Majighu2015
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 2,936
- 3,958
Wapinzani wapo ili kuweza kuisimamia serikali kufanya kazi zake vizuri. Mwl. Nyerere alihakikisha upinzani unakuwepo pamoja na kwamba alikua chama tawala kwa sababu alielewa faida ya upinzani kuwepo nchini.
Tumeshuhudia ufisadi mwingi ambao umeibuliwa na wapinzani na kuweza kuiamsha serikali usingizinini na pia kuwapa wananchi fursa kuweza kujua kodi zao zinavyotumiwa vibaya na baadhi ya watu wasiotakia mema nchi yetu. Kingekua kipo chama kimoja tu tusingeweza kufahamu haya yote na ni sababu hizo hizo za kuionyesha serikali ufisadi uliopo uliowapaisha wapinzani mpaka kuwa na wabunge wengi kwenye uchaguzi uliopita baada ya wananchi kuona kwamba serikali haifanyi kazi zake vizuri na kuweza kukiadhibu chama tawala kwenye sanduku la kura.
Unapoua upinzani tusitegemee mambo tuliyoyaona siku za nyuma kuyaona tena kwa sababu kuwepo chama tawala peke yake hakitaweza kuiongoza serikali yake. Hii itasababisha serikali kujiendesha yenyewe ambayo ni hatari sana kwa mstakabali wa nchi yetu.
Kwa mwanasiasa ambae yupo makini na ana maslahi na nchi yetu hawezi kushabikia eti upinzani upotee kwa nia ya chama kimoja kushinda kila kitu. Mimi kama mwananchi wa kawaida ningependa kupata ukweli kuhusu utendaji wa serikali yangu na ukweli hauwezi kutoka serikalini pekee kwa sababu hakuna serikali itakayojisemea mabaya. Wapinzani wapo ili kuyasema hayo mabaya yaliyopo serikalini na ni kwa nia nzuri tu ya kuifanya serikali itekeleze wajibu wake.
Naishauri serikali ya Raisi Magufuli iruhusu upinzani kufanya kazi yake. Naamini raisi ana nia njema na nchi yetu lakini hawezi kufanya kazi yake vizuri upinzani usipokuwepo. Siasa za kubana upinzani zimepitwa na wakati na pia watanzania wanaelewa kinachoendelea. Kuna mambo mengi sana yanatakiwa yafanyike ili nchi yetu iweze kusonga mbele,kwa sasa watanzania wanazungumzia ubakwaji wa demokrasia badala ya kuzungumzia maendeleo yao. Wanasiasa wameshaanza kubaguana,wananchi nao pia wameanza kubaguana kivyama. Hii ni hatari sana kwa nchi yetu na serikali isipoangalia hali itakua mbaya sana huko mbeleni. Serikali ilitafakari hili kwa jicho la tatu ili tuweze kusonga mbele la sivyo tutashindwa kufika huko tunakokutaka.