Mwanasheria Mkuu aviwakia vyombo vya usalama sakata la Ben Saanane

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
947
BEN+PICHA.jpg

Dodoma. Hatimaye Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amevunja ukimya wa sakata la kutoweka kwa kada wa Chadema, Ben Saanane, akieleza kuvishangaa vyombo vya usalama kutochukua hatua sahihi ili kupata ukweli.

Masaju ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kumshangaa kwa kufanya kazi ya kuitetea Serikali bungeni badala ya kuhakikisha inatekeleza majukumu yake.

Mchungaji Msigwa alisema hayo wakati akichangia hotuba za bajeti za Ofisi ya Rais (Tamisemi) na Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Jana, AG Masaju aliinuka na kuzungumzia kutoweka kwa Saanane, ambaye ni msaidizi wa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na pia kujibu hoja za wabunge wa upinzani.

Akizungumzia matukio ya utekaji jana, Masaju aliliambia Bunge kuwa hafahamu sababu za suala hilo kujitokeza mara kwa mara ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria.

“Mambo ya utekaji yanajitokeza sana hapa, sijui kwanini? Mimi naomba kushauri mheshimiwa mwenyekiti, polisi waendelee kushirikiana na watu walio karibu sana na huyu mtu anayedaiwa kupotea,” alisema.

“Waisaidie polisi ili tupate ukweli. Kwanza familia yake na watu ambao amekuwa akifanya nao kazi kwa karibu watoe ushirikiano kama ambavyo wabunge wameshauri. Katika suala hili hatuwezi kuwa na double standard (kigeugeu).”

Saanane alitoweka katika mazingira ya kutatanisha Novemba 15 mwaka jana na licha ya wazazi, Chadema na wanaharakati kuhoji alipo, Jeshi la Polisi limekuwa halitoi taarifa hadi linapoulizwa na waandishi wa habari.

Hali hiyo imefanya mjadala wa kutoweka kwake uendelee kukua na wabunge kuamua kuhoji mamlaka husika kuhusu alipo, huku wakisema hofu inaongezeka kutokana n a matukio mengine ya utekaji, uvamizi na mbunge kutishiwa bastola siku moja baada ya kuachwa katika Baraza la Mawaziri.

Mjadala huo ulifikia hatua ya wabunge kuihusisha Idara ya Usalama wa Taifa na matukio hayo, jambo lililomlazimu Naibu Spika Tulia Ackson kupiga marufuku kuizungumzia taasisi hiyo.

Jana, Masaju alisema Mbowe alisema alikuwa akijua kuwa polisi wanafanya kazi, lakini hajui siku hizi wanafanyaje kazi.

Alisema watu walio karibu na familia wangesaidia kutoa taarifa Jeshi la Polisi.

“Mtu yeyote aliyeko kwenye public (umma) atusaidie halafu, we will take action accordingly (tutachukua hatua kadri inavyotakiwa). Mimi nilivyojua polisi walikuwa wanafanya kazi. Siku hizi sijui wanafanyaje kazi,” alisema Masaju.

“Sasa hivi tungekuwa na watu wanaoisaidia polisi kwa karibu mno. Sasa how we can handle this matter so much successfully ( ni vipi tunaweza kulishughulikia jambo hili kwa mafanikio)?” alihoji Masaju akionekana kumaanisha kuwa kama polisi wangekuwa wanafanya kazi vizuri, wananchi wangejitokeza kusaidia kutoa taarifa.

Alisema Mbowe amesaidia katika suala hilo katika hotuba yake ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

“Mheshimiwa Mbowe ametusaidia katika hotuba yake. Hakuna mtu aliye juu ya sheria,” alisema Masaju.

“Moja, watatueleza tangu lini mtu huyu anayedaiwa kupotea au kufariki, alipotea? Ilichukua muda gani kutoa taarifa? Halafu familia na watu waliokuwa karibu na huyu mtu na hii familia wameshapeleka suala hilo katika vyombo vya habari kwamba huyu mtu amepotea?”

