Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Salim Abdallah 'Try Again' amezungumza na Azam Tv kwamba, rais wa heshima wa timu hiyo Mohammed Dewji 'MO' anarudi kusajili.
Try Again amesema kuwa tayari wamefanya kikao na rais wa heshima wa Simba SC, Mohammed Dewji'MO' watasajili kwa kishindo ili msimu ujao wafanye maajabu.
"Tumeshindwa kufanya vizuri msimu huu hilo halitutoi mchezoni, tumekutana kama viongozi kwa lengo la kusawazisha makosa yetu hilo limefanyika kwa usahihi".
"Tutasajili wachezaji ambao wana njaa ya mafanikio, tutabaki na wachezaji kadhaa, kuna wengine mikataba yao imekwisha, na wengine kutokana na viwango vyao tutawaaga, lakini nawapongeza wachezaji wetu wamepambana kweli kweli".
"Na kwa sasa tunafanya mchakato wa kupitia CV ya makocha waliotuma maombi na baada ya kumpata atakayekuwa sahihi kabla ya msimu huu haujaisha atapewa nafasi ya kutoa mapendekezo ya usajili na tutaanza bila kuchelewa ili tuendane na mbio za maandalizi mazuri ya mwanzo wa msimu 'Pre Season". amesema Try Again
Wakati huo huo Try Again alitaja sababu zilizomuondoa Kocha Pablo Franco Martin kuwa ni kushindwa kufikia malengo ya klabu, kutwaa taji la Ligi Kuu, Kombe la Azam Sports Federation Cup, Klabu Bingwa Afrika hatua ya Nusu Fainali, ambayo yalikuwa kama sehemu ya makubaliano ndani ya mkataba.