Mwenyekiti wa CCM anajulikana, kwa nini wasimtangaze tu ili kubana matumizi?

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
CCM ndio chama chenye Serikali iliopo madarakani , Serikali ambayo imewatangazia watanzania kuwa in serikali ya kubana matumizi.Tunaishauri CCM ili kuiunga mkono serikali yake imtake Mwenyekiti anayemaliza muda wake Mh.Kikwete amtangaze
Mwenyekiti mpya wa chama hicho badala ya kupeleka Wajumbe Dodoma Na kutumia fedha nyingi wakati fedha hizo zingetumika kutengeneza Madawati ya wanafunzi.Pia CCM itakuwa imeiunga mkono Serikali yake kivitendo.Kidumu chama cha mapinduzi.
 
Sera ya kubana matumizi ni ya Magufuli binafsi sio CCM, CCM sera yao ni kula bata mwanzo mwisho na kupiga madili tu. Kwanini mnaona wanaogopa sana kumpa chama Magufuli? Asilimia 90 wanaolalamika ugumu wa maisha ni CCM hao hao sio Magufuli maana wao ndio wapiga dili wakuu. Mwaka huu tutaona Lumumba wanakulana nyama wenyewe kwa wenyewe.
 
Wazo zuri sana ila kwa ccm ni tusi kubwa sana ngoja waje uwasikie mapovu yanavyowatoka utafikiri kiwanda cha mapovu
 
Mkutano wa Tarehe 23 ni zaidi ya kumchagua mwenyekiti. Agenda kuu ni kumchagua mwenyekiti lakin bado kuna agenda nyingi zitakazojadiliwa
 
Wache wakapate posho walau kidogo na kusafisha macho, hali ni mbaya sana mtaani, mifukoni kunawaka moto - Pia kumbuka lazima Justifications ziwepo; makaratasi yaonyeshe Mkutano Mkuu wa chama ulifanyika na kumchangua Mwenyekiti mpya ingawa kiuhalisia kashachanguliwa tayari na mfumo. (Kama Rais akitoka CCM ndiye atakuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi)
 
Kwa Magufuli kila goti litapigwa.

Pia hamna jiwe litakalobaki bila kugeuzwa
 
Kwa Magufuli kila goti litapigwa.

Pia hamna jiwe litakalobaki bila kugeuzwa
Kwa hiyo wewe Asubuhi unampigia magoti mungu wako Magufuli. Kweli miungu ya watu inatofautiana. Sisi wengine Mungu wetu haombewi huyu makufuli analialia aombewe kila wakati nani ampigie magoti. Kima wachache sana wa Lumumba ndo watampigia
 
CCM ndio chama chenye Serikali iliopo madarakani , Serikali ambayo imewatangazia watanzania kuwa in serikali ya kubana matumizi.Tunaishauri CCM ili kuiunga mkono serikali yake imtake Mwenyekiti anayemaliza muda wake Mh.Kikwete amtangaze
Mwenyekiti mpya wa chama hicho badala ya kupeleka Wajumbe Dodoma Na kutumia fedha nyingi wakati fedha hizo zingetumika kutengeneza Madawati ya wanafunzi.Pia CCM itakuwa imeiunga mkono Serikali yake kivitendo.Kidumu chama cha mapinduzi.
Naona ukweli wa hii hoja kwa sababu kwa vyovyote atapita tu sasa kwa nini asikabidhiwe hadi mwaka 2017 ambapo ndo muda hasa uwa uchaguzi ndani ya ccm. hii itaokoa hela na muda pia
 
Back
Top Bottom