Matukio ya hivi karibuni yanayozunguka utendaji wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kauli zilizotolewa na viongozi wakuu wa nchi kuhusu mwenendo wake, zimeibua shauku kubwa kuhusu hatima ya kiongozi huyo kijana.
Sasa kuna dalili kuwa ile hali ya kumwagiwa sifa na Rais John Magufuli, iliyochangia kung’arisha nyota yake, imebadilika.
Wachambuzi wa mienendo ya siasa za Tanzania wanasema, kitendo cha Rais Magufuli kuagiza hadharani makontena ya Makonda yalipiwe ushuru ni dalili za kumchoka mteule wake.
“Umesikia hili sakata la Dar es Salaam, eti Mkuu wa Mkoa ameleta makontena, ameambiwa alipe kodi, kwa nini asilipe kodi"? Alihoji Rais Magufuli.
Kabla ya kauli hiyo ya rais, tayari Makonda alikwishaandika barua kwa Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango na barua yake kuvuja kwa bahati mbaya? akitaka vifaa hivyo visamehewe kodi.
Baada ya TRA kusisitiza kuuza makontena hayo Makonda alitahadharisha kuwa atakayeyanunua atalaaniwa na Mungu.
Siku moja baada ya kauli hiyo, Dk Mpango aliagiza yapigwe mnada akisema, “Kamishna piga mnada mara ya kwanza, ya pili na ya tatu kadri sheria inavyoruhusu. Hata mimi ningekuwa na hela ningekuja kununua tuone hiyo laana itatoka wapi.”
Wachambuzi wanadai kuwa ujasiri wa Dk Mpango dhidi ya Makonda, hata kama alikuwa anasimamia sheria haukuwa wa kawaida.
Kuna makada mbalimbali wa CCM nao wamejitokeza hadharani kupinga uongozi wa Makonda.
Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally alikaririwa akisema Makonda alipaswa kuwashirikisha wenzake tangu hatua za awali, kwa kuwa Serikali ni moja, akikumbusha kuwa Dar es Salaam ni mmojawapo ya mikoa isiyotekeleza vyema Ilani ya CCM kutokana kufanya kazi bila ushirikiano.
“Na hii habari ya Dar es Salaam ya Makonda, hakuna Dar es Salaam ya Makonda, ni Dar es Salaam chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda.” alisema.
“Kuna wakati namsikia anasema wananchi wangu, nani kamwambia anao wananchi wake? Hakuna wananchi wako. Hakuna kiongozi anamiliki wananchi, ni wananchi wenzangu.”
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba, alipotakiwa kutoa maoni yake juu ya uongozi wa Makonda alisema, kwa sakata la makontena ni bora mlengwa akatumia busara na kujipima.
"Rais akishasema kamaliza wewe mteuliwa utumie busara kuamua, ayatafakari hayo maneno ya bwana mkubwa ambaye ndiye mwamuzi wa mwisho, akishasema lipa lazima ulipe". alisema.
Kada mwingine maarufu wa CCM na mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam Dr. Benson Bana alisema, matamshi yaliyotolewa na viongozi wenzake ni fundisho tosha ajitafakari na kupima kauli zake.
"Ingawa anafanyakazi nzuri, na kuleta maendeleo lkn lazima awe mstari wa mbele kusimamia sheria. Nadhani ameshapewa ujumbe wa kutosha sasa ajitafakari na abadilike". Bana alisema.
Chanzo: Mwananchi.
Mwanzo wa mwisho utawala wa Makonda Dar?