Kero ya Kigamboni ni umeme kukatika katika ingawa ambaye yupo kule tangu 2010 atakwambia sasa hivi haukatiki.
Miaka hiyo umeme ulikua unakatika hadi wiki mbili siku hizi labda ni mara mbili au tano kwa mwezi.
Wamakonde, Waarabu na Wanafunzi wa Chuo ndiyo wengi.
Ukifika ukiulizia gesti ukiona unapelekwa gest ambayo hamtumii barabara ya lami ila mmeingia makazi ya watu na nje ni kama nyumba kataa.
Ni mbaya sana, kuanzia huduma mpaka samani zake.
Wanajeshi wa Navy hawatojisumbua na kukulinda jilinde mwenyewe, kua attention haswa haswa ukiwa pale Ferry usiku na maeneo ya huku mbele usiku wa manane.
Kuna siku pantoni litazingua kama utaamua kupanda fiber/ vimtumbwi jiridhishe kua hakuna meli inayoingia au kutoka. Walikufa watu zaidi ya 5 siku hiyo na haikutangazwa popote.
Hairuhusiwi kupiga picha ndani ya pantoni, ukikamatwa jifanye hujui kiswahili. Hairuhusiwi kuingia na mtungi wa gesi kwenye pantoni.
Nauli ya pantoni ni 200, nashauri uwe na hela inayochenjika kwa urahisi pia kama wameishiwa tiketi hautapita hadi wazipate upya. Kama ni askari utapita bila kulipa na hata mwendokasi hautalipia.