Au ni kukosa uwezo wa menejimenti, oganaizesheni na ubunifu miongoni mwa polisi.
Ninaamini wakati umefika wakuwa na polisi wasomi wachache lakini wanaoweza kutumia mbinu za kisayansi na kiteknolojia kuendesha majukumu yao.
Ninakumbuka siku moja tulibambikiziwa kesi na mwenye hoteli mmoja marehemu kwa hivi sasa, mimi na waandishi wangu kama 6 hivi.
Doh, kikundi cha polisi 20 pale Msimbazi walikuja kuandika stetimenti zetu kwa penseli na karatasi chafu! Kweli uwezo kama ndivyo, mdogo?
Ninafikiri tumekaa na vyombo na mifumo tuliyo nayo kwa muda mrefu na tunahitaji kuifumua na kufuma upya kulingana na wakati na mabadiliko yanayoendelea kutokea ndani na nje ya nchi.