Mwanasheria Mkuu wa Serikali amuunga mkono Jecha

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, George Masaju amemuunga mkono Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, kwa kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana na kusema hatua hiyo ni halali kutokana na sababu zilizotajwa.

“Ukichukua kasoro zote na hii ya mgombea kujitangaza mshindi... ni tatizo kubwa, lazima mtaingia kwenye matatizo iwapo huyu kajitangazia ushindi halafu matokeo yamtangaze mshindi tofauti na huyo,” alisema Masaju.

Akizungumza kwenye kipindi cha Siku 100 za Serikali ya Awamu ya Tano, kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1), juzi usiku, Mwanasheria huyo alisema ZEC iko huru kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na uamuzi uliofanywa na Mwenyekiti wa Tume hiyo ni kitendo halali.

Masaju alisema kasoro zote zikichunguzwa, ikiwemo hiyo ya mgombea kujitangazia ushindi, kulikuwa na kila sababu ya kufuta matokeo hayo ili uchaguzi urudiwe.

Alisema iwapo dosari hizo, zingeachwa bila kufanyiwa kazi, hata wagombea wasio na sifa ya kushinda katika uchaguzi huo, wangesema na wao ni washindi hivyo kungetokea machafuko ambayo yangeweza kuleta matatizo makubwa zaidi.

Ila kwa hatua iliyochukuliwa na ZEC ni jambo sahihi la kurudisha amani na kupanga tarehe nyingine ya kurudia uchaguzi huo, ili kasoro hizo zirekebishwe na mshindi apatikane kwa haki na kuepuka machafuko.

Masaju alisema awali Rais John Magufuli wakati akihutubia Bunge kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe, alisema atashirikiana na Rais wa Zanzibar kumaliza suala la uchaguzi, ila hakusema ataingilia uhuru wa Tume.

“Rais alipohutubia Bunge kwa mara ya kwanza aliahidi kushirikiana na Rais wa Zanzibar kumaliza suala la uchaguzi, ila hakusema ataingilia uhuru wa Tume na ndicho alichofanya, Zanzibar ina amani,” alisema Masaju.
 
kitendo cha jecha ni halali kwa sababu ni yeye pekee kwa mijubu wa sheria anayeweza kufuta matokeo ya uchaguzi.
lakini je kitendo hicho ni sahihi?
je kulikuwa na malalamiko yoyote yaliyopelekwa na chama chochote kuhusu dosari hizo? je sheria inairuhusu ZEC kufuta matokeo ya uchaguzi SUA MOTO?
je ni legal grounds zipi amabazo jecha alizitumia kufuta matokeo ya uchaguzi?
inawezekana kweli kulikuwa na kasoro kadhaa ambazo ama ni fatal kiasi cha kuathiri matokeo ya uchaguzi lakini je kuna uthibitisho gani kuwa sababu hizo ni fatal? kiasi cha kufanya matokeo yafutwe?
je kitendo cha maalim seif kukusanya matokeo yaliyobandikwa na ZEC kwenye vituo vya kuhesabia kura viliyowekwa na ZEC yakiwayameruhusiwa kubandikwa na ZEC ni kosa kisheria? je kosa hilo ni fatal kiasi cha kusababisha kufutwa kwa uchaguzi?

kuendelea kuutetea upuuzi wa Jecha ni kuendelea kuimarisha mizizi ya dhuluma na uvunjaji wa haki za raia na zaidi ni kuua mizizi ya demokrasia.

tujaribu kutumia taaluma zetu katika kuimarisha misingi ya haki na demokrasia, siyo kwa sababu ni employees wa serikali tunawajibika kutetea hata upuuzi huku ni kudhalilisha taaluma zetu.
 
hivi niulize? kwa nini maalim Seif alijitangaza mshindi kabla ya tume kutangaza? ???????na je kama tume ingemtangaza Shein kuwa rais kungeweza kutokea nini. labda tuanzie hapo
 
hivi niulize? kwa nini maalim Seif alijitangaza mshindi kabla ya tume kutangaza? ???????na je kama tume ingemtangaza Shein kuwa rais kungeweza kutokea nini. labda tuanzie hapo
Hivi alitangaza kura zake alizopata au alijitangaza kwamba ameshinda?
 