Masaju alisema watu waliokuwa wanafanya kazi na Saanane, watu wake wa karibu na familia yake watoe taarifa katika vyombo vya dola ili vifanyie kazi kwa karibu.

Pia Masaju amewashukia wabunge wa upinzani kuwa wamekuwa wakiwatukana mawaziri wakati wanawaomba waende majimboni mwao kutatua kero zao.

Kuhusu uhuru wa mijadala ndani ya Bunge, Masaju alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano iko wazi kuhusu mijadala ya Bunge.

“Isome ibara ya kwanza na ya pili, unayo haki tu katika mijadala wakati wa kutekeleza majukumu yako ya Bunge ukizingatia Katiba na sheria za nchi,” alisema.

Alisema hadi sasa Serikali haijakataza vyombo vya habari kuripoti mambo yanayoendelea bungeni.

“Niwashauri waheshimiwa wabunge kama mtataka kurudi kwenye Bunge hili teteeni mambo yanayowahusu wapigakura wenu. Bunge la mwaka 2010 lilikuwa na hiyo live broadcasting lakini wabunge wengi hawakurudi,” alisema.

Kuhusu wateule wa Rais, Masaju alisema Rais John Magufuli amekuwa bungeni tangu 1995, mawaziri wanaomsaidia ni watumishi wa umma walikuwepo humu tangu kipindi hicho.

“Mimi nimeanza kazi mwaka 1994, kinachobadilika ni wanasiasa na nyie wenyewe mlienda kuomba kura, mkashindanishwa msio na uzoefu na walio na uzoefu. Walio na uzoefu wakashinda na wameunda Serikali,” alisema.

Alisema Serikali hii inaongozwa na watu wanaotekeleza majukumu yao kwa ufanisi na ndio maana imeweza kutekeleza mambo yake kabla hata ya miaka miwili.

Kuhusu ushirikiano, Masaju alisema lazima uanzie bungeni na kupanuka hadi majimboni.

“Hamuwezi kuwa mnawatukana mawaziri, mnamtukana hapa Mwanasheria Mkuu, waziri mnamtukana halafu kesho mnamwambia aje jimboni kwako, kufanyaje huko?” alisema huku akipigiwa makofi na wabunge wa CCM.

Wakati akisema hayo, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema alisimama kuomba mwongozo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge alimtaka aketi na kumpa fursa Masaju aendelee.

“Unasema waziri hana uwezo, sasa unamuitia nini jimboni?” alihoji.

Alisema Serikali haiwezi kuruhusu watu wachache wakaharibu amani ya Taifa kwa vitendo ama kwa kauli zao ama kwa nyendo zao.

“Ni lazima turudishe nidhamu ndani ya Bunge hili. Lazima amani itawale na usalama,” alisema Masaju.

Akichangia makadirio hayo, Mbunge wa Mtera (CCM), Job Lusinde alishauri kuanzishwa kwa dawati maalumu litakaloshughulikia upotevu wa watu.

“Naamini kuna watu wengi wamepotea. Leo tukiwauliza wabunge kila mmoja katika jimbo lake kuna mtu aliyepotea (watasema yupo). Hivyo endapo litaanzishwa dawati hilo, litasaidia kufanikisha kupatikana ufumbuzi,” alisema.

Akihitimisha mjadala wa hotuba yake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene alisema bado kuna matatizo mengi katika halmashauri mbalimbali kuhusu manyanyaso ya Machinga ambao wanafukuzwa kila mahali na kuwafanya washindwe kuchangia uchumi wa nchi yao.

“Hawa ni watu ambao wanachangia kwa sehemu kubwa uchumi wetu kama tutawapanga vizuri na kuwajali katika biashara zao, duniani kote watu hawawezi kuwa na uchumi rasmi, lazima wengine wawe nyuma na ndiyo hao Machinga,” alisema Simbachawene

Waziri aliwataka wakurugenzi kote nchini kuangalia namna bora ya kutenga maeneo mazuri ya kufanyia biashara na kuweka miundombinu mizuri ya maeneo hayo ikiwemo umeme na barabara ambayo yatakuwa na kivutio kikubwa cha watu wengi kukimbilia huko.

