Mwenzi mshirikina

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,010
Reaction score
60,484
Waswahili wanasema Mtu akipata Pesa ndo utamjua vizuri, ukipata matatizo ndo utamjua mwenzi wako vizuri lakini pia mwenzi wako akipata matatizo ndo unapata fursa ya kumjua vizuri kwa namna atakavyokabiliana na tatizo lake.

Sasa je ikitokea mwenzako kapata matatizo ya kikazi,kifedha, kifamilia,ugonjwa alafu ukagundua kwamba anaamini sana ushirikina na ndo kimbilio lake la kwanza kutafuta utatuzi wa tatizo lake utafanyaje?! Hapo ni baada ya kuishi ama kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu miaka miwili na hukuwahi kujua msimamo wake kuhusu hayo maswala.
 
kua na hofu ya mungu na kujua mungu ndo kila kitu ktk maisha yangu ndo nguzo yangu ya kwanza either kwenye mapenzi au popote pale. Kua mshirikina katu siwez endeleza penzi mana mshirikina tayar kamkana mungu
 
kushiriki ushirikina nawe mshirikina...............akianza ushauri huo achana nae
 
"A staggering 93% of Tanzanians said religion was very important part of their life, but many people still consult with doctors.."..#ThisDay

Urafiki, uchumba na hadi ndoa ni stages zilizowekwa ili kuchunguza na kujua yote hayo. Zamani wazee waliwaonyesha vijana wapi/nyumba gani inafaa kuingia na moja ya vitu walivyoweka kipaumbele ni pamoja na kuepuka washirikina, wenye maradhi ya kurithi n.k

Hivi vitu ni lazima kuvibaini kabla ya kuanzisha familia. Sema siku hizi tunabebana wala hatuangalii hayo..
 
kweli ni mbaya sanaaaaaaaaa. mtu akiwa mshirikina tegemea haya:

  • hawezi kuwa na maendeleo, pesa itashia kwa waganga
  • kuwa na chuki na watu, maana anamini anarogwa
  • ipo siku atasema hadi mama yake mzazi ni mchawi.
  • kila siku atagombana na majirani kwa ujinga wa kuamini ushirikina.
Jikaze muelimishe tu, tena kama mwanaume ni aibuuu. kama hamjaoana ni bora uanze mbio mapemaaaa.
 

Siku hizi hata chakula asichopenda mwenzi kinajulikana siku kikipikwa/kikinunuliwa na sio mwanzo mahusiano. Mengi yanajulikana baadae kwa "bahati mbaya" na sio kwenye process ya kufahamiana.
 
Siku hizi hata chakula asichopenda mwenzi kinajulikana siku kikipikwa/kikinunuliwa na sio mwanzo mahusiano. Mengi yanajulikana baadae kwa "bahati mbaya" na sio kwenye process ya kufahamiana.
Sasa wewe ukijua mumeo ni mtu wa sangoma baada ya kuachishwa kazi au biashara zake kwenda ovyo utafanyaje?
 
Sasa wewe ukijua mumeo ni mtu wa sangoma baada ya kuachishwa kazi au biashara zake kwenda ovyo utafanyaje?

Hiv had mnaoana ina mana hamjajuana mienendo na tabia zenu tu???? Ndoa n final stage either umeridhika nae au umeamua liwalo na liwe
 
Hiv had mnaoana ina mana hamjajuana mienendo na tabia zenu tu???? Ndoa n final stage either umeridhika nae au umeamua liwalo na liwe
Kama Lizzy alivyosema hapo juu, ''siku hizi hata chakula asichokipenda mwenzi kinajulikana siku kikipikwa''...
Meaning, yapo mengi sana wenzi either wanafichana au hawajali kufahamu/kuambiana wakati wa urafiki/uchumba, wanakuja kushtuka wakiwa ndani ya ndoa..!
 
Last edited by a moderator:

Yeah nkweli
 
Last edited by a moderator:
Sasa wewe ukijua mumeo ni mtu wa sangoma baada ya kuachishwa kazi au biashara zake kwenda ovyo utafanyaje?
Hahahahaha...

Nashukuru Mungu nlonae naujua msimamo wake ila ningekuwa sijui ningejitahidi sana kum-convince otherwise na kumpa mbinu mbadala za kukabiliana na tatizo lake. Aking'ang'ania huko ningetafuta namna tu nimuache maana mtu wa aina hiyo hakawii kumtoa hata mtoto kafara au kumloga mkewe akidanganywa na waganga kuwa mkewe ndo chanzo cha matatizo yake.
 
Lizzy ongera kuwa na mwenza mwenye kumjua Mungu maana moyo wa mtu ni msitu, wapo ambao akipata tatizo aidha kufukuzwa kazi, biashara haziendi na mengineyo mtu wa kwanza kumshirikisha ni lafiki akija ndani anaushauri wake katoka nao uko anakuja yeye kaja na midawa yake na mambo yake, ukiuliza tu duuu! ni bonge la kesi ukizingatia unawatoto huna kazi, ukiondoka unakwenda wapi kumbadilisha mtu ghafla ni Neema ya Mungu. Ukipata mwema wewe mwambie Mungu asante wapo yanayowakuta hayo na hawana jinsi wanataka hawataki watashiriki tu ni shidaa haya mausiano.
 

suregirl acha kabisa. Hii imemtokea mtu wangu wa karibu. Jamaa kafanya madudu yake, mambo yalivyoharibika badala ya kurekebisha kiuana-ume kakimbilia kwa mganga. Alivyokutwa na vifurushi vya dawa na hirizi anajidai eti ni dawa ya tumbo.

Tatizo kuna watu wanapenda sana shortcut. Kuliko kuhangaisha akili anaona bora awahi kwa mganga kupiga ramli.
 
Last edited by a moderator:
Watu wana upofu wa ufaham Lizzy
 
Siku hizi vijana wako busy kufanya ngono hayo ya kujuana na kufahamiana labda baada ya kuingia mikataba ya ndoa.
 
mie mtu asiye mtumainia Mungu apitie mbali kuleeee maana hiyo imani haitakuwa kwake tu bali ni kwa familia ya kwao walivyozoea wa hivyo mkiishi tatizo likitokea tu hawakawii kusema mume/mke wake ndo kamroga mtu wa ivo ata akijikwaa imani yake itaenda kuleeee kwenye kurogwa mie ptuuuuuuuu
 
Hivi ushirikina ndio nini? Naomba kuelimishwa. Maana kama kwenda kwa mganga kuna tosha mtu kuwa mshirikina basi WATZ wengi kama sio wote ni washirikina. Kuna utafiti ulifanyika mwaka 2013 juu ya watu wanaoamini ktk waganga wa kienyeji. Uganda 48% wanaamini, Kenya 28% wanaamini, Tanzania 87% wanaamini. Kwa sababu ya kuzorota Kwa huduma za afya nchini 60% ya WATZ wanatumia huduma za waganga wa kienyeji. Tuacheni kuwa wanafiki kwa kujibalaguza kwenye mitandaoni WATZ tunatumia waganga ktk mambo yetu mengi. Kuanzia siasa hadi kwenye nyumba za ibada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…