Mtanzania Safi
Member
- Oct 9, 2014
- 95
- 13
Dira, Leo jumatatu trh 22-28, december 2014.
MWIGULU ANAVYOWALILA MAIGE NA NGELEJA BARAZA LA MAWAZIRI (2)
(Nukuu iliyo ndani, "mpaka leo sijui kosa la Maige na Ngeleja ni nini!")
Kwa wasomaji wapya: katika toleo lililopita, makala haya yaliishia katika aya inayosema, "Katika operesheni tokomeza ujangili, wabunge wa CCM walikutana, bila kuwahusisha mawaziri watuhumiwa, kwenye ukumbi wa Pius Msekwa Dodoma na kuazimia mawazir hao wawajibike na kumtaka waziri mkuu awajulishe na kuwataka waje bungeni kutangaza maamuzi hayo jioni ya siku hiyo".
Endelea.
Mwezi mei, 2013, Mbunge mbunge wa nyamagana Hezekiah Wenje alisema bungeni kwamba, Bunge lilimuonea Maige.
Akichangia hotuba ya bajeti ya Waziri mkuu, Wenje alilalamikia utaratibu wa bunge kufanya maazimio kwa kufuata upepo bila kuchunguza kwanza.
"Mhe. Spika, mwaka jana (2012) Maige tulimfanyia kitu tunachoweza kukiita political mob justice', kwani tulimhukumu kwa tuhuma za kusafirisha wanyama hai kupitia KIA (Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro) Novemba 2010 huku tukijua kwamba Maige si mlinzi wa airport wala hakuna mahala popote ambapo alikuwa amesaini kuidhinisha kusafirishwa kwa wanyama hao.
Tena tulimfanyia hivyo kumbe wakati huo watuhumiwa 6 wa tukio hilo wakiwa mahakamni Moshi. Hii si sawa", alisema Wenje.
Katika mkutano huo huo wa mei 2013, Mbunge wa simanjiro Christopher Ole Sendeka naye alilalamikia uamuzi wa bunge kuhusu Maige na Ngeleja mwaka 2012 kwamba haukuwa wa haki kwani watuhimiwa hawakupewa muda wa kujieleza.
Aidha, Sendeka alimuomba radhi hadharani Lowassa kwa kumhukumu bila kujiridhisha na tuhuma zilizokuwa zikimkabili mwaka 2008.
"Mh. Spika, mtindo huu wa watu kufanya lobbying na sisi kuwahukumu mawaziri si sawa. Tuliwaondoa akina Maige na Ngeleja bila kuwasikiliza kwa shinikizo la wafanyabiashara malobbists bila kuwasikiliza walalamikiwa."
Mpaka leo sijui kosa la Maige na Ngeleja ni nini! Naomba radhi sana kwa mh.Lowassa kwani naye tulimhukumu kwa mkumbo", alisema Sendeka akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya Nishati na Madini.
Novemba 2014, Mbunge wa Longido, Michael Lekule Laizer naye alipaza sauti akilalamikia kitendo cha bunge kutoa nafasi ya kusikiliza maelezo ya Waziri Muhongo kwa saa mbili ikihali bunge halikufanya hivyo kwa mawaziri tuliowawajibisha bila kuwasikiliza", alisema Lekule Laizer.
April 23, 2012 kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, kupitia mwenyekiti wake James Lembeli (CCM, Kahama)iliwasilisha taarifa yake bungeni ikimtuhumu aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ezekiel Maige kugawa vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa upendeleo na kuweka mazingira ya rushwa kwa kuendesha zoezi hilo la ugawaji vitalu bila uwazi na kutoa matokeo ya waliopewa vitalu bila kutaja vitalu walivyogawiwa.
Aidha, taarifa hiyo ya kamati ilihusisha uchunguzi ambao kamati ilifanya kufuatia kuwepo kwa taarifa kwamba twiga wawili walitoroshwa nje ya nchi kwa kutumia kibali kilichotolewa April 16, 2011 na Mohammed Madehele aliyekuwa Afisa Wanyamapori Mkuu kwa niaba ya aliyekuwa Katibu mkuu wa wizara hiyo, Maimuna Tarishi. Katika taarifa yake, Kamati ilimtuhumu Waziri Maige kwamba alifanya upendeleo kwa kuzigawia kampuni 16 za uwindaji wa kitalii ambazo hazikuwa na sifa.
Hata hivyo, taarifa hiyo ya kamati ilieleza kuwa kwa ujumla utaratibu uliofuatwa katika zoezi la ugawaji vitalu ulizingatia sheria na taratibu .
Kwa upande wa tuhuma za utoroshwaji wa twiga wawili April 16, 2011, taarifa ya kamati ilisema, "Kamati haikupata ushahidi wowote kwamba twiga(wawili waliotolewa kibali cha kukamatwa trh 16, 2011kupitia kamapuni ya Junglew International ya Dodoma kwa niaba ya kampuni ya SAVANNA Plains International schools ya Shinyanga), walikamatwa, kuuzwa au kusafirishwa nje ya nchi".
Kwa upande wa zoezi la ugawaji vitalu uchunguzi uliofanyika baadaye baada ya Waziri Maige kuwajibishwa, ulioonesha kwamba zoezi la ugawaji vitalu lilizingatia sheria na kwamba hakukuwepo kampuni yoyote iliyopewa kitalu bila kuwa na sifa stahili kama ilivyotuhumiwa bungeni na kamati ya Lembeli.
Uchunguzi huu ulifanya na Waziri Kagasheki aliyevaa viatu vya Maige baada ya Maige kuondoshwa.
Kufuatia uchunguzi huo uliofanywa na Kagasheki, Waziri huyo aliamua kutofuta zoezi la ugawaji vitalu lililofanywa na Maige na wala hskuzinyang'anya vitalu kampuni 16 zilizotuhumiwa bungeni kwamba zilipewa vitalu bila kuwa na sifa
Aidha kuna taarifa kwamba kampuni hizo 16 zililalamika kwa Spika kwa kuchafuliwa biashara zao kwa kutangazwa kwamba zilikuwa na sifa na zilifuata utaratibu uliowekwa kisheria.
Kampuni zinazoendelea na uwindaji wa kitalii ni zile zile 60 zilizogawiwa na Maige, novemba 2011(zikiwemo 16 zilizotuhumiwa kwamba zilipewa bila sifa).
Sheria ya wanyamapori na, 5 ya 2009 inaelekeza kwamba kampuni haiwezi kugawiwa kitalu kama haitakuwa na sifa.
Na mwandishi wetu,.