Mwanamke ni sawa na kivuli

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Posts
23,367
Reaction score
55,053
Huu ni mfano tosha ambao unaweza kuwaelezea wanawake kwa usahihi zaidi pale anapokuwa kwenye mahusiano yasiyo ya kweli.

Sifa moja ya kivuli huonekana baada ya mwanga kummlika kitu na baadae hutokea kivuli cha hicho kitu kilichomulikwa na mwanga.

Sasa hivi kwa wale wote ambao wanahangaika katika mapenzi yao basi fahamu kuwa kivuli hakiwezi onekana sehemu isiyo na mwanga yaani naamanisha kuwa mwanamke atatokea kwako kama kivuli ila mwanga ukizima basi habari imekwisha.

Pongezi kwako mwanamke ambaye huna tabia za kivuli kutokea kwenye mwanga, kila la kheri wenzangu mliobahatika kukutana na wanawake wasio na sifa hizi ila tujipongeze na sisi wenye wanawake vivuli katika mahusiano maana tunavumilia mengi.
 
Daa nyie watu ni hatari kwa misemo Raphael umewaza nn mkuu yamekukuta Poti wangu???[emoji15][emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Daa nyie watu ni hatari kwa misemo Raphael umewaza nn mkuu yamekukuta Poti wangu???[emoji15][emoji2] [emoji2] [emoji2]
Tetemeko linaninyemelea na dalili zote zipo wazi, nimejiandaa pia kisaikolojia nisije kuathirika nalo.
 
Wanawake wengi hawapo tayar ku grow na mwanaume.. hawako tayar kuanza na mtu from the bottom to the top.. wanachotaka akukute tayar upo on top.. ndo maana wanaume wenye pesa wengi huwasumbua sana wanawake kwenye mahusiano coz haoni hatar kwan mwanamke kamsaidia kufika hapo alipo?? wala haoni uzito kukutupa kuleee..... msyuuuuuu... me napita tu
 
Great thinker, pita tu leseni yako imekidhi vigezo mkuu.
 
Sio hatuko tayari kuanza na mtu chini...

Tatizo baada ya mafanikio mnaanza kutugeuka. Mliechuma nae hamuwajali tena mnahangaika na wanje ambao wala hawajui tumepitia mangapi mpaka kufika hapo.

Sasa mtu anaona ya nini apoteze nguvu na muda wake then aje kulia huko mbele,anaona bora atafute mwenye nazo tayari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…