Mwisho wa mwaka mbaya kabisa kwangu kuwahi kutokea

Ndugu wanajamvi
Tujipe pole na mambo magumu yanayoendelea kutupata ikiwemo Mkurugenzi wetu Melo kuswekwa lumande, lema kuendelea kusota, mara zika, Ben saa8 kapotea
Nina imani tutapita ktk vipindi hivi vigumu.
Binafsi nimekuwa na wakati mchungu kabisa katika maisha yangu kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
Mwezi jana nilifiwa na mama yangu mzazi aliyeniachia madogo 3, kwa mara ya kwa nimeanza kuhis kukomaa zaidi ukilinganisha pesa ilivogoma.
Last week alikuja niaga mpenzi wang ambaye ni mnyaturu wa manyoni, huyu Dada ni askari nilikutana naye mwaka mmoja nyuma,nilichelewa kwenda kwao kwa sababu ya dini, ingawa siku za hivi karibuni nilibadili msimamo nimuoe tu yy, na tukahaidiana kutambulishana mwezi march next year akichukua likizo kubwa.
Sasa jana nimepiga simu usiku saa tano, kanapokea kajamaa ,du!!! I was shocked, nilisikia maumivu sana.
Nikaongea na huyo Dogo akadai yeye anaye miaka 6 kweny uhusiano, nimeamua kumuacha huyo Dada ingawa nasubir kesho arudi tuzungumze kwa nini aliamua kufanya vitendo vya namna hiyo, nilikuwa naye karibu kiasi kwamba ofsn kwao wanajua natoka naye hata ofsin kwangu pia wanajua.
Nilitaka nimuoe kabla ya kwenda shule kwa masomo ya juu zaidi,
Ki ukweli nimeumia sana sana, nimeshindwa kumsimua hata rfk ang wa karibu, nipo ndani tu leo,

Nchi yangu pendwa haileweki, Mama amenitoka na mchumba tena kaondoka du mwaka mbaya huu.
pole sana chief unayopita wewe ndo yaliyonikuta mimi wik iliyopita nimeachana na mchumba angu niliyedumu nae kwa miaka minne na tulipanga mwakani mwezi wa 3 tuoane kumbe yaliyopo nyuma ana mtu mwingine wana zaid ya mwaka na wana enjoy love.wanawake cyo watu.
 
We unaoa askari una akili wewe? Vitu vingine mnajutakia tu, kisa salary msaidiane maisha? Sikupi pole kuhusu huyo mchuchu..yani seriously we sio askar uoe askari duh
 
Pole mkuu kwa kuondokewa na mama. Huyo kicheche achana nae, mi mwenzio nilishajaziwa hadi mimba. Nikailea miezi mitatu, bahati nzuri raia wema wakaning'ata sikio kuwa kuna njemba napokezana nayo! Nikatupa kule. Ilikua 2006 hadi leo niko poa! Ukimrudia haya!
 
Mkuu acha kulinganisha uchungu wa kufiwa na mama mzazi na vitu vya kijinga, yani mama yako amekubeba tumboni miezi tisa, akakuzaa kwa uchungu, akakulea kwa shida, amekusomesha hadi kufika hapo ulipo, leo unamlinganisha na huyo mwanamke aliyekufanya wewe mchepuko!!
 
Wajulishe rafiki zako wa karibu hasa mnaoshibana ili upate sapoti yao. Usipende kukaa peke yako ndani kwani katika "upweke" mengi huweza kutokea hasa maamuzi yasiyo chanya.
Badala ya kuhuzunika sasa, furahi kwani hili limetokea mapema kabla hamjafanya mamuzi magumu.
Let her go, bro!
 
We unaoa askari una akili wewe? Vitu vingine mnajutakia tu, kisa salary msaidiane maisha? Sikupi pole kuhusu huyo mchuchu..yani seriously we sio askar uoe askari duh
Sio kila anayeoa mfanyakazi basi anaoa kwa ajili ya salary, usiwe single sided mind
Ao askari wa form 4 failure wana mshahara kias gan
 
Mkuu acha kulinganisha uchungu wa kufiwa na mama mzazi na vitu vya kijinga, yani mama yako amekubeba tumboni miezi tisa, akakuzaa kwa uchungu, akakulea kwa shida, amekusomesha hadi kufika hapo ulipo, leo unamlinganisha na huyo mwanamke aliyekufanya wewe mchepuko!!
Hapana sijafanya ulinganifu wowote hapo juu
 
Hapana sijafanya ulinganifu wowote hapo juu
Umesema mwaka mmoja umempoteza mama yako na pia umesikitishwa na kuachwa na hyo mpenzi wako. Yani maumivu ya kupotelewa na mama unayaweka kundi moja na maumivu ya kuachwa na mwanamke!111!!! hapo ndo kwenye ulinganifu.
 
You gotta go through hell to appreciate the heaven, my borther.

2016 has been a topsy turvy one for moi, but a great one all together. The chick I connected and cared big-time for started acting up, so I decided to chill(still miss her); invested quite a sum on some that went south; but I also achieved great things that I'll forever be proud of. Like Tupac once put it, so many battlefield scars while driven in plush cars.
 
Back
Top Bottom