tutatumia dola kubaki madarakani" bila aibu na kwa kujiamini kabisa ( That was the middle of the end). Mwalimu wa siasa wa chuo kikuu uwezo wake wa kufikiria ukaishia hapo, akasahau kuwa siasa ni ushawishi.

Utawala wa awamu ya 6 umeingia nao wanaendeleza makosa yaleyale ya kutegemea dola. Mbaya zaidi, CCM ya sasa hivi haina watu wenye mvuto kabisa katika uongozi wake, zamani CCM ilikuwa ina viongozi wanaojua siasa hasa, hata kama ni za uongo ( propaganda), watu kama Kingunge Ngombale Mwiru, John Malecela, Abrahaman Kinana, Jakaya Kikwete, Edward Lowassa nk... angalau walikuwa wanajua siasa na wana ushawishi katika nchi.

Lakin wanasiasa waliopo sasaiv CCM hawana ushawishi wala hawajulikani kwa wananchi, hata ukiamua kufanya utafiti mdogo tu ukauliza wananchi huko mtaani nani ni Katibu mkuu wa sasa wa CCM, hakuna anaejua, wala naibu wake, hakuna anaejua wala kujali..( the end of the end). Hata ukitafakari ni kiongozi gani aliyopo CCM sasaiv ana mvuto kwa wananchi na ana uwezo wa kupambana na Tundu Lissu kwenye uchaguzi wa 2025 kama kutakuwa na uchaguzi huru na wa haki na akashinda.. unaona hakuna. Tutegemee matumizi makubwa sana ya nguvu za dola kuliko kipindi chochote toka nchi ipate uhuru ili CCM ibaki madarakani.

Chama Cha Siasa kinapofikia mahali hakina "touch" na wananchi kinakwisha, Chama Cha wakulima na wafanyakazi inapofikia kiongozi wake anawaambia "wale wasioweza kulipia gharama za choo wabaki na mavi yao nyumbani" ... Kiongozi wa Chama anawananga na "anawaringishia" walala hoi kuwa hawajui "utamu" wa kupanda V 8 lenye kiyoyozi kinakwisha, Chama ambacho viongozi wa serikali yake wanaambia kwa madharau wenyenchi kuwa kama hawataki tozo mpya inayowaumiza "wahamie Burundi"...kinakuwa kimefika mwisho wa mwisho. Namna pekee wanayoweza kuendelea kubaki madarakani ni kwa kutumia mabavu ya dola. Na historia inaonyesha siku zote wananchi huwa wana uwezo wa kuishinda dola..hata kama itapita muda gani. Mwisho wa CCM umefika. It's a matter of time..
 
Kete ya mwisho ya ccm ni police,usiombe RPc au OCD kahaidiwa ubunge baada ya kustaafu, wapinzani watapata tabu Sana eneo hilo.
Na hapa ndio chanzo kikubwa cha yote haya, maana mtu ambae ni mtumishi wa umma kama polisi, au usalama unakuta ana kadi ya CCM..hii ni aibu kubwa na mwanzo wa uovu
 
Karata kubwa yaa ccm ni wapiga kura mbumbumbu walioko vjjn..kama hatutawaelimisha bibi zetu tuliowaacha huko vjjn ...kura haztakuja kutosha ...unakuta mama n maskin hana hata unga amevaa kilemba cha ccm...walahi napataga hasra sanaa
 
Utawala umeshaanza kufitinika.
 
kuhusu ccm kufika mwisho, kwa hakika wameshafika.
hawana ubunifu wala ushawishi, wanademka tu kama mwenyekiti wao wa chama anavyodemka hivi sasa.
mwenyekiti wao anaongelea nadharia nyingi.
wanasabisha njaa kwa wananchi ili waendelee kushika madaraka.

2025 si mbali hakuna rangi ccm wataacha ona, hii ni fununu tu na hawana uwezo wa kubadili chochote 2025.
 
Na hapa ndio chanzo kikubwa cha yote haya, maana mtu ambae ni mtumishi wa umma kama polisi, au usalama unakuta ana kadi ya CCM..hii ni aibu kubwa na mwanzo wa uovu
ulishawahi jiuliza kwa nini nafasi za kujiunga na mafunzo ya jeshi lazima zipitie kwa mwenyekiti wa mtaa?
kwa ufupi kupata nafasi hiyo lazima uwe mwanachama wa ccm. 😑
 
Ccm wanaibaka nchi, nchi haiwataki wanalazimisha
 
Leo gazeti la chama limedemka na mama. Ile picha alichoraga kipanya mama amelala na nyoka Ina make sense sasa
 
Nimecheka sana... eti hakuna anaemjua katibu mkuu ccm wala Naibu wake, na hakuna anayejali.
CCM sasa maji ya shingo. Ni genge la watu wenye uroho wa kutawala. Hii habari ya gazeti la Uhuru kupotosha habari za ccm, ni kengele rasmi kwamba mwisho wa enzi umefika
 
Angalia wanavyoparangana wao kwa wao



Hiyo ni ndani ya siku moja hiyo...



Ndani ya siku moja hiyo hiyo tena...

 
Karata kubwa kwa CCM ni udhaifu wa wapinzani.

Unapohisi CCM ni dhaifu, angalia wapinzani wake ni dhaifu zaidi.

Laiti kama ule umoja wa UKAWA wa 2015 ungekuwepo hadi sasa, CCM ingepata tabu sana.

Sasa hivi ukiangalia Mwenyekiti yupo ndani, makamo mwenyekiti yupo nje ya nchi, halafu utegemee 2025 kutatokea maajabu ikiwa Polisi wapo upande wao bila kusahau wakurugenzi.

The only way CCM itatoka madarakani kwa mazingira ya sasa ni kwa mpasuko wa ndani ya CCM, itokee team Magu na Team Mama, halafu wapinzani waungane na Team Magu , hapo mchuano utakuwa mkali sana, ila CCM ikiwa haina mpasuko hakuna wa kuiondoa madarakani sababu bado wapinzani hawana hiyo nguvu
 
Ni kweli..Hao wataondoana madarakani wenyewe. Nyerere alisema watu wa kuwaondoa CCM madarakani CCM ni CCM wenyewe. Walianza mwaka 2015, wakageukana, wale ambao walikuwa upande wa Lowassa "wakawakomesha" wa membe kwa kumpigia kura Magufuli. Sasa ipo siku watageukana halaf watampigia kura mtu ambae kwa namna yoyote hawezi kushinda. Lakin hata hivyo, ni nani sasaiv ndani ya CCM mwenye mvuto wa kushinda? Makamba? Mwigulu? Simbachawene? Hakuna... history can take a surprising turn. Nani aliamini siku moja Messi ataenda PSG kwa mazingira yale? Lakin ndo imekuwa hivyo. Na itakuwa hivyo kwa CCM. Hawatojua hata nini kimetokea. Save this for reference one day
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…