Mwanaume akishakupata baada ya muda mfupi upendo wote wa awali hupungua

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
14,893
2,000
Hiyo ni kauli kutoka kwa baadhi ya wanawake. Je kauli hiyo ina ukweli kiasi gani? Kuna bahati mbaya moja, ambayo baadhi ya wanawake hawaijui.

Hii ni ile yakudhani kwamba, mwanaume akishaanzisha uhusiano na mwanamke au wakioana, kiwango cha kupendana kitakuwa ni kile kile milele. Lakini ukweli ambao hawaujui ni kwamba, binadamu ana hisia na hisia hizi huweza kuchoka, watu wanapokaa pamoja au wanapokuwa pamoja katika uhusiano kwa muda mrefu, hufikia mahali ambapo kiwango cha hisia za upendo hushuka kwa maana kwamba, zimechoka.

Hebu fikiria inakuwaje ndugu au jamaa yako ambaye umekuwa ukitamani aje kukutembelea kutoka mbali anapokaa kwa muda fulani kwako, zile cheche za hamu zinapungua, wala bila kukosana au tatizo lolote? Ni hisia zimechoka, hata unaponunua nguo au kiatu kizuri sana, baada ya kuda fulani, ule 'mchecheto' wa awali kukihusu,hupungua au kwisha.

Ni suala la hisia pia, si kwamba, hiyo nguo au kiatu hukipendi tena. Kama mwanamke halijui jambo hili, linapotokea, hudhani kwamba, mwenzake sasa hampendi, na ndipo hapo kauli kama: ''Mwanaume akishakupata baada ya muda mfupi upendo wote wa awali huisha'' Haya ni malalamiko ya wanawake katika kujaribu kuonyesha ushahidi wa hali hii.

Wanashindwa kujua kwamba, kabla ya kuanzisha uhusiano au kuoana, hisia zilikuwa bado ziko juu, kwa sababu bado watu hawa walikuwa hawajaanza kuwa pamoja kwa muda mwingi Ni mwongo anayeweza kusema kwamba, katika mahusiano yake au ndoa yake hajawahi kuhisi hisia za upendo kwa mwenzake kushuka angalau kidogo.

Kuna kutofautiana tu katika viwango vya kushuka kwa hisia hizo. lakini kila binadamu hisia zake za upendo hushuka. Kuna sababu nyingi zenye kufanya kiwango cha hisia za upendo kushuka lakini kubwa huenda ni maumbile, sababu nyingine ni uwezo wa kila mmoja kubadilika kufuatana na mazingira, uwezo wa kutenda na kutoa kauli nzuri kwa mpenzi wake katika mahusino.

Lakini pia utayari kwa kila mmoja kuondoa zile tabia ambazo mwenzake anasema zinamkera. Kushuka kwa hisia za upendo hakuna maana ya kuondoka kwa upendo. Upendo unapoondoka umeondoka, lakini hisia za upendo zinaposhuka zinaweza kurudishwa na hali ikarejea kama zamani tu. wakati mwingine hurudi zenyewe kama zilivyopotea. Lakini wapo baadhi ya wanawake hisia za upendo za wenzi wao zinapopotea, hubabaika na kuharibu mambo.
 

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
173,998
2,000
Wanawake wengine wanalazimisha mapenzi matokeo yake ndo hayo kuwa kwenye uhusiano mgumu. Wengine usafi siku ya kwanza baada ya hapo anajisahau. Asilimia kubwa ya wanawake wanakutana na wachafuzi tu huku wao wakidhan ni waoaji.
 

mensaah

JF-Expert Member
Sep 12, 2016
985
1,000
Tatizo lenu ni wasumbufu sana

hasa wakati mnafatiliwa unamsumbuwa mwanaume mpaka anachoka ,unakuja kukubali mwanaume hisia zishakufa,

na akija kukuiona ulichokuwa unamsumbulia hakina lolote ndo kabisaaaaaaaa humuoni tena unabaki unahangaika
Mkuu uko sahihi 100% yaan uzungushwe were utadhan ni deni mpaka siku anakubali hisia juu yake zilishaisha so kilichobaki unapita na 120 speed
 

sumbai

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
15,157
2,000
Ndio maana haitakiwi kuwa expect too much from your partner......ukiwanayo hiyo lazima umchoke tuuuu

Haitakiwi kurelax baada ya kuingia kwenye uhusiano, inasababisha kuchokana.......ndio maana unatakiwa uwe mbunifu deile....
Lazima mwanamke uwe msafi, ujipambe....... Outing saaana na vacations.