Hivi mtu akipata mimba na kila dalili zikionekana afya safi,ni kosa kujitabilia kuwa nategemea kupata mtoto? Katika nchi ya Tanzania hatujawahi kuwa na Wana sheria wakuu wa serikali labda yule Mzanzibar aliyewatolea uvivu wakati wa Bunge Maalumu la Katiba 2014 huyo ndiye pekee alitumia weledi wake wa sheria kwa manufaa ya serikali na watanzania wa kawaida.Sasa Chenge,Werema,Banyikwa,Masanju,Lubuva na Marc Bomani wote waganga njaa ilimatupo yao yashibe.
 
hivi niulize? kwa nini maalim Seif alijitangaza mshindi kabla ya tume kutangaza? ???????na je kama tume ingemtangaza Shein kuwa rais kungeweza kutokea nini. labda tuanzie hapo

Mbona suali lako limejibiwa zaidi ya mara 1000000000 , hivi unakuwa unasoma kinachoandikwa??

Jibu

Matokeo yote ya kwenye vituo huwa yanawekwa saini na hao viongozi wa Zec waliowekwa kwenye vituo .

Matokeo hayo huwa yanakabidhiwa kwa mawakala na kutundikwa ukutani .

Alichofanya Maalim Seif ni kukusanya hayo matokeo na kujumlisha , na kuwaomba Tume wamtangaze kabla ya kuchakachuliwa kama vile walivyozowea . Huku bara Watu wa Lowasa walikuwa wakikusanya matokeo lakini kabla hawajamaliza walivamiwa na polisi na vyombo vya usalama na hapo hapo watu wa Malocks waliwahi kumtangaza ndiye mshindi. Hii ndiyo Demokrasi ya TZ na nchi nyingi za Afrika

kwa uwazi zaidi msikilize tundu Lisu anajibu vizuri hilo suali lako

Zile fomu kutoka katika vituo vya kupiga kura vilionesha idadi ya kura kila mgombea alizopata.

Na kila mgombra alisaini kuridhia matokeo hayo isipokuwa wagombea urais.

Alichokifanya Maalim Seif ni kujumlisha na kuangalia amepata kura ngapi na mwenzake amepata ngapi majimbo ya uchaguzi.

Sasa baada ya matokeo kuonekana kawazidi washindani wake akaamua kusema alichokipata tofauti na wenzake. Je, alijitangaza kuwa rais au alitangaza alichopata na kuwashinda wenzake?

Na kama kajitangaza kuwa rais kwanini asifunguliwe mashtaka ya kuvunja utaratibu wa ZEC na sheria ya uchaguzi Zanzibar?

Ukiacha taaluma yako na kufanya kazi kwa kuupendelea upande usohaki basi ni kupotoka.

Afadhi aliyeyasema hayo hapo kwenye post kaonesha upande wake.

Kuna huyu aliyesema haya japo sikumbuki kama ni hivi alivyosema kwa usahihi wake ila maana sitokuwa nimeikosea.

"If you do not show your side, you're supporting the oppressors" ~Desmond Ntutu
 
Don't argue with full, people might not notice the difference. They will think you're all the same. Ngoja sheria ichukue mkondo wake.
 
Alijitangaza kuwa yeye kashinda uchaguzi au hkuwepo nchini?

Kwa kuwa kura alizokua amepata na matokeo kuwekwa kwenye vituo, hakukua na miujiza kwamba kuna mgombea mwingine angefikisha idadi kumzidi. Ni sawa tu na penalty, ikifika idadi fulan unajua mpizan wako hawezi kukufikia na hivyo unashangilia kabla hata refa hajapuliza kipyenga
 
hivi niulize? kwa nini maalim Seif alijitangaza mshindi kabla ya tume kutangaza? ???????na je kama tume ingemtangaza Shein kuwa rais kungeweza kutokea nini. labda tuanzie hapo

Labda tumalizie hapo. Uchaguzi wa 1995 , kila mzanzibari alijua mshindi ni nani, hata vyombo vya habari vya nje na ndani ya nchi kam vile kama vile DTV vilidiriki kumtangaza mshindi.

Mshindi kufikia kupewa pongezi za awali na mwenyekiti wa tume . Matokeo ghafla yalipinduliwa na akatangazwa mshindi wa CCM ambae hakushinda. Mwenyekiti alipotea miezi mitatu.

Katika kutangazwa kura , kwa mara ya kwanza katika historia ya Zanzibar kura za rais zilizo haribika zilizidi 5,000 ! Hakuna kilichotokea baada ya kutangazwa mgombea amae ni tofauti alitangazwa na vyombo vya habari.