Kwa upande wake Waziri wa Utumishi, Angela Kairuki alisema suala la uwajibikaji na utawala bora limeimarika kwa kiasi kikubwa ikiwemo nidhamu ndani ya utumishi wa umma.

Aliwaagiza waajiri wote kufuata taratibu za uwajibishaji kwa watumishi wa chini yao ikiwemo kuzingatia muda wa kushughulikia matatizo ndani ya muda usiozidi siku 120 ili kuwapa nafasi watumishi kujua hatma yao. Kuhusu watumishi kupewa mafunzo, alisema utaratibu huo bado unaendelea na kwa mwaka wa fedha 2015/16 watumishi 395 walipewa mafunzo wakati kwa mwaka 2016/17 jumla ya watumishi 654 walipewa mafunzo ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuboresha utumishi wao.

Waziri alitaja idadi ya watumishi 54,236 kwamba wataajiriwa kwa mwaka wa fedha 2017/18 baada ya watumishi hewa zaidi ya 19,708 kuondolewa katika mfumo ambao uliwezesha kuokolewa kwa Sh 19.8 bilioni ambazo zingetumika kwa mishahara na watumishi.

Alisema tayari jumla ya watumishi 1595 walioshiriki kuongeza watumishi wamewajibishwa na wengine kufukuzwa kazi na kesi ziko mahakamani huku kukiwa na marejesho ya Sh 9 bilioni ambazo zimelipwa na watumishi hao.

Chanzo: Mwananchi
 
nimemsikiliza mwanasheria mkuu lakini nilichong'amua mmmmmhhhhh ... not good to the complainants. Hebu msikilizeni vizuri.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mleta mada mpuuzi kweli. Sijui kaandika nini hapa. Naona kabaki online ili aone nini tunacho comment. Hata hivyo ambao hamjacomment kwenye huu upuuzi msifanye hivyo kwani dogo mwenyewe amejiunga jamiiforum Aprili hii, hivyo anahitaji tuition ya jinsi ya kuanzisha mada zenye mashiko.
Mhhhhhhhh wewe bashite nini
 
Hapo sasa dogo umefanya kweli. Huko chini nilikublast baada ya kuleta mstari mmoja wa thread bila ufafanuzi. Nashukuru umejifunza na kujirekebisha faster.
 
Mleta mada mpuuzi kweli. Sijui kaandika nini hapa. Naona kabaki online ili aone nini tunacho comment. Hata hivyo ambao hamjacomment kwenye huu upuuzi msifanye hivyo kwani dogo mwenyewe amejiunga jamiiforum Aprili hii, hivyo anahitaji tuition ya jinsi ya kuanzisha mada zenye mashiko.
Mleta mada amejirekebisha wakuu baada ya kupondwa.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Ninachojua,polisi na vyombo vya usalama huchunguza jinai iliyotendwa,baada ya kuchunguza,hupeleka faili kwa mwanasheria mkuu wa serikali ili atoe maelekezo ya kisheria kama ushahidi umetosha au laa,au nani anatakiwa ahojiwe ili kukidhi masharti.

Pia anaweza na alitakiwa atoe maelekezo na au kukutana na polisi kujua nini kinaendelea,aombe faili na kama kuna lolote au yeyote wa kuhojiwa,ahojiwe

Sasa badala ya kuwapa maelekezo ndani ya faili kwa barua,yeye anawapa barabarani
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Aache drama kwani habari za kupotea kwa Ben kazijua leo?
Yeye kwa mamlaka aliyonayo mbona alikaa kimya?
Akisikia akina makengeza wanahoji ndo anakuja mbio mbio na kujifanya ana hoja nyingi.