Mentality ya kuridhika na kuapreciate kitu from your partner Ni muhimu,
 

Allen Alfred

JF-Expert Member
Nov 22, 2015
832
1,000
Hapa mimi nafikiri hili jambo la kuchokana na hisia kupungua ama kushuka liko pande zote mbili sema linaonekana zaidi kwa upande wa wanawake kwa sababu wameumbwa kuwa watu wa kusema tofauti na wanaume walio wengi huwa wanayahifadhi tu vifuani mwao.
Unaweza kumfanya mwenza wako akakupenda kama mwamzo kils siku yako kwa kuwa mtu mpya kila siku yako,mtoto wa kike/ kiume kuwa mbunifu,sasa wewe unakuta mwanamama ana tumbo kuubwaa yaan hata ile hamu ya kumtizama hakuna,mwanamama muda wote uko ndani ya matenge tu weka vazi flan wakati flan ili mumeo aone na atamani kukuangali,yaan akikuona mate ya hamu na mawazo juu yako yawe makubwa (samahani kama ntakuwa nmekosea kiswahili)!!
Mwanamama mume anarudi nyumbani we umejinyoosha tu sebuleni hapo,anaingia unamuangalia tu hata kusema umpokee kwa mahaba na huba waaapi,sasa hayo mapenz yake kwanini yasipungue wakati akikaa na wenzie huko anasikia wanayofanyiwa na wake zao.
Mwanamama mchezo tu wenyewe mpaka mpigane roba daah jamani,wacheni hizo asee!!!
Miongoni mwa vitu nnavyovijua kuhusu mapenzi ni kwamba hakunaga kitu kidogo katika mahusiano ya kimapenzi
 

KARANJA 007

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
6,011
2,000
nini kifanyike sasa
Hakuna cha kufanyika mamii,inabidi kuvumiliana tu na kulea watoto baaas,ukianza ooooh baby i love you oooh baby mbona siku hizi huninyoi mazivu,oooh baby siku hizi huniletei coffee kitandani nikiamka? oooh baby mbona siku hizi hunibebi mgongoni kunipeleka kwenye bath tub kuniogesha? oooh baby mbona siku hizi huninyonyi nanihiii kabla hujaenda kazini? ,basi ujue ukizidisha hayo maswali kwa baby wako,daah utatupwa na ataanza kurudi usiku wa manane alewa tooop na tayari kaisha pewa dog style na Esther wa Corner Bar,tena machakani,ukitaka usalimike kuwa mpole na usiwe na maswali mengi,hapo huruma itamjia na ataamka kiakili na kugundua nyama ni ile ile tu,tofauti mapishi au vipi?,kama una swali zaidi njoo PM,nakuahidi sikutongozi kabisaaaaa ila nitakupa somo mujarrab.
 

ContinousImprovement

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
289
500
Hiyo ni kauli kutoka kwa baadhi ya
wanawake.

Je kauli hiyo ina ukweli kiasi gani?

Kuna bahati mbaya moja, ambayo baadhi
ya wanawake hawaijui.

Hii ni ile yakudhani
kwamba, mwanaume akishaanzisha
uhusiano na mwanamke au wakioana,
kiwango cha kupendana kitakuwa ni kile
kile milele.

Lakini ukweli ambao hawaujui ni kwamba,
binadamu ana hisia na hisia hizi huweza
kuchoka.

watu wanapokaa pamoja au
wanapokuwa pamoja katika uhusiano kwa
muda mrefu, hufikia mahali ambapo
kiwango cha hisia za upendo hushuka kwa
maana kwamba, zimechoka.

Hebu fikiria inakuwaje ndugu au jamaa
yako ambaye umekuwa ukitamani aje
kukutembelea kutoka mbali anapokaa kwa
muda fulani kwako, zile cheche za hamu
zinapungua, wala bila kukosana au tatizo
lolote?

Ni hisia zimechoka, hata unaponunua nguo
au kiatu kizuri sana, baada ya kuda fulani,
ule 'mchecheto' wa awali
kukihusu,hupungua au kwisha.

