Emoj
JF-Expert Member
- Oct 9, 2015
- 838
- 1,302
Marafiki ni watu wazuri sana ila ni watu wabaya sana ukikosea katika kuwachagua maana unawezajuta maisha yako yote.Mwanamke mwenzangu ulieolewa sio kila mwanamke ni wa kuwa nae rafiki hasa baada ya kuolewa.
Ni vyema kuwa na rafiki anaeamini katika ndoa na mwenye Imani na Dini na pia awe ameolewa. Itawasaidia sana katika kujengana kiimani na katika familia zenu.Achana kabisa na marafi wasio na faida kwako na wasio amini katika ndoa, Epuka marafiki ambao nyie kila siku ni kusengenya mara fulani kafanya hivi mara sijui nani yuko hivi mara tutafute mchepuko. Achana nao.
Marafiki wa kuwa nao ni wale wanaoamini katika ndoa na wanaokusaidia kujenga future yako na familia kingine mwanamke umeolewa tambua wewe ni mama wa familia na familia bora hujengwa na mama bora, mambo ya kutukana mtaani au kwa social media haipendezi.
Familia bora itatoka wapi kama mama wa familia umeolewa hujitambui kila siku kugombana na watu na kutukana mara uko na marafiki wasioeleweka?.Watoto utawalea katika maadili gani kama mama uko hovyo?.Hakuna mwanaume anayependa mwanamke ambaye yeye kila siku kwake haishiwi vituko na mikasa.
JIHESHIMU KAMA MAMA WA FAMILIA BORA.