Hii nchi viongozi wanafiki sana, Sio Chadema sio Ccm wala sio watendaji kila mtu mnafiki tu
 
Ben Sanane ahojiwe Mbowe, ujinga wa kupiga kelele bungeni ni kupoteza ukweli ili ionekane serikali haifanyika. Ni kichekesho.
Hivi Chacha Wangwe ambaye alikuwa Makamu
 
Ben Sanane ahojiwe Mbowe, ujinga wa kupiga kelele bungeni ni kupoteza ukweli ili ionekane serikali haifanyika. Ni kichekesho.
Hivi Chacha Wangwe ambaye alikuwa Makamu
Alomtolea NAPE BASTOLA AHOJIWE NANI?
 
Policcm washirikiane na AG,kwakua wote wanajua kilichomkuta Ban Saa 8.huyu AG ndo alisema Mawazo,asiagiwe Mwanza sio kwao.asijitie kushangaa ya Ben !akishangaa AG,mwanachi wa kawaida naye afanyeje ?Leo ndo anasikika baada ya Msigwa kusema? Huyo nae ni bashite tu.tusimpe pumzi mpaka amlete saa
8.mnafiki wa kuzimu huyo.jitu zima linadhalilisha elimu na taaluma yake kwakutumika na ccm kama toileti pepa hovyo kwelikweli dude hili ! Mungu uluyemuumba AG mnafiki kama huyu,Ww ndiye unayemjua nakuomba Bwana wangu,umshuhulikie sawasawa na unafiki wake,apate kinacho mstahili.Amen
 
Tunaoelewa causes ya Kilichomkuta Ben tujikumbushe haya

HII NDIO SABABU YA KUTAKA KUTOA UHAI WAKO MTOTO WA MAMA Ben-Rabiu Wa Saanane......WALIKUNYAKUA.....WAKAFUTA POST ZAKO ZTE ZA TAR.9,-13 LEO WANATAMKA KWA VIBURI ETI"ALIYETANGULIA MBELE YA HAKI....HALITABAKI JIWE JUU YA DAMU YA Ben......

ALICHOANDIKA WEEK KABLA YA KUNYAKULIWABen-Rabiu Wa Saanane
...
Onyo:Nitawajibu kwa wepesi wanaostahili ili Siku nyingine wajipange kumtetea kwa hoja.Najadili bado Sakata La PH.D ya Mhe.Magufuli na Uhakiki wa vyeti.Nitawajibu hawa wasomi wacahche wa Ph.D walioamua kumtetea wanayemuita "Ph.D Holder" mwenzao kwa kurusha vijembe na kuibua vioja badala ya hoja.Lakini wajue suala hili halitaishia hapa linaenda beyond huu mjadala.Nashukuru tu kwa wale waliotoa ushirikiano na kutupa data nyingine ambazo ni classified.Tutajuana mbele ya safari.Maana nimeona dalili za kuja kuibua hadi kuanzia wajumbe wa Bodi hadi katibu Tawala wa mkoa fulani huko wa kanda ya Kati.

Hahahaha! Hapa Iundwe tume tu sasa! Na itakuja na majibu Ph.D Thesis ilitetewa kwa lugha gani.Yote yatabainika tu.

1:Evarist Chahali anaandika "nasikitika kuona Ph.D Mwenzetu tena aliyesoma Sayansi akituhumiwa bila uthibitisho wowote.......sisi wengine tuko huku scotland tunazeekea PhD" Kisha anaandika "...sioni kosa lolote kwa yeye kumteua profesa aliyesimamia Ph.D yake kwani hata kama ingekua ni mimi ningemteua kwani unapaswa kumteua mtu unayemfahamu vizuri....'.Aaliandika hayo na mengine mengi tu

MAJIBU YANGU:

-Chahali hakuna jibu lolote ulilotoa kujibu hoja za uhalalali wa Ph.D ya magufuli na wala hujaweza kumtetea vizuri kwa hoja za kisomi kuwa ni kwanini asihakikikwe .

