MWANZA: Jeshi la Polisi lamkamata mfanyabiashara akiwa na madawa ya kulevya

Dionize N

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,848
3,293
Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya yanayodhaniwa kuwa heroine kiasi cha pinchi 240 na ndonga mbili.

Msangi3.JPG

DCP Ahmed Msangi - RPC Mwanza

Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa leo, imedai kuwa mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Kassim Hemed Kesi mwenye umri wa miaka 43, amekamatwa majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa Kanyerere kata ya Butimba wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza

Taarifa hiyo imedai kuwa mtu huyo ni mfanyabiashara wa spear za magari katika mtaa huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kuwa awali polisi walipata taarifa za mtuhumiwa huyo kuwa anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, hivyo askari walikuwa wakiendelea na upelelezi pamoja na uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo.

Aidha wakati askari wakiendelea na upelelezi dhidi ya tuhuma za mfanyabiashara huyo, jana tarehe 09.02.2017, polisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kwamba mtuhumiwa huyo ameingiza mzigo mkubwa wa madawa ya kulevya kutoka Dar es Salaam na ameanza kuusambaza mtaani.

SINEMA ILIVYOKUWA

Askari walianza kufanya ufuatiliaji wa haraka kuhusiana na taarifa hizo, ndipo ilipofika majira ya saa sita usiku askari walifika hadi nyumbani anapoishi mtuhumiwa na kuizingira nyumba yake yote na kumuona kupitia dirisha akiendelea kufunga madawa hayo kwenye vikete vidogovidogo maarufu kama pichi.

Wakati askari wanataka kuingia ndani ya nyumba mtuhumiwa alishtuka na kukimbiza mzigo huo wa madawa ya kulevya chooni ili kupoteza ushahidi.

Aidha askari waliona kitendo kile kupitia dirishani na baadhi YA askari waliingia ndani na kufanikiwa kukuta pinchi 240 zikiwa chooni lakini bado hazikuwa zimetumbukia shimoni na kufanikiwa kuzitoa kwenye tundu la choo.

Msangi amesema wakati huohuo askari wengine waliokuwa nje walikwenda kuvunja bomba linalopitisha uchafu/choo linalokwenda kwenye shimo na kuweka kizuizi hapo na kufanikiwa kupata ndonga 2 za dawa za kulevya huku nyingine zikibebwa na maji .

Polisi wanaendelea na mahojiano na mtuhumiwa ili kuweza kubaini mtandao wa watu aliokuwa akijihusisha nao katika biashara hiyo ya madawa ya kulevya.

Source: EATV Mtandaoni
 
Amekudanganya nani..? Ukiona wapiga debe wanaendelea kupiga debe vituoni uelewe wanaendelea kupata supply kama kawaida.. Umejifungia chumbani unasema vijiwe vimekufa..
Nipo kitaa njoo nikupeleke vijiweni...acha kuongelea chumbani
 
inamana alikuwa amepokea mzigo uliokimbizwa dar ili auuze mwanza............kumbe msako kila kona..........hili zoezi liwe endelevu...mikoani nako hali ni mbaya wasiishie dar tu wafike mikoa yote ya nchi....................
 
Hizi ndio mbinu za kuanza kupata mtandao.. Huyo mtuhumiwa akihojiwa na kutaja cheni yake hapo wataweza kumfikia mpaka bosi wao..
Sio akina makonda wanakimbilia kutangaza kwenye vyombo vya habar kutafuta kiki za kisiasa
Haya mambo ni mazuri japo sometime nayaogopaga sana. Anaweza kubanwa na mwishoni ukasikia anasema ulikuwa ni mzigo wa 'Philemoni'. Nakumbuka tu simulizi za Muhindi aliyekwenda kuungama pale Kawe nyakati zile!
 
Back
Top Bottom