Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James umetuacha kwenye matatizo kwa kuwatunuku vijana wa bajaji zaidi ya 100 kadi za chama Njombe

kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
320
154
1544707735051.jpeg
Picha.Baadhi ya wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi mjini Njombe wakimsubiri mwenyekiti Kheri james katika ukumbi wa Tubo.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM chama cha mapinduzi Taifa Kheri james amewakabidhi madereva wa bajaji zaidi ya 100 mjini Njombe kadi za chama cha mapinduzi.

Kheri james amewakabidhi vijana hao katika ukumbi wa Turbo mara baada ya kufika mjini hapo akiendelea na ziara yake mkoani Njombe akitokea katika halmashauri ya wilaya ya wanging’ombe.

Mwenyekiti naomba nikusindikize kwa ujumbe huu Licha ya kuwa wananchi na wapiga kura wa chama chako wa mkoa wa Njombe hususani katika halmashauri ya mji wa Njombe wametumia mda mrefu kukusubiri na kusikiliza ujumbe wako mzuri ulioubeba kutoka ofisi pendwa za Lumumba, hakika machozi na majuto yataendelea kwa wakazi wa Njombe mjini hususani wa kipato cha chini ambao wengi wao tegemezi lao ni usafiri wa bajaji,boda boda na daladala ili kufanikisha shuguri zao za kila siku.

Mkuu sijui ni viongozi wako wa aina gani waliokushawishi uwatunuku vijana wetu wa bajaji kadi angali wanajua fukuto la mgogolo wa vyombo vya usafiri wa bajaji,daladala na bodaboda ndio kwanza mbichi.

Yaani tunawaza sana kwa kuwa hata hivyo hii leo kuja kwako tulidhani kwamba huenda hii migogoro ingekwisha maana vijana wa dalala bado wapo katika shida ila walitulizwa kidogo na mamlaka (SUMATRA) mpaka tarehe 12 ya mwezi wa 12 2018 yaani siku ya jana wakimsubiri mkuu wetu mpendwa Christopher olesendeka atatue shida zao lakini bado majukumu yake yanaendelea kumbana kwani tumeendelea kumuona huko mjini akihudhuria utiaji wa saini katika ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme katika bonde la mto Rufiji.

Mkuu nimalizie tu kwa kusema hakika hawa vijana wa Bajaji ambao hii leo wametunukiwa kadi za chama kwa kweli wataongeza jeuri kwa kuwa wana baba mwema kwao na leo wamepata pa kujivunia kwa kuwa tangu mwanzo ilifahamika kuwa migogoro haiwezi kuisha kirahisi kutokana na maswala ya kisiasa yanayoendelea katika mji wetu wakati bado kuna wananchi tunaoelekea nje ya mji na hata katika hospital yetu ya kibena kuwaona wagonjwa tunaoendelea kupata shida inapotokea migomo ya daladala na kusitisha huduma zao.

mc.amiri/mr.mtaani
 
Back
Top Bottom