MWANZA: Kiwanda cha Multi Cable Limited chaungua moto

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,728
Reaction score
4,181
Kiwanda cha Multi Cable Limited kilichopo Kijereshi, kata ya Ihoma jijini Mwanza kinaungua moto muda huu harakati za kuzima ndo zinaendelea chanzo cha moto hakijajulikana.

===========



Kiwanda chote cha Multi Cable Limited kilichopo eneo la Kijereshi kata ya Igoma jijini Mwanza ,kimeteketea kwa moto leo.

Kiwanda hicho kimeanza kuwaka saa nne mchana kutokana hukuchanzo kikibainika ni hitilafu ya nguvu za umeme.

Kiwanda hicho cha Multi Cable Limited kinajihusisha na utengenezaji wa nyaya za umeme na bomba za kupitisha nyaya hizo.

Mmoja kati ya wafanyakazi wa kiwanda hicho, anasema wao walishtukia moshi ukiwa unatokea kwenye 'store' wakagundua kwamba ni nyaya zimegusana kwenye paa na kusababisha moto huo.



Mwananchi
 
Duuuh pole nyingi ziwafikie...Jitihada za kuuzima moto zifanyike kunusuru watu na mali
 
Udanganyifu wa BIMA (Insurance Fraud) ni janga la Kitaifa kwa sasa. Vyombo husika viangalie hili kwa ukaribu na umakini zaidi.
 
Udanganyifu wa BIMA (Insurance Fraud) ni janga la Kitaifa kwa sasa. Vyombo husika viangalie hili kwa ukaribu na umakini zaidi.
Wacha walipwe kama biashara zinzkufa wafanyeje. wacha wivu nawe choma yako ulipwe
 
Wacha walipwe kama biashara zinzkufa wafanyeje. wacha wivu nawe choma yako ulipwe
Tatizo la vichaa kama wewe ni kuropoka bila kujali madhara ya tatizo husika kwa ujumla.
Sidhani kama unafahamu kwa upeo wa akili yako ya kuwa kwa kufanya udanganyifu wa Bima kunasababisha kupanda kwa gharama za tuzo/jazi ya Bima (Insurance Premium) na kusababisha usumbufu kwa wateja wengine wa huduma ya Bima.
Pathetic Creature!
 
Kwanini pole isiwe kwako?
Kwani hizo kodi ni mali zake?
Matukio haya yanakwamisha Mpango Mikakati wa Mh. Rais kuanza kuzisaidia Nchi za Ulaya na kupeleka Mitumba Ulaya baada ya kuvaliwa na wa Tz!
 
Duh nimetoka post ya tashrif na huku moto tena
 
Kiwanda cha Multi Cable Limited kilichopo Kijereshi, kata ya Ihoma jijini Mwanza kinaungua moto muda huu harakati za kuzima ndo zinaendelea chanzo cha moto hakijajulikana
Kata ya IHOMA iko maeneo gani huko Mwanza?
 
Mwenyewe. Umefanya uchunguzi ukagundua wamekichoma wenyewe?.
 
Ndoto ya Tanzania ya Vi-wonder inazidi kufa,maana hata vile vichache vilivyopo vinafungwa na vingine ndio kama hivi vinaungua moto. Alietoa wazo la Tanzania ya Vi-wonder akajisafishe kwa Muumba wake kwanza inaelekea si msafi.
 
Ni wapi nilipoandika WAMEKICHOMA!!!???? Nimetoa angalizo. Wewe unakurupuka na kunilisha maneno.
Pathetic!
Unasema hujuma unamaanisha nini. Pole sana ila acha matusi pia pambana na hali yako mjumbe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…