Ni suala la
hisia pia, si kwamba, hiyo nguo au kiatu
hukipendi tena.

Kama mwanamke halijui
jambo hili, linapotokea, hudhani kwamba,
mwenzake sasa hampendi, na ndipo hapo
kauli kama:

''Mwanaume akishakupata baada ya muda
mfupi upendo wote wa awali huisha''
Haya ni malalamiko ya wanawake katika
kujaribu kuonyesha ushahidi wa hali hii.
wanashindwa kujua kwamba, kabla ya
kuanzisha uhusiano au kuoana, hisia
zilikuwa bado ziko juu, kwa sababu bado
watu hawa walikuwa hawajaanza kuwa
pamoja kwa muda mwingi

Ni mwongo anayeweza kusema kwamba,
katika mahusiano yake au ndoa yake
hajawahi kuhisi hisia za upendo kwa
mwenzake kushuka angalau kidogo.

kuna
kutofautiana tu katika viwango vya kushuka
kwa hisia hizo.

lakini kila binadamu hisia
zake za upendo hushuka.

Kuna sababu nyingi zenye kufanya kiwango
cha hisia za upendo kushuka lakini kubwa
huenda ni maumbile, sababu nyingine ni
uwezo wa kila mmoja kubadilika kufuatana
na mazingira, uwezo wa kutenda na kutoa
kauli nzuri kwa mpenzi wake katika
mahusino.

lakini pia utayari kwa kila mmoja
kuondoa zile tabia ambazo mwenzake
anasema zinamkera.

Kushuka kwa hisia za upendo hakuna
maana ya kuondoka kwa upendo. Upendo
unapoondoka umeondoka, lakini hisia za
upendo zinaposhuka zinaweza kurudishwa
na hali ikarejea kama zamani tu.

wakati
mwingine hurudi zenyewe kama
zilivyopotea.

Lakini wapo baadhi ya wanawake hisia za
upendo za wenzi wao
zinapopotea,hubabaika na kuharibu mambo.
Hili ni tatizo. Mnakariri. Kupendwa kwa kumaanisha kunaongezeka zaidi pale mnapokutana kimwili.

Wewe unaweza dhani amekusahau, Kumbe amegundua wewe ni spender, so kaamua kuwekeza pesa iliyopo Leo, ili Kesho hela ya kuspend isitoke kwenye savings account.

Wanawake hamrithiki.
 

chuganian

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
1,075
2,000
Hakuna cha kufanyika mamii,inabidi kuvumiliana tu na kulea watoto baaas,ukianza ooooh baby i love you oooh baby mbona siku hizi huninyoi mazivu,oooh baby siku hizi huniletei coffee kitandani nikiamka? oooh baby mbona siku hizi hunibebi mgongoni kunipeleka kwenye bath tub kuniogesha? oooh baby mbona siku hizi huninyonyi nanihiii kabla hujaenda kazini? ,basi ujue ukizidisha hayo maswali kwa baby wako,daah utatupwa na ataanza kurudi usiku wa manane alewa tooop na tayari kaisha pewa dog style na Esther wa Corner Bar,tena machakani,ukitaka usalimike kuwa mpole na usiwe na maswali mengi,hapo huruma itamjia na ataamka kiakili na kugundua nyama ni ile ile tu,tofauti mapishi au vipi?,kama una swali zaidi njoo PM,nakuahidi sikutongozi kabisaaaaa ila nitakupa somo mujarrab.
asante sana
 

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,012
2,000
Tatizo wakitoa penzi sasa wanakugeuza kama ATM yao!Kabla ya kukupa penzi mizinga huja kwa step step sana lkn akikupa sasa wewe ndiyo bank yake inakua!
Hapo unapiga unakimbia kuokoa pesa zako
 

jechalism

JF-Expert Member
Nov 11, 2016
259
250
Tatizo lenu ni wasumbufu sana

hasa wakati mnafatiliwa unamsumbuwa mwanaume mpaka anachoka ,unakuja kukubali mwanaume hisia zishakufa,

na akija kukuiona ulichokuwa unamsumbulia hakina lolote ndo kabisaaaaaaaa humuoni tena unabaki unahangaika
Very true mkuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom