Mwenge huu si ule wa Nyerere

Mwenge huu si ule wa Nyerere

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Jana, nikiwa naelekea Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe kwenye shauri,nilikuta magari na pikipiki zimejazana barabarani. Ni saa mbili asubuhi.Ilikuwa ni katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Minaki. Kulikuwa na askari wa kutosha ambao walikuwa wakiyaongoza magari yapite upande uliobaki wa barabara kuelekea na kutoka Kisarawe. Kumbe ilikuwa ni sherehe za mbio za Mwenge.

Ngoma zilikuwa zikirindima hadi barabarani.Nilichokiona ni kwamba wahusika wa mbio hizo ndio waliokuwa wengi. Wananchi walikuwa wa kuwahesabu na wasio na shauku yoyote. Hadi viwanja vya Mahakama ya Wilaya Kisarawe,ilisikika mbiu ya kuwataka wananchi wajipange barabarani ili waweze kuushangilia mwenge wa Uhuru. Gari la matangazo lilichagiza rai hiyo kwa kuusifu na kuupigania kwa kujivunia mwenge huo.

Lakini,wananchi hawakujipanga (labda katika maeneo ambayo sikuyaona) barabarani kama walivyoombwa. Wengi walikuwa wakiendelea na shughuli zao za kila siku. Kimsingi,waliukacha wito wa kuushangilia mwenge na kuusifu. Niseme tu kwamba,mwenge wetu sasa haushangiliwi na kusifiwa kama mwanzo. Haupewi kipaumbele na wananchi kwa kuusifu na kujazana kwenye sherehe zake. Mambo sasa yamebadilika. Si kama enzi za Hayati Mwalimu Nyerere.

Wananchi hawautaki mwenge??
 
Mh!!! wewe kijana temea mate chini .. eti condom? zimefanyaje hizo
 
Back
Top Bottom