Mwenye simulizi za Willy Gamba anisaidie

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
892
1,709
Habari bandugu,

Nakumbuka wakati niko shule ya awali kulikua na simulizi ambazo zilisisimua sana za Willy Gamba mpelelezi maarufu huyu, naomba mwenye nazo au anaejua zinako patikana anijuze. Story kama zile zikitengenezewa Movie tena ya kiswahili. Aisee tutafika pahala shida kubwa hawa Bongo Movie wetu wamebaki kujikomba kwa matajiri na wadada kujiuza tu halafu leo wanaandamana tuache kununua kazi za nje eti tununue zao.
 
Ni Riwaya za kipelelezi za Aristablus Elvis Musiba huku main character katika simulizi zile akiwa Willy Gamba (Mpelelezi mashuhuri ulimwenguni).

Kuanzia Hujuma,Njama,Kikosi cha kisasi nk ni moja kati ya riwaya zake za kuotea mbali.Softcopy za vitabu hivyo havipatikani kiurahisi kutoka na teknolojia pamoja na ujanjaujanja wa Wabongo.

Badala ya kuhifadhi maandishi ya waandishi nguli (Musiba, Agoro, Mtobwa, Kezilahabi nk), basi ndiyo kwanza wanashusha neti na kukoroma huku wakiendeleza maandishi za waandishi uchwara na simulizi zao za mapenzi.

Sina pa kukueleza pa kupatia maandishi ya Musiba Mkuu.Ukipata pa kuazima itakuwa jambo la msingi ila sidhani kama kuna sehemu wanaviuza hivyo vitabu.
 
Mimi majuzi,nilikutana na mtu anauza Ubungo... Ni VYA CHINAKICHINA ! Vina makosa ya uchapishaji lukuki,tuma gharama ya ya kusafirisha nikutumie NJAMA !
 
Nina matoleo yafuatayo ambayo nimeyatunza kwa uhakika: Njama, Kikosi cha kisasi, Kikomo, Hofu, roho mkononi n.k...ni zaidi ya riwaya hasa kwa wenye idea za upelelezi
 
Nilikisubiriaga HUJUMA lakini sikupata kukiona,sijui mtunzi alichoka kuandika,wakavumisha eti serikali imekipiga marufuku.
Kitabu cha kwanza kukisoma nikiwa darasa la pili ni KIKOMO,tangia hapa sijaacha kusoma riwaya,japo nili upgrade kusoma Novel hivi vya kiswahili havinisisimui tena
 
Nilikisubiriaga HUJUMA lakini sikupata kukiona,sijui mtunzi alichoka kuandika,wakavumisha eti serikali imekipiga marufuku.
Kitabu cha kwanza kukisoma nikiwa darasa la pili ni KIKOMO,tangia hapa sijaacha kusoma riwaya,japo nili upgrade kusoma Novel hivi vya kiswahili havinisisimui tena
 
Back
Top Bottom