Habari zenu wakuu.
Ni miezi sasa nipo na huyu binti kwenye mahusiano, ikatokea kwenye kurupushani za kwichi kwichi akapata mimba, akaniuliza utailea? Nikasema yes nitailea usitoe, basi nikaanza kuilea kidogo kidogo mpaka sasa ina miezi mitatu.
Kilichonifanya niandike post hii ni kutaka ushauri kwa lifuatalo.
Siku chache zilizopita uchumi wangu haukuwa sawa, kwa hiyo alipohitaji kitu sikuweza kumpa kwa muda huo, hiyo hali ikaendelea hivyo akawa anabadilika akisikia kuwa sina, ilipofika mahali akaniambia ataitoa mimba kwa kuwa siihudumii, hapa alifikia kuniambia kuwa sina tofauti na mtu aliyeikataa mimba( Hapa nilistaajabu kwa kuwa nimekubali na nimemhudumia kwa kipindi fulani