Mwanini umpotezee mtu muda wakati unajua umeandaliwa mke Kijijini kwenu?

Sinoni

JF-Expert Member
May 16, 2011
6,535
11,437
Kwanini umpotezee mtu muda & gharama na thamani anayokupa huku ukijuwa fika kuwa "kijijini unapotoka una mtu uliyeandaliwa tayari"?
 
Na wengine ni wajanja tu, hapo kaamua tu kuoa kwengine ndo atakudanganya ooh nyumbani wamenitafutia mtu wa kuoa/kuolewa. Ingawa ni kweli wapo wanaolazimishwa wakaoe/kuolewa makwao, but wengi wanakuwa wanatumia tu hiyo excuse kukutosa.

Tangu upo mtoto, kuna makabila kabisa utakuwa tu unasikia sikia home wakiyaponda. Sasa hadi ufike uzeeni utakuwa hujui tu kuwa home hawataki nipeleke mtu wa kabila lingine? Na familia nyingi siku hizi wasipokutaka watatumia excuse ya kabila, tena haswa kwa mabinti. Maana wanajua binti tukimwambia hatumtaki kisa dini, kuna wengine hawakawii kubadili dini ndani ya dakika. So wanakukomesha na kabila kama utaweza kuhama kabila lako. Na kuna watu (haswa wanaume), wachumba zao wanakataliwa na wazazi lakini wanakomaa hadi misimamo yao inakubalika ( God forbid).

Mtu akikuletea mambo ya kabila, basi Mshukuru tu Mungu endelea na maisha. Huwezi kulazimisha ndoa kama mtu hataki ni hataki tu. Inauma sanaaa but jifunze tu kushukuru kwa kila jambo.
 
Wasichana bhana naona huwa mnashindwa kuelewa vitu vidogo sana, na msipokubaliana na huu ukweli intawacost always:

1. Kuanza mahuasiano si guarantee ya kuoana. Yaan wewe unataka mtu akikuapproach tu basi ajicommit kwamba atakuoa. Na ndicho wanaume wanachofanya ili akupate kwanza. No huo mtazamo ufuteni kabisa.

2. Kadri mahusiano yanavoendelea kuna kujuana baadhi ya tabia za ndani kabisa za mwenzi wako ambazo pengine you cant tell na huwezi kumbadili. Mfano: unagundua anapenda sana pesa kwa hiyo maendeleo ni ndoto, hana akili za kujenga, uchoyo(ubinafsi), maneno mengi sana(kulalamika), haridhiki or hatosheki n.k
Vitu hivi huwa nyie hamfikirii mnakimbilia kusema kaniahidi kunioa, we unafikiri siku zote tutaishi kwa maigizo, baada ya familia kwa tabia hizo si itakuwa balaa.

Mfano: Nilikuwa na msichana ambaye kwa muonekano alikuwa katulia sana. Nilimuapproach baada ya muda akakubali, mapenzi yakaanza kwa kasi na mazito hadi raha. Interesting alikuwa hajawahi kuwa kwenye mahusiano serious kama ya kwangu na ya kwake means alikuwa Bikra. Baada ya kuendelea sana nilikuja kugundua matatizo yafuatayo. Alikuwa ni Mkali kupindukia yaan anaamrisha na kufoka balaa sio kwangu but kwa wanaomzunguka. Na kuna wakati akijisahau ananifokea hata mimi ila akijishtukia napotezea. Alikuwa na kiburi kilichopitiliza. Hakukuwa na namna zaidi ya kumwacha tu kwa kumtengenezea mazingira ingawa yy hakujua kama sababu mi hizo. Future waifu ni kazi kumpata.

Acheni kulalamika mjichunguze kwanza.
 
Kama mtu hakupendi hakupendi tu na ni moja ya ishara ya ubinafsi hasa kwa wanaume maana hafikirii mtu amejitoa kiasi gani, nilishawahi kusikia mdada mmoja na huyu bwana mmoja mpk wamechukua mkopo kununua kiwanja ndo jamaa anamwambia huko kwao hawataki amuoe yeye na akaoa mwingine na mkopo ulichukuliwa kwa akaunti ya mdada. Sasa sijui kiliandikishwaje mana mahusiano mengi mwanaume huwa kama ndo mmiliki hata akigharamia mwanamke
 
Nina mtu wangu hapa binti flani hivi tuna almost mwaka na miezi tangu tuanze uhusiano ,Mwanzoni akaniambia dear mdogo wangu karudishwa shule anadaiwa ada naomba niongezee laki 5 nimekwama,nikampa hyo laki 5,sasa ikawa ndio fungulia dimba sasa ni kila week yeye kafulia tu na hapo ameajiriwa serikalini.Nikisema nihesabu hela niliotoa huwa najiuliza huyu mtu tutawezena kweli ndani??Siku ukimpa hela utaitwa majina yote mazuri ya mapenzi,Sasa juzi nimemlipia mchango wa harusi,hata cjatulia nadaiwa tena hela ya kula,nikamuahidi nitampa ila channel zimegoma sasa ile kumwambia mambo sio mazuri asubirie amenuna na tumegombana nnahisi nimdelete tu maana sitaki Gold digger mimi.
 
Sasa Kama tabia yako mbovu sijapendezwa Na wewe ulitaka nikwambiaje labda?
 
Nina mtu wangu hapa binti flani hivi tuna almost mwaka na miezi tangu tuanze uhusiano ,Mwanzoni akaniambia dear mdogo wangu karudishwa shule anadaiwa ada naomba niongezee laki 5 nimekwama,nikampa hyo laki 5,sasa ikawa ndio fungulia dimba sasa ni kila week yeye kafulia tu na hapo ameajiriwa serikalini.Nikisema nihesabu hela niliotoa huwa najiuliza huyu mtu tutawezena kweli ndani??Siku ukimpa hela utaitwa majina yote mazuri ya mapenzi,Sasa juzi nimemlipia mchango wa harusi,hata cjatulia nadaiwa tena hela ya kula,nikamuahidi nitampa ila channel zimegoma sasa ile kumwambia mambo sio mazuri asubirie amenuna na tumegombana nnahisi nimdelete tu maana sitaki Gold digger mimi.
wasiwasi ni akili mkuu..
 
Back
Top Bottom