kikurajembe Original 2015
Senior Member
- Feb 27, 2016
- 109
- 138
Wana JF,
Naamini Mungu amewapa siku njema. Hongereni na poleni kwa majukumu mazito ya long-weekend ya Easter Holiday.
Miezi kadhaa iliyopita tulishuhudia kwenye vyombo vya habari kuwa mwanamke mmoja jina-SOPHIA MANGANYE kama sijakosea ubini kwa kuwa ni jina la kikabila naweza kuwa nimekosea waliofuatilia kwa makini na wanaofahamu majina haya ya kikuria wanaweza kunisahihisha lakini ujumbe wangu kwenu wana jf,serikali yetu na waheshimiwa wabunge kwa ujumla bila kujali vyama,ni kama ifuatavyo;
Nilichokiona leo STARTV katika kipindi cha makala maalumu kwa ajili ya huyu mama ni kwamba; mwanamke huyu shujaa SOPHIA haikuwa mara yake ya kwanza kuvamiwa na majambazi na kukataa uonevu kwa haraka.
Taarifa zinaonyesha kuwa alishawahi kuvamiwa hapo awali akiwa nyumbani kwake na pia alithubutu kuhatarisha maisha yake kwa kubishana nao na aling'a ng'ania silaha aina ya smg-SUB MACHINE GUN ikiwa na magazine yenye risasi thelathin karibia aichukue. Kilichomsaidia kaka jambazi ni kitendo cha kuvaa mkanda shingoni hivyo mwanamama akashindwa kuichukuwa.
Endapo mama huyo angekuwa na mafunzo kidogo hata ya militia,angejua ku"pool traiger" tungekuwa na mahesabu mengine.Jambazi alipiga kelele na wenzie walikuja na kumuokoa mwenzao na mama yetu alipokea kipigo kitakatifu,akaachia silaha wakakimbia mwituni.Luckly walimuachia roho yake kwakuwa alikuwa ameshapiga kelele sana watu wengi walikuwa wameanza kufika.
Tukio kama hilo likamtokea tena lakini safari hii akiwa dukani kwake,majambazi walimvamia na kumtaka awape pesa akazubaa kidogo kama anayewatafutia kwenye madroo ghafla akashikilia bunduki upande wakitako huku akipiga ndulu-kelele.
Kaka jamabazi alitumia nguvu zake zote lakini hakuweza kumgeuzia mama mtutu wala kufanikiwa kushika "triager". Safari hii kelele na maamuzi yake yakijasiri yalizaa matunda kwani majambazi waliposikia ujio wa polisi na baadhi ya wasamaria wema wasio na woga walikimbia na kumuachia mama yetu shujaa SOPHIA hiyo silaha na kutokomea kusiko julikana.
Kitendo cha ku"risk' au kuhatarisha maisha yako kwa kupambana na majitu yasiyo na huruma,tena yaliyozoea kujipatia mali za watu bila ridhaa yao.kutumia nguvu na kuua watu wasio na hatia mara kwa mara. kwakweli mwana JF utaniunga mkono ni jambo la kijasiri sana.
Honestly,hata baadhi ya sisi wanaume huwa ni kwa nadra sana kufanya maamuzi magumu kama aliyofanya mama yetu Sophia.Mara nyingi huwa tunatii amri kuwekwa chini ya ulinzi wanaiba na kutuua. Ama tukijarubu ku-resist tunaishia kupigwa risasi na kupoteza maisha. "Rejea tukio la wizi NBC kariakoo muhasibu alipojaribu kupambana na majambaz wa bodaboda ili wasimnyange mfuko wa pesa kwa sasa hatunaye ni marehemu".Kaka yetu yule aliyekuwa Airtel na pia akahamia Zantel,aliyejenga mjengo salasala hata hakufanikiwa kuzindua na kuishi humo,alikuwa na mfuko wa mil.10.alipoambiwa lete akabishana nao kirahisi walimmiminia risasi kifuani na kumuua kisha kutokomea. Matukio mengi sana ya namna hii wanaume huwa tunaishia kuuwawa.