Mara hii mgombea huyohuyo hakutaka yatokee tena yale 1995 na kwa vile mara hii Tume kutaka ionekane kuwe iko huru zaidi ilianzisha utaratibu kwa mara ya kwanza kura za rais nazo pia zihisabiwe vituoni na matokeo yabandikwe vituoni baada ya kuhesabiwa. Seif Sharif mara hii ali "pre- empt"

Kwa vyovyote vile makosa yaliorodheshwa ikiwa ni kweli, basi huwezi kuhalalisha uchaguzi wa Rais wa jamhuri ya muungano. Chaguzi zote mbili ni batili na irejewe.

Mwanasheria huyo alipaswa kuzungumzia zaidi uchaguzi wa Meya wa Dar kuliko uchaguzi wa zanzibar, kwa vile ni mbumbumbu na siasa za Zanzibar. Zanzibar pia tuna mwanasheria mkuu, na hajatoa hoja za kipumbavu kama hizo. Lakini ni kawaida msema pweke huwa mshindi
 
Mkwere alimtangaza mapushap kua ndie rais wa awamu ya tano tarehe 24/10/2015 yaani kabla ya uchaguzi kufamyika.
Kwani ukisema kura zilizopigwa zinaonesha nimeshinda kwa hiyo tume ikamilishe kutangaza matokeo haraka..hili linafuta matokeo kwenye karatasi za kura ?
kama ni sheria ilikiukwa kuna sheria gani inayokipa mamlaka chama tawala kupiga wananchi risasi kwa kosa la kikatiba la kuandamana ?
kama walivyofanya january 27 2001 Pemba !
mbona hicho chama hakikufutwa ?????
 
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, George Masaju amemuunga mkono Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, kwa kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana na kusema hatua hiyo ni halali kutokana na sababu zilizotajwa.

“Ukichukua kasoro zote na hii ya mgombea kujitangaza mshindi... ni tatizo kubwa, lazima mtaingia kwenye matatizo iwapo huyu kajitangazia ushindi halafu matokeo yamtangaze mshindi tofauti na huyo,” alisema Masaju.

Akizungumza kwenye kipindi cha Siku 100 za Serikali ya Awamu ya Tano, kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1), juzi usiku, Mwanasheria huyo alisema ZEC iko huru kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na uamuzi uliofanywa na Mwenyekiti wa Tume hiyo ni kitendo halali.

Masaju alisema kasoro zote zikichunguzwa, ikiwemo hiyo ya mgombea kujitangazia ushindi, kulikuwa na kila sababu ya kufuta matokeo hayo ili uchaguzi urudiwe.

Alisema iwapo dosari hizo, zingeachwa bila kufanyiwa kazi, hata wagombea wasio na sifa ya kushinda katika uchaguzi huo, wangesema na wao ni washindi hivyo kungetokea machafuko ambayo yangeweza kuleta matatizo makubwa zaidi.

Ila kwa hatua iliyochukuliwa na ZEC ni jambo sahihi la kurudisha amani na kupanga tarehe nyingine ya kurudia uchaguzi huo, ili kasoro hizo zirekebishwe na mshindi apatikane kwa haki na kuepuka machafuko.

Masaju alisema awali Rais John Magufuli wakati akihutubia Bunge kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe, alisema atashirikiana na Rais wa Zanzibar kumaliza suala la uchaguzi, ila hakusema ataingilia uhuru wa Tume.

“Rais alipohutubia Bunge kwa mara ya kwanza aliahidi kushirikiana na Rais wa Zanzibar kumaliza suala la uchaguzi, ila hakusema ataingilia uhuru wa Tume na ndicho alichofanya, Zanzibar ina amani,” alisema Masaju.

Alichokifanya Maalim Seif ni kujumlisha na kuangalia amepata kura ngapi na mwenzake amepata ngapi majimbo ya uchaguzi.

Hapo ndipo Seif alipokosea kazi hiyo kisheria inatakiwa ifanywe na tume sio mtu binafsi.Mfano wewe ungejifungia chumbani na kujumlisha ukiwa na hawara yako halafu mkaibuka kusema hizi ndio kura zenyewe!!! Watu watahakiki vipi ukweli wake???? Hizo za Seif NANI kazihakiki kuwa za kweli na chombo gani cha kisheria KILICHOHAKIKI?

Ndio maana tume inabidi ndio itangaze kwanza na wengine wote mtakaojumlisha popote mlinganishe hizo jumla zenu na za tume sio Tume ilinganishe jumla zake na zile alizojumlisha na kutangaza Seif na Wanywa viroba wenzie wa UKAWA.

Tatizo la kutozingatia sheria lina gharama ndizo hizo ikiwemo kurudia uchaguzi
 
Back
Top Bottom