Mwanasiasa bora wa mwaka 2014

Mwanasiasa bora wa mwaka 2014

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
3,115
Reaction score
3,864
Tujadili kidogo kumtafuta mwanasiasa bora wa mwaka 2014 tukizingatia mchango wake kwa siasa na maendeleo ya Taifa.

Warioba:

Ameongoza tume ya mabadiriko ya Katiba na kutoka na rasmu inayokubalika na wengi na pande zote za muungano. Kutokana na hilo amejikuta matatani hata kushambuliwa na kundi la mahafidhina wasiotaka mabadiliko ndani ya chama chake.

Mbowe:

Aliongoza kambi ya upinzani kudai mambo mengi yenye manufaa kwa taifa. Kubwa zaidi amewezesha kuundwa kwa UKAWA jambo ambalo limekuza demokrasia na matokeo ya serikali za mitaa ni kielelezo. Aliunda serikali balaza kivuli linalotokana na vyama vitatu.

Zitto:

Huyu alikuwa na mwaka mgumu sana kisiasa, alifukuzwa ndani ya chama chake. Alijaribu kuanzisha chama lakini team yake inamwangusha. Amemaliza mwaka vizuri kwa kuongoza kamati ya PAC katika kashfa ya Escrow.

Dr Slaa:

Huyu hachuji katika siasa za nchi hii. Ameongoza chama chake kufanya programu ya Chadema ni msingi iliyozaa matokeo mazuri uchaguzi wa SM. Aliongoza chama kufanya mkitano mkuu wa uchaguzi uliokuwa wa kihistoria, chama pia kimeweza kununua vifaa vya uenezi vya chama ikiwa ni pamoja na pikipiki.
 
Unatia mashaka, zaidi umeegemea one side kwanini?
 
ungeacha watu mwenyewe wachague na kutoa sababu isiwe fixed
 
Unatia mashaka, zaidi umeegemea one side kwanini?

Inawezekana kweli lakini hapa nilitaka kumweka Sitta kwa kazi ya kutunga katiba pendekezwa kamaanemaliza vizuri lakini unajua kilichotokea ndg!
 
Unatia mashaka, zaidi umeegemea one side kwanini?
Sasa wewe ulikuwa unataka awaweke wanasiasa wa magamba?

Wewe unadhani wanasiasa wa kambi hiyo nyingine kuna nini cha zaidi walichochangia cha maana kwa ajili ya ustawi wa Taifa hili?

Zaidi sana ndiyo wametuongezea umasikini, kutokana na kugawana kama njugu, pesa yetu ya Escrow pale Mkombozi bank, na kuyasomba mabilioni mengine, kwenye viroba na magunia ya lumbesa, kule Stanbic bank!
 
Mi naona mleta mada yuko sawa kabisa, yeye katoa maoni yake na mtazamo wake, kama kuna mwingine ana mtazamo hasi kuhusu hao aliowataja ni vyema akauweka tu hapa jukwaani pia tukaujadili pamoja. Au kama kuna mwanasiasa mwingine ambaye wewe unadhani anafaa kuwa mwanasiasa bora wa mwaka 2014 (bila kujali itikadi za vyama) unaweza pia kumweka na yeye tumwone, mwisho wa siku tutaona nani ni zaidi ya mwingine.

Any way, kwa mtazamo wangu naona Mbowe ndiye anaweza kuwa mwanasiasa bora kutokana na kukiongoza chama chake vizuri na hata kambi ya upinzani bungeni katika kuendesha harakati za upinzani ndani na nje ya bunge.
 
Sasa wewe ulikuwa unataka awaweke wanasiasa wa magamba?

Wewe unadhani wanasiasa wa kambi hiyo nyingine kuna nini cha zaidi walichochangia cha maana kwa ajili ya ustawi wa Taifa hili?

Zaidi sana ndiyo wametuongezea umasikini, kutokana na kugawana kama njugu, pesa yetu ya Escrow pale Mkombozi bank, na kuyasomba mabilioni mengine, kwenye viroba na magunia ya lumbesa, kule Stanbic bank!

Niowaongezee kina Mwigulu,Makamba, kigwangala na Nyalandu.
 
Akitoka Warioba anafuatiwa na zitto then kafulila.
Tujadili kidogo kumtafuta mwanasiasa bora wa mwaka 2014 tukizingatia mchango wake kwa siasa na maendeleo ya Taifa.

Warioba:

Ameongoza tume ya mabadiriko ya Katiba na kutoka na rasmu inayokubalika na wengi na pande zote za muungano. Kutokana na hilo amejikuta matatani hata kushambuliwa na kundi la mahafidhina wasiotaka mabadiliko ndani ya chama chake.

Mbowe:

Aliongoza kambi ya upinzani kudai mambo mengi yenye manufaa kwa taifa. Kubwa zaidi amewezesha kuundwa kwa UKAWA jambo ambalo limekuza demokrasia na matokeo ya serikali za mitaa ni kielelezo. Aliunda serikali balaza kivuli linalotokana na vyama vitatu.

Zitto:

Huyu alikuwa na mwaka mgumu sana kisiasa, alifukuzwa ndani ya chama chake. Alijaribu kuanzisha chama lakini team yake inamwangusha. Amemaliza mwaka vizuri kwa kuongoza kamati ya PAC katika kashfa ya Escrow.

Dr Slaa:

Huyu hachuji katika siasa za nchi hii. Ameongoza chama chake kufanya programu ya Chadema ni msingi iliyozaa matokeo mazuri uchaguzi wa SM. Aliongoza chama kufanya mkitano mkuu wa uchaguzi uliokuwa wa kihistoria, chama pia kimeweza kununua vifaa vya uenezi vya chama ikiwa ni pamoja na pikipiki.
 
Warioba ametisha nadhan hadi kuhatarisha.maisha yake
 
Mwigulu nchemba ameleta tumaini jipya katika kuondokana na rushwa.
 
Kwangu Warioba halafu Mh.Mbowe......... Warioba kasimama kidete kuielewesha jamii juu ya uchakuzi kwenye rasimu,hakujali uanachama wake ndani ya CCM,jaji ameweka maslahi ya Taifa mbele....Nikija kwa Mbowe,huu muunganiko wa vyama vinavyounda UKAWA unatosha kuamini kuwa Mbowe ni mwanasiasa anayejua mikakati na kwenda na wakati,ameweka umimi na uchadema Pembeni
akaangalia kile Watanzania wanataka.....kuitoa CCM madarakani......hakika umoja huu ni tishio kwa CCM........ Kwa Nyongeza ni kuwa Nchemba nuru ya Bwana imemshukia kijana kaumaliza mwaka huku nyota yako ikichomoza kwa kasi, Mungu aendelee amzidishie moyo wa kujitambua,ikibidi siku moja atubu kwa aliyoyafanya hapo kabla.
 
Yeyote aliye CCM ni fisadi kama wenzake!

Wanasiasa wote mafisadi tu sema wanatofautiana viwango wengine wake za watu, viti maalum, ruzuku za chama, majengo dubai etc. Hapa tunaangalia ahueni.
 
Back
Top Bottom