Mwenyekiti Wa CCM Si Analipwa Na Chama?Au Anajitokea

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Cheo cha urais ndio cheo kikubwa cha kisiasa kushinda vyeo vingine vyote.Ndio maana siku zote,Rais akimaliza muda wake.Inakuwa vigumu sana kumwajiri au kumpa kazi nyingine aifanye.

Labda kazi za ushauri na usuluwishi tu.
Sasa nimejiuliza hivi CCM si wanamlipa JK mshahara Kwa kazi ya Mwenyekiti?
Kama wanamlipa ni muda muafaka kwa JK kuokoa fedha za chama na kumwachia Rais Magufuli avute huo mshiko.

JK kazivuta kwa miaka 10 inatosha mzee,Mwachie Ngosha naye aanze kuzichanga,
Kwa wadhifa aliokuwa nao JK ni kujizalilisha kuendelea kulipwa mshahara na ka tasisi kama CCM ukizingatia CCM hii si ile tena.Ruzuku yao imepungua sana,Na hali yao kifedha si kama zamani.

Pili sioni haja ya Nape kula mishahara miwili.Ni vizuri awaachie vijana wengine wa lumumba nao wapate mkate wa kila siku.Wapo vijana wengi wa CCM wasio na ajira na wanaweza kuimudu nafasi ya Nape kwa ubora na viwango.
 
Last edited by a moderator:
mkuu,
suala la kuacha uchairman JK linataratibu si kwamba anakomaa tu makusudi sawa tu na nape. kuna kanuni na katiba zao. so ni suala la muda na kanuni.
 
mkuu,
suala la kuacha uchairman JK linataratibu si kwamba anakomaa tu makusudi sawa tu na nape. kuna kanuni na katiba zao. so ni suala la muda na kanuni.
Ni sawa mkuu,Kuna taratibu zake kweli.Lakini yawapasa waongozwe na busara pia
 
Back
Top Bottom