Mwenye namba ya Vodacom Customer Care naomba anisaidie haraka. Huu mtandao wa ajabu sana!

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Vodacom umekuwa mtandao wa ajabu sana. Huduma ya msingi kama M-Pesa mtu ana shida anataka aongee na mhudumu moja kwa moja tena haraka, nyie mnaturekodia kijikatuni chenu kinaongea mambo yake. Halaf kikimaliza kuropoka simu inakata.

Mbona zamani ilikuwa rahisi?

Mimi nimetuma hela (tena hela kubwa tu) niliyemtumia anasema bado hajaipata na mimi pia message ya muamala haijaja mpaka sasa, napiga kwenu mnanipa miongozo iliyokaririwa kwenye simu.

Eti kinakuambia 'Futa message kwenye simu ndio utaletewa message ya muamala simu itakuwa imejaa'

Mmeambiwa natumia Itel inayojaa message tatu? Are you serious? Hamna siku mmenichefua kama leo. Na ole wenu pesa yangu ipotee.

Ndugu naombeni namba ya hawa binadamu. Usiniambie 100 maana ndio niliyopiga.
 
Wakuu hio 100 inajulikana hata aliezimia anaijuaa...
Sio Vodacom peke yake, mtandao wowote piga 100.
Piga hii namba 100. Wakikuuliza umetoa wapi namba zao waambie nimekupa mimi.
Ndio niliyotumia na matokeo yake nataka kuongea na mhudumu moja kwa moja...
Wao wamenirekodia ka katuni kao kanaongea km vile vispika virivyorekodiwa vinatangaza dawa ya panya na virobotooo nakat m hela inapotea hii....

Ndugu tuwe serious....

Hawa jamaa nitawashtaki....hii hela ikipoteaa

Yaani hapa nilikua na safari ila nimeiahirishaa maana sielewe naweza gogwa na gari.....
Nazuguka tu hapa chumbani....
 
Wakuu hio 100 inajulikana hata aliezimia anaijuaa... Ndio niliyotumia na matokeo yake nataka kuongea na mhudumu moja kwa moja...
Wao wamenirekodia ka katuni kao kanaongea km vile vispika virivyorekodiwa vinatangaza dawa ya panya na virobotooo nakat m hela inapotea hii....

Ndugu tuwe serious....

Hawa jamaa nitawashtaki....hii hela ikipoteaa

Yaani hapa nilikua na safari ila nimeiahirishaa maana sielewe naweza gogwa na gari.....
Nazuguka tu hapa chumbani....
Piga hiyo namba utafika kuongea na mhudumu. Chagua kipengele cha MPESA au kipengele chochote ambao utaweza kuongea na mteja.

Halafu pesa haipotei kirahisi hivyo, hadi ipotee ni hatua ndefu ni suala la muda utaona hela yako.
 
Ukitaka kujua ni wakingese, weka salio la buku alafu usijiunge na usitumie cm kabisa.. Baada ya masaa matatu tizama salio lako uone km hujakuta 602.
 
Acha kujipa shida na michango ya juu hiyo wanayokwambia upige 100.
.
Fanya hivi ingia hapa Www.vodacom.co.tz ikishafunguka click palipoandikwa we're online anza kuchati na Tobi kisha bonyeza msaada zaidi atakuja muhudumu halisi ambaye atakusaidia very fast na utawakubali wakiona hamuelewani wanakutwangia simu muda huohuo.
.
Utakuja kunishukuru
Khaligraph
 
Hiyo mikampuni ya outsource ni ya kipumbavu sana yanapunguza wafanyakazi halafu wanatengeneza kitu inaitwa IVR ndio hicho kikatuni
 
Acha kujipa shida na michango ya juu hiyo wanayokwambia upige 100.
.
Fanya hivi ingia hapa Www.vodacom.co.tz ikishafunguka click palipoandikwa we're online anza kuchati na Tobi kisha bonyeza msaada zaidi atakuja muhudumu halisi ambaye atakusaidia very fast na utawakubali wakiona hamuelewani wanakutwangia simu muda huohuo.
.
Utakuja kunishukuru
Khaligraph
Kaka ubalikiwe sana sanaaaaa
Nimefanikiwa maana mara ya kwanza nilipitia huku tukashindwana
Screenshot_2020-01-05-19-36-49.jpeg
Screenshot_2020-01-05-19-36-27.jpeg
Screenshot_2020-01-05-19-36-38.jpeg
Screenshot_2020-01-05-19-39-06.jpeg
 
Attachments

  • Screenshot_2020-01-05-19-36-27.jpeg
    Screenshot_2020-01-05-19-36-27.jpeg
    36.4 KB · Views: 27
Nimefanikiwa
Ila bado siwapi sifa yoyoteee..
Namba zote kuanzia 100 mpk hizo nyingne hakuna hata moja unayoweza ongea nao direct..

Sasa kwa njia hii itakuwaje kwa mtu asiweza ingia mtandaoni?
 
Back
Top Bottom