Suala la wewe kukaribia kuzeekea Ph.D ni suala linalohusiana na uwezo binafsi kichwani tu wala sio suala la kutufanya wengine tushindwe kuhoji uhalali wa Ph.D ya Magufuli

Nilidhani kwa mimi kuhoji uhalali wake ingekuwa ni suala ambalo wewe Ph.D holder ulipaswa kuliunga mkono ili kuepusha taaluma ya kiwango cha Ph.D kudhalilishwa kwa watu wanaozipata kwa njia zisizofaa

-Hivi kwa msomi wa kiwango chako hukuona uchungu alipowaita watoto wa watu vilaza pasipo uthibitisho wowote kisayansi lakini unaibuka eti kuona uchungu kwa Ph.D mwenzako kutuhumiwa?

-Katika majibu yako ulinitaja Ben mara nyingi kwelikweli.Hii sio dalili nzuri kwa msomi wa ngazi ya Ph.D tena Mwalimu wa lugha ya kiswahili huko Glasgow Scotland

-Pia ulisema eti machapisho ya Ph.D hayadaiwi Facebook.Cha ajabu utetezi wako uliojaribu kuutoa kutetea hoja dhidi ya taaluma ya mhe.Magufuli uliutolea hukuhuku Facebook.Labda vilevile unaonekana kwamba uelewa wako kwenye maendeleo ya sayansi na Teknolojia ya Habari uko katika kiwango kisichoridhisha. Facebook ni mtandao wa kijamii na watumiaji wake wanaweza kujadili lolote hata miswada ya sheria au rasimu ya katiba au jambo lolote zito

-Pia inaonekana suala la uadilifu kwako si jambo kubwa.Hivi tukianza kufikiria kuteuana kwa sababu unanijua au kwa sababu ni rafiki yako tuliwahi kusoma pamoja au uliwahi kunifundisha kitakuzuia nini kumteau mtu kisa nimelala nae chumbani?

Kama kwenye Lecture za Ph.D hukuwahi kukutana na lecture ya moral values katika stage za awali kabisa za Literature basi si kosa lako.Vinginevyo ungekutana na theory za akina Trevino na Nelson kwenye Ethnical Problems au Rushworth Kidder kwenye "Trilemma conflicts"

Leo tunapambana na ufisadi,tunapambana na utamaduni wa kubebana na kulindana (Culture of Nepotism and Impunity) halafu msomi wa Ph.D uanaandika kwa utetezi wa ajabu kabisa kama huu?

Sikushangai ndio maana hata katika majibu yako ulishindwa kutangaza mgogoro wa kimaslahi ulio nao kwani wewe ni mfanyabiashara unayefanya biashara kwa mgongo wa jina la Magufuli

Pengine utetezi wako wa usiokuwa wa kisomi umelazimika kuufanya kutokana na aidha biashara hiyo au pengine ulipokuwa(sidhani kama uliacha) Usalama wa taifa ulikula kiapo cha utiifu kwa rais badala ya Utiifu kwa Jamhuri ya Muungano.

Next time ukija na Utetezi hapa njoo na Utetezi wa kisomi na uje na majibu ya kutosha.Magufuli alisomaje Ph.D kwa miaka 3 wakati hakua fulltime student? Tuanzie hapo tu maana huko kwingine ni kuzito kwako

Prospectus ya UDSM ina sharti lifuatalo juu ya muda kwa wanafunzi wa Ph.D:
7.2.7 a The duration of the registration period, including the six months of
research proposal processing, shall be three years for full time and
five years for part-time candidates.

Kwa kipengele hicho tu ungetuambia basi ni vipi Magufuli alipewa Ph.D.

