Mwelevu uijenga nyumba yake, lakini --------...!

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
SIFA MUHIMU ZA KUZINGATIA UTAFUTAPO
MTU WA KUISHI NAYE




MARA nyingi vijana hupata taabu sana katika
suala la kuchagua mchumba. Vijana wa kiume
ndio hasa hupata wakati mgumu zaidi kwani
jamii imewapa wajibu wa kuanzisha
mazungumzo yahusianayo na mapenzi. Hata
hivyo, vijana wa kike nao wanao wajibu wa
kuchagua ili kuhakikisha kuwa hawaanguki
mikononi mwa mabazazi wa kuwalaghai na
kuwatumia kwa raha za miili yao kisha
kuwaacha kwenye mataa.
Ni jambo la kawaida kwa vijana walio wengi,
wawe wa kike au wa kiume, kuangalia sura na
mwonekano wa mtu. Lakini unapotafuta
mchum ba kwa malengo ya kuishi naye
maisha yako yote kama mume na mke
haipendezi kuangalia tu mwonekano, maana
Waswahili husema si kila king’aacho ni
almasi. Kwa sababu hiyo, hapa yatabainishwa
mambo muhimu ya kuangalia na kuzingatia
katika suala hili.
1. UADILIFU
Pamoja na sifa zote za uzuri zinazoweza
kubainishwa na kufanywa kuwa vigezo vya
uzuri wa mwanamke na mwanaume na hata
zikatumiwa kumpata Miss au Mr Tanzania,
sifa kuu impasayo mtu anayefaa kuwa
mchumba kuwa nayo ni sifa ya uadilifu.
Mtu anapokuwa na uadilifu (pengine uaminifu)
, maana yake ni kwamba tabia ya mtu huyu
anayoionesha nje ndiyo tabia yake halisi na
anapofanya jambo jema analifanya kwa roho
yake na si kwa unafiki.
Mtu anapokuwa mwadilifu ataheshimu maadili
na kufanya wema, hata pale inapokuwa rahisi
kwa wengine kukengeuka na kufuata njia za
mkato ambazo mara nyingi si za halali.
Mtu mwadilifu pia huwa na sifa za ukweli na
kujitolea kuwasaidia watu wengine bila kujali
faida – haya yote ni mambo muhimu ambayo
mtu mwenye kuwa nayo huwa na msingi wa
ujenzi wa uhusiano imara na wa kudumu.
Watu wanaoweza kujivunia furaha ya kweli
katika maisha yao ya ndoa, ni watu ambao
wamekutana wote wakiwa na sifa ya uadilifu
ambayo hujumuisha mambo mengi.
Zipo ndoa nyingi zenye furaha ya bandia.
Furaha hii mara nyingi hutokana na ridhiko la
kimwili alipatalo mtu kutokana na kukidhiwa
kwa mahitaji yake ya kimwili yanayohusiana
na haki za msingi za binadamu – yaani
chakula, mavazi na malazi. Lakini furaha ya
kweli ya maisha ya ndoa, watu hawaipati
isipokuwa katika uhusiano ambao wenza
wamethibitishana kuwa waadilifu.
2. HEKIMA
Mtu mwenye uadilifu wa kweli, mbali na kuwa
mwema kwa mwenzake, pia huhakikisha
anakabiliana kwa busara na hekima na
matatizo yote yanayoweza kusababisha
kuyumba kwa uhusiano, hususan yale yaliyo
nje ya uwezo wake.
Uzoefu unaonesha kuwa wapenzi, hususan
wanandoa walio katika uhusiano wa muda
mrefu wanaoendelea kufurahia unyumba wao
si wale ambao walipendana kwa mvuto na
wala hawana mambo mengi ya asili
yanayowaunganisha kuliko wale
wanaotengana. Lakini la muhimu ni kwamba
watu hawa huwa wamejifunza jinsi ya
kukabiliana kwa hekima na matatizo
yanayojitokeza, hususan yale yanayotokana
na tofauti zao kimtazamo.
Ukiachilia mbali sifa ya uadilifu, watu hawa
huwa wamejifunza kukabiliana na matatizo
kuhusiana na uzazi na ulezi wa watoto,
uhusiano na ndugu, jamaa na marafiki, suala
la ngono, fedha na maisha ya unyumba kwa
ujumla.
Habari njema ni kwamba uadilifu na hekima ni
mambo ambayo mtu yeyote anaweza kujifunza
na kisha kufanyia kazi. Ndiyo maana
wanandoa hufundishwa kabla ya ndoa na hata
wanapokuwa tayari wameoana huendelea
kuhudhuria semina za kidini na kijamii kwa
ajili ya kujiimarisha.
Kwa hiyo, kama mume/mke wako mtarajiwa
anaonekana kuwa na utayari wa kujifunza
kuhusiana na jinsi ya kuishi na mtu wa jinsia
nyingine, ana nafasi kubwa ya kuwa mke/
mume mzuri baadaye.
3. UPOLE
Mfalme Suleiman katika mojawapo ya semi
zake za hekima alisema mwanamke
-------- huibomoa nyumba yake kwa
mikono yake. Yamkini ndivyo ilivyo pia kwa
mwanaume --------, maana upumbavu
haujengi.
