Mwanasheria na Mhandisi wa Jiji la Mwanza Kizimbani

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
HALMASHAULI ya Jiji la Mwanza leo imesimamisha kazi watumishi wawili kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kusababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. 300 milioni.

Waliosimamishwa kazi ni Ezekiel Kunyaranyara, Mhandisi na Makusudi Bwabo, Mwanasheria wa Jiji.

Kunyaranyara anatuhumiwa kusimamia vibaya fedha za miradi ya maendeleo zilizotolewa kwa ajili ya matengenezo ya dharura.

Bwabo anatuhumiwa kutokana na kulalamikiwa na wafanyabiashara kwamba wakati wa kukusanya mapato katika biashara zao, huwatisha na hata kuwapeleka mahakamani bila sababu za msingi.

Miradi anayotuhumiwa kusimamia wakati wa ukarabati na kuwa chini ya kiwango ni jengo la machinjio liliopo Nyakato, Kata ya Mhandu, Daraja la Mwananchi lililopo Kata ya Mahina, mitaro ya barabara za Kata za Mhandu, Mkuyuni, na ukarabati wa kituo cha kulelea watoto waisho katika mazingira magumu.

Adamu Mgoyi, Mkurugenzi wa Jiji, na James Bwire, Meya wa Jiji, wamethibitisha kuwa wamesimamisha watumishi hao kwa tuhuma hizo.

Bwire amesema mhandisi huyo ameshindwa kuonesha uzalendo wa kusimamia miradi hiyo, badala yake imetekelezwa chini ya kiwango.

Ametoa mfano wakituo cha kulelea watoto wasiojiweza, kuwa kilipaswa kukarabatiwa kwa Sh. 19 milioni lakini ukarabati uliofanywa ni upakaji wa rangi pekee.

“Huyu mhandisi mwenyewe ndiye aliyependekeza na kuomba fedha hizo kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho, lakini Sh. Milioni 19 zimetumika kwa kukapaka rangi, chokaa na kutengeneza milango miwili tu, badala ya kukarabati sehemu zilizoelekezwa,” amesema Bwire.
 
kilichonifedhehesha kwamba Muhandisi hela kaomba mwenyewe kwa maneno mengine wembe kaulilia yeye mwenyewe
 
Halmashauri zote walaji ni DED, DE na PMU. Hayo ndio majipu yanatakiwa yatolewe na Miguu yake
 
nashangaa rais anahangaika na dar es salaam pekee mwanza ndio kuna madudu kupita maelezo si TRA Tanesco reli mwisho wa matatizo ni jiji
 
Duh! Kunyaranyara hatimae umekwenda mahakamani!
aende tu kwanza amejaza kabila lake ofis zote za wahandis kuanzia wahands wa majengo maji na barabara weng kabila lake afu wanadharau kama yule ps wake ndo baasi ukienda na bahasha tu pale anajua unatafuta kazi
 
Hawa wakurugenzi wa halmashauri, magu angebadili wote, na watakao ingia wale kiapo cha maadili na wataje Mali zao. Kuna mkurugenzi mmoja tu ambae namfaham sio fisadi, yuko iringa municipal, anaitwa Hamad Sawa...!!! Huyo labda azungukwe na wajanja
 
Hawa Wakurugenzi wamekichafua sana chama chetu halafu mwishoni wakajiandaa kupokea fungu la Minywele kama sio Mkwere ku block account ya yule mfadhili with October 2015 ili wafanye manuva nchi apewe Mkwe wa Fisadi wa Stanbic
 
ccm mbele kwa mbele
Hao awana kazi yoyote ni makada tu wa ccm waacheni wale Mbona munawabugudhi wakale wapi sasa?
Ila huyo mwanasheria kazi anayo
 
Back
Top Bottom