2: Dr.Lawi Yohana anaandika "Njoo kwangu nikupatie ufafanuzi.Mheshimiwa tulikuwa nae darasa moja.Tafuta reserach gap au problem statement ya Chapisho lake ndio utajua''

MAJIBU YANGU:

Sihitaji kuja kwako kupata ufafanuzi. Ni aidha yeye Mhe.Magufuli atoke front au chuo kiseme vinginevyo zoezi hili la uhakiki linahitaji sasa iundwe tume huru kuchunguza taaluma za viongozi wakuu na zile zenye mashaka basi wahusika wakazi-defend upya na wakishindwa wapelekwe mahakamani.

Nilishasema Profesa wake aliyesimamia Thesis yake hapaswi tena kutoka hadharani kama alivyokuwa prof.Michael Baron aliyesimamia thesis ya Barack Obama.Huyu aliyesimamia ya Mhe.Magufuli hawezi kuwa na moral authority tena maana tayari ameshateuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya TIB .Aliteuliwa haraka hata kabla Rais Magufuli kumalizsa Mwaka mmoja Madarakani

Kuhusu hilo la Research Gap sasa ndipo tunapotaka kuona namna Mhe.Magufuli alivyoonesha weledi kwenye Empirical method,Conflict statement na ni kitu gani kipya alichojibu kupitia utafiti wake. Sasa wewe una uwezo gani wa kuja na majibu ya kisomi zaidi ya kutishia watu tu kuwa alikuwa Classmate wako au eti nije kwako ukanifafanulie

Halafu inanishangaza kuwa wewe ni Mkurugenzi wa Mitihani Chuo kikuu Huria lakini hupendi kusoma instructions ukaelewa kabla ya kujibu.Niliandika angalizo kabisa katika ile post yangu kwamba asije akaibuka mtu huko akamtetea kwa hoja kuwa eti anathibitisha Uhalali wa Ph.D ya Mhe.Magufuli kwa kuwa alikutana nae kwenye kordo au cafteria.Sio utetezi wa kisomi.Au eti kusema tu nilikuwa nae darasa moja.Sio utetezi wa kisomi

3: Dr.Rose-Mary Chisha anaandika '' Unapenda sana Ligi.Kwani Magufuli alikufanya nini?Ben stop being radical on your critiscism.What advise do you have for the prospective Ph.D Candidates then"?

MAJIBU YANGU:

-Yeyea alivyoamrisha Uhakiki wa Vyeti alilenga kuanzisha ligi? Advise to Prospective Ph.D Candidates? Well,

For you PhD, ensure your literature review, statement of research problem and methodology are very rich. Try and sharpen your focus so that you don't digress. In other words, narrow your focus to what you actually intend to research on. Read at least 50 papers/books in your particular area to broaden your mind and to find out what others have done and how they did it. You don't have to repeat a research unless you wish to disprove or further the work. Your research should actually contribute to the existing body of knowledge not duplicating any part of it.

4:Dr: Gladys Malongo anaandika 'Hakuna asiyejua kuwa Rais Magufuli ni mtu mwenye akili nyingi na mchapakazi hodari.Kama alisoma miaka 3 huoni kuwa ni genius? Mtoto wake wa kiume amesoma na wanangu wanasema ana akili sana.Huyo Ben Saanane aache upotoshaji na siasa chafu."

Majibu Yangu:
-Kipimo cha akili nyingi ni nini?
-Mwanao kusoma na mtoto wake wa kiume na kusema ana akili ndio uhalali wa mtu kusoma Ph.D miaka 3 kinyume na masharti ya chuo na pia inahalalishaje chapisho lake? Kwa hiyo huo ndio uhakiki?
-Halafu kwa taarifa yako hiyo hoja ya kuwa na mtoto wa Kiume mwenye akili bora usingeiweka hapa

Uthibitisho wa kisayansi ni kuwa Uwezo wa akili (IQ) ya Mtoto wa Kiume hurithi kutoka kwa mama na ile ya mtoto wa kike hurithi kutoka kwa baba.Sasa sijui yule Mtoto wa kule UDOM unataka kutukumbusha jambo gani?Angalia badala ya kutetea ukajikuta unazidi kummaliza

-Hana historia ya kuwa Genius akiwa sekondari na historia yake kitaaluma inaonesha alijiunga Diploma ndipo akaibukia kwenye digrii.Kipindi hicho hakua na majukumu ya kifamilia au majukumu makubwa kiuongozi.Ph.D kasoma akiwa na familia na pia mbunge na waziri.Linganisha hapo.