MAAJABU: "WATAKAO LETA SILAHA KWA HIYARI YAO HATA AKISEMA AMEOKOTA PORINI KUPEWA SHS MILLIONI MOJA-TZS 1000,000"-MH.PAUL MAKONDA RC DSM; ALIYEPIGANA NA MAJAMBAZI KIASI CHA KUHATARISHA MAISHA YAKE,NDG ZAKE NA MAJIRANI ZAKE-SERIKALI KUPITIA JESHI LA POLISI SHS LAKI 5
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kamanda wetu Gemin Mushi alijitahidi kwa uwezo wa office yake baada ya kupata silaha iliyokombolewa kutoka mikononi mwa majambazi na mama yetu Sophia wakampa zawadi ya shs laki Tano TZS 500,000/= Sikatai tena nampongeza sana Kamanda Mushi lakini serikali yetu,wanabodi na wabunge hiyo ni sawa?
Lazima tujiulize maswali haya,
1.Mama yetu ambaye alikiri kwa kinywa chake kuwa yeye ni mama mwenye mume na familia ya watoto kumi.kwakuwa ameshajitokeza kuonyesha anaweza mapambano na majambazi maisha yake hayapo hatarini?
2.Kwakuhatarisha maisha yake ana-security gani?
3.Kama mwanamke Taifa limemfanyia nini? Kuna mwingine sina hakika lakini nasikia alipambana na majangili wasiue wanyama pori akapewa pesa ya kutosha,akapandishwa cheo,akapewa tuzo, akapelekwa nje ya nchi,na amekuwa kama sehemu ya utalii wa ndani.kila anayefika hapo mbugani anaitwa kuonyeshwa yule askari aliyetetea wanayama pori wasiuwawe je aliyetetea
maisha ya binadamu?
4.Pamoja na kamanda G.MUSHI kutangaza kuwa mtu atakayetaka kwenda kumuona ama kuongea na huyo mama lazima akachukue baraua ya polisi ama lazima apitie polisi ili wamfahamu anahitaji nini,anatoka wapi? ni vizuri lakini haitoshi. Je anayetaka kumuua atapitia polisi kuhojiwa kwanza? na atakuwa tayari kusema nia yake ovu?
USHAURI KWA SERIKALI:
1. Nashauri jeshi la polisi kila siku wafanye doria maeneo hayo na wawe na tabia ya kupaki landcruizer yetu yenye maandishi 6 POLICE wakagonge hodi kwa mama na kuwajulia hali, jambo hilo litawatia hofu watu wabaya wenye nia ya kumuangamiza mama yetu shujaa.Mkumbuke silaha moja ikiwa mikononi mwa adui yaweza kuangamiza mamia ya roho za raia wema wasio na hatia.
Aidha pia ni vema kufikiri kitendo cha kwenda kuwasaka majambazi porini,msituni ama kwenye makazi yao ili kuwanyanganya silaha moja waliyoiiba mikononi mwa walinzi wetu huwa inatugharimu roho za watu wangapi? tena sio roho za majambazi peke yao,raia wema wapita njia ya mapambano ama wakati mwingine twaweza kupoteza hata roho za hao askari wetu wenyewe. SWALI: Je mama yetu Sophia kupata silaha-smg hiyo kumegharimu roho za watu wangapi?.Ndiyo maana tunasema.
2.Zawadi nzuri kwa mama wamjengee uzio wa nyumba yake ama wampe pesa ya kutosha ajenge mwenyewe.
3.Ufanyike utaratibu wa kumhusisha katika dhana ya ulinzi shirikishi
4.Kama serikali au taifa kwa ujumla wafanye jambo la kumbukumbu kwa huyu mama
5.Wabunge wote kwa ujumla wao bila kujali ccm,cuf wala chadema wakirudi bungeni wapaze sauti,kumsaidia huyu mama,wamchangie hela kidogo hata shs elfu hamsini kila mmoja,wamkabidhi Mh.Speaker.kisha aitwe bungeni ili kuthamini mchango wake na kuumpa "recognition"
Tena waongozwe na Mh.Esther Bulaya na Esther Matiko na wabunge wengine wa huko Rorya au mkoa mzima wa mara. Mkiacha naamini wabunge wa mkoa wa DSM watapitia hapa na watapaza sauti.Mh.Mdee,Mnyika,Mtolea,Dr.Faustine,kubenea,Zungu.
Mbarikiwe