Mwanamke mwema

Mke mwema ni Mungu tu anaweza kukuunganisha naye. Lakini vigezo vya mke mwema vinafahamika. Jambo la kwanza ni awe na hofu ya Mungu. Kama hawezi kumjali Mungu unadhani atakujali wewe? Msichana ambaye kutoa mimba kwake ni jambo rahisi atashindwaje kutoa penzi kwa wanaume wengine kirahisi? Pili ni lazima muwe na mambo mengi ya kushabihiana. Kama yeye anapenda kuangalia muvi wewe hupendi anapenda kutoka out wewe hutaki si mtakorofishana tu? Tatu ni lazima mke wako awe anakuthamini wewe kuliko marafiki zake na jamaa zake. Bila hivyo watamyumbisha kwa kumjaza maneno yatakayoleta ugomvi kati yenu. Nne ni lazima wewe na mkeo muwe mnawasiliana kwa uwazi bila kufichana lolote. Kama mmoja wenu ataudhika halafu hasemi akikaa na hasira moyoni jambo dogo likitokea siku ingine anaweza 'alipuke' kwa hasira umshangae - kumbe kuna hasira ya siku nyingi ilikuwa imejificha. Ukitaka kujua kama hizo tabia nilizotaja ziko ndani ya mpenzi wako usianze naye mahusiano ya kingono maana 'ukishajikamatisha' hivyo huwezi tena kumchunguza ipasavyo.
 
Nice point
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…