-Halafu uchapakazi hodari pia kwenye somo la saikolojia kuna cognitive theory ambayo inasema watu ambao ni hardworking sana hawana IQ kubwa. Prof.Kitila unaweza kumsaidia huyu mama (Ph.D Holder)

5: Dr. Faustin Masanja anaandika 'Ben Saanane labda aseme ni kwanini specifically amaeamua Ph.D ya magufuli na sio wengine.Au bado ni hasira za uchaguzi maana Wachagga awalikuwa wamejipanga kweli kukamata dola.Kwani kama alifanya analysis kwa ushirikiano na wengine ni kosa?he should show some respect to Ph.D holder maana yeye bado jasho linamtoka hajaipata bado.Ana ahasira zake tu,tuachane nae"

MAJIBU YANGU:

-Kwa hiyo wewe umemtetea kwa hoja ya ukabila? Duh

-Ona sasa ,Tangu lini katika Thesis ukashirikiana na mtu kufanya analysis? Hivi wewe nawe ulifanya Ph.D kweli? Unaweza kushirikiana na wengine katika stage mbalimbali lakini linapokuja suala la Interpretation ni jambo lingine na ndio maana kama kweli ulifanya Ph.D utakua uliweka Tamko la kiapo(Declaration statement) kama hii hapa chini

"Declaration

The experiments described in this thesis were carried out by myself and, where indicated, in collaboration with colleagues. The data analysis and interpretation is my own work. This thesis has been written entirely by myself. "

Next time usije tena kujianika hadharani hivi.Halafu unasema "Tuachane nae".Ninyi akina nani sasa? Huko ni kukimbia mjadala

That is an excuse to run away from the truth of the matter. It is clear most of you PhD holders are not qualified to defend what you have in the public.

Thank you.Tena pole Dr.
Yaani ninyi na Ph.D wenzenu mlioamua kumiminika kuja kumtetea hakuna scholarly argument mliyojenga kujibu hoja zaidi ya kuleta hekaya ,kejeli na kulialia tu

6:Dr.Helga Urio anaandika "Nimesoma andiko la ben Saanane .Ameandika ila tu amesahau kuandika kuhusu yeye hapo Mlimani alipata ngapi .Hata yeye tunaweza kuweka zake hadharani"

MAJIBU YANGU:

-Dr.Helga nakuheshimu. Kama una matokeo yangu hapo mlimani weka.
-Wewe unajua hapo mlimani nilifanya Matriculation tu na kisha nikaja hapo wizarani kipindi hicho ikiitwa Wizara ya Elimu ya Juu kuchukua barua iliyoandikwa na Katibu mkuu wa wizara kipindi hicho Dr.Naomi Katunzi kwa ajili ya Kuanza maandalizi ya kwenda nje ya nchi kwa masomo tena kwa udhamini wa serikali na wanafunzi wenzangu.Hiyo ilikuwa mwezi Agosti 2005

-Kama ni Matokeo yangu hapo wizarani mnayajua maana chuo kilikua kinayapost Ubalozini na Wizarani .Ni First Class with Hons. Acha kupotosha Umma

Badala yake jibu hizi hoja za uhakiki wa vyeti badala ya kujiletea vihoja.Ni suala la Uadilifu hapa.We are not doing dramma

Magufuli rode to power on the back of being incorruptible and for being touted as a man of impeccable integrity. It is a moral burden for the President, so it matters.

Unless someone exhausts on this to our full comprehension, Magufuli's Ph.D and the college he went through remain flagged!!

A Luta continua,Victory ascerta........

Ben Saanane
 
Back
Top Bottom