Siku zote kitu kinachovunja uhusiano wa
kindoa si makombora ya nyuklia, bali ni ulimi.
Kwa kadri mtu anavyoutumia ulimi wake
anaweza kuijenga au kuibomoa nyumba yake.
Katika kumwangalia mtu ambaye unaweza
kujenga naye nyumba ya kudumu, ni vema
kumchunguza na kuhakikisha kuwa si mtu
mwenye kupenda kurefusha maneno, maana
hakika huyu atasababisha ugomvi mara kwa
mara na uhusiano hautadumu.
Wapo watu ambao ndoa zao zina sifa ya
ugomvi na karibu kila mtu anafahamu na hata
wamekuwa kero kwa ndugu, jamaa na
majirani zao, mara kwa mara wakiwaamsha
watu usiku wa manane wakitafuta suluhu.
Mara nyingi wanaume ndio huanzisha ugomvi,
lakini ugomvi huwa na nguvu zaidi kama
mwanamke ni msemaji. Dawa ya kuzuia
ugomvi usiokuwa na mpango ni kupunguza
maneno na kuepuka kutafuta ushindi katika
ubishi. Lakini kinga ya tatizo hili ni kuepuka
kujiingiza katika uhusiano na mtu ambaye
umejihakikishia kuwa si mwingi wa maneno.
Bahati nzuri, jamii huwatambua wanawake/
wanaume ambao wanaweza kuwa wake/
waume bora baadaye kwa hiyo ni wajibu wa
mtafutaji kuhakikisha kuwa anafanya
uchunguzi wa kina kabla ya kujitosa kwa mtu
ambaye baadaye atamtaabisha.
Mwanandoa aliyeifahamu vema dhana ya
ndoa – kwamba ni maisha ya kuvumiliana na
kuchukuliana, hufahamu ni wakati gani wa
kusema na wakati gani wa kukaa kimya. Mtu
huyu pia hufahamu njia nzuri na salama ya
kujiondoa kwenye tatizo anapoona mwenzake
anaelekea kubaya, ili hatimaye uhusiano wao
uendelee kuwa salama japo wao wanaweza
kuwa wamekwaruzana.
Mtu huyu mwenye upole hujiweka katika mkao
wa upatanishi na huhakikisha kuwa kila
mjadala mkali unapita na kumalizika salama.
Ni wazi kuwa katika kutafuta, kama
hukukurupuka, utamwona mtu mwenye hulka
hii – upole.
4. MVUTO
Hisia za mvuto wa kimapenzi ni muhimu
katika kujenga uhusiano. Mtu mmoja akauliza,
ni yupi bora – yule anayenivutia sana au yule
anayenipenda sana? Maisha ni ya ajabu sana.
Huwa inatokea kuwa mtu unayevutiwa naye
sana yeye havutiwi nawe, bali anavutiwa na
mwingine ambaye naye hana mpango naye!
Haya ndiyo maisha. Uzoefu unaonesha kuwa
asilimia kubwa ya watu walio katika ndoa
hawajawaoa/kuolewa na watu waliokuwa
wakiwapenda sana enzi za ujana wao, au wale
waliotimiza ndoto za ujana wao. Bahati njema
miongoni mwa wanandoa hawa wapo wale
wenye ndoa imara sana.
Mvuto wa kimapenzi ni muhimu sana, lakini
watu husema maji yakisema usininywe yajibu
kuwa wewe pia huna kiu nayo. Japo inaweza
kuonekana kama ni aina ya ‘sizitaki mbichi
hizi’ lakini si vema kujisumbua na mtu
asiyekupenda.
Badala ya kujihangaisha na mtu
asiyekupenda, kaa chini na umsubiri
anayekupenda hata kama huhisi kuvutiwa
naye sana. Baadaye utamzoea na maisha
yatakuwa mazuri, kisha utajiuliza baadaye
yule aliyekuringia alikuwa na nini cha ziada?
Lakini iwapo mambo mengine yote
yatakwenda sawa, ni vema na muhimu kabisa
kuhakikisha kuwa mtu unayepanga kuwa naye
maisha yako yote ni mtu anayekuvutia kimwili
na kiakili, maana vinginevyo unaweza kupata
sababu ya kukidhi kiu yako nje – jambo
ambalo si maadili mema katika ndoa na
maisha.
NI MUHIMU KUWA MAKINI
Katika nyakati za ujana, watu wengi
hubabaishwa kwa mengi. Vijana wa kiume
hubabaishwa na sura, maumbile na pengine
rangi na kusahau mambo muhimu yaundayo
orodha ya sifa za mke mwema.
Kwa upande wao, vijana wa kile pia waweza
kubabaishwa na pesa, maumbile, sura,
utanashati, umaarufu au kuchoshwa na
shinikizo la umri, hivyo kujikuta
wakijitumbukiza kwa wanaume wasio na sifa
za waume wazuri.
Lakini tukirejea kwenye msemo wa zamani
kuwa uzuri si hoja bora tabia, ni wazi kuwa
tutafikia mahali tutajenga mahusiano imara
na yasiyotikiswa na sunami zozote za
kimaisha. Ilimradi tu uhakikishe kuwa mtu
mwenyewe anakupa mvuto kimapenzi, maana
vinginevyo kutakuwa hakuna maana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…