Mwenyekiti wa kijiji (CCM) awatapeli wananchi kwa viwanja hewa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Bukombe. Mwenyekiti wa Kijiji cha Azimo kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe (ccm)mkoani Geita, Dickson Ulimwengu anadaiwa kuuza viwanja hewa vya Sh7 milioni kwa watu zaidi ya 150.

Ulimwengu amekiri kuchukua fedha za wananchi kwa ajili ya kuwatafutia viwanja akisema ameanza kuzilipa fedha hizo kidogo kidogo kwa amri ya mahakama.

Mkazi wa kijiji hicho, Emmanuel Yohana amesema mwenyekiti huyo amekuwa akikusanya fedha za wafanyabiashara wa mboga mboga na wananchi wengine akidai kuwatafutia viwanja vya bei nafuu.

“Ametumia uongozi wake kuwahadaa wananchi wampatie fedha ili awatafutie viwanja vya bei nafuu, baada ya kutoa fedha anawapatia risti feki haina mhuri wa halmashauri,”alisema Yohana.
 
Mwenyekiti ameiga tabia za viongozi wake wakuu wa ccm jinsi wanavyofanya utapeli wa kuwaibia wananchi.Sasa huyo aliyetapeli visenti vya kahawa atang'ang'aniwa wakati matapeli wa mabilioni hawaguswi.
 
Back
Top Bottom