Mwendokasi waache kuibia abiria

Mwendokasi waache kuibia abiria

Tyupa

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
802
Reaction score
657
Mamia kwa mamia ya abiria wanaochukuliwa na mabasi ya mwendo kasi kutoka Mbezi Luis kwenda mjini kwenye shughuli za ujenzi wa taifa wote huteremshwa Kimara terminal halafu tena mabasi hayo hayo au mengine huanza kuwapakia tena kwa nauli nyingine kwenda mjini.

Haijajulikana hasa sababu kubwa ya kuwatesa abiria na kuwapotezea muda wao mwingi kwa kuwashusha na kuwapakia tena.

Hata hivyo abiria wengi wameshagundua kuwa wahusika akili yao yote ni kupata hela zaidi kutoka 650/= na ile ya 400/= na kuwa 1050/=.

Kama shida ni hela kwanini isihalalishwe ili abiria wasiwe wanasumbuliwa na kupotezewa muda wao kwa kuruhusu ruti ya moja kwa moja kwenda mjini? Na ile ruti ya mjini kwenda Kimara nayo iwe ya moja kwa moja hadi Mbezi.

Tunaomba viongozi wenye dhamana sio mhusika na hii UDART waliangalie hili kwa makini kwani linatia aibu kubwa kwa sababu linaondoa dhana yote ya mwendokasi kuwa kero iliyokubuhu.
 
wanajiona wajanja hivi magari ya muhimbili yapogo?
 
kama nauli ya kwenda mjini ni 800 kwa wenye kadi kwanini kusiwe Na tiketi za 800 toka mbz kwenda mjini au mjini kwenda mbezi

kwanini iwe lzm kukata tkt tena kmr?
 
Mkurugenzi mtendaji bwana Kusena tunaomba majibu kwa nini abiria wanalazimika kukata tiketi mara mbili? Halafu tunakuomba uje Mbezi Luis uje ujionee mwenyewe jinsi abiria wanavyoteseka.
 
Inabidi waweke mabasi ya express na ticket special kwa ajili ya mbezi to town
 
Mamia kwa mamia ya abiria wanaochukuliwa na mabasi ya mwendo kasi kutoka Mbezi Luis kwenda mjini kwenye shughuli za ujenzi wa taifa wote huteremshwa Kimara terminal halafu tena mabasi hayo hayo au mengine huanza kuwapakia tena kwa nauli nyingine kwenda mjini.

Haijajulikana hasa sababu kubwa ya kuwatesa abiria na kuwapotezea muda wao mwingi kwa kuwashusha na kuwapakia tena.

Hata hivyo abiria wengi wameshagundua kuwa wahusika akili yao yote ni kupata hela zaidi kutoka 650/= na ile ya 400/= na kuwa 1050/=.

Kama shida ni hela kwanini isihalalishwe ili abiria wasiwe wanasumbuliwa na kupotezewa muda wao kwa kuruhusu ruti ya moja kwa moja kwenda mjini? Na ile ruti ya mjini kwenda Kimara nayo iwe ya moja kwa moja hadi Mbezi.

Tunaomba viongozi wenye dhamana sio mhusika na hii UDART waliangalie hili kwa makini kwani linatia aibu kubwa kwa sababu linaondoa dhana yote ya mwendokasi kuwa kero iliyokubuhu.
Mbezi town parefu :kwa 650 ni loss kubwa :la msingi atakaeona gharama apande daladala za kawaida mpaka kimara then apande mwendo kasi and versa is true :nahis wanapata changamoto ya kuweka nauli special ya mbez to town au town to mbezi :itakuwa ngumu kucontrol abiria wanaopandia njiani, aliyelipa nauli ya direct au aliyelipa 650:

Labda kama raia mwema toa ushaur :ni jinsi gani wafanye kuondoa hiyo kero
 
Kusena akili yake yote ni kupiga hela swala la kumaliza kero kwake halipo,labda hayo malalamiko watoe waheshimiwa hata hivyo hakuna mheshimiwa anaehangaika kupanda mwendokasi au daladala.Shida hii itakuja kumalizwa na raisi wetu Maghufuli atakapopata fursa ya kunusa yeye mwenyewe kuwa watu wake wanapata mateso na masumbuko yasiokuwa na kipimo.Maelfu kwa maelfu ya malalamiko yanatolewa kwa mdomo na mengine kwenye masanduku ya maoni lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.Kubenea Mbunge wa Ubungo yuko mbali mno na watu wake waliompa ubunge.Aje siku moja tu Mbezi Luis au Kimara terminal ajionee mwenyewe jinsi wazee na akina mama wanavyoteseka.Wanapakiwa kwenye mabasi kwa shida kubwa halafu wanashushwa na kuanza kuahangaika upya kuyapanda magari hayo hayo tena yaliowashusha.Iwapo nauli ni ndogo ya 650/= serkali iwaongezee haraka ili mbasi yawe yanawabeba abiria moja kwa moja kutoka Mbezi kwenda mjini au mjini kwenda Mbezi.
 
Back
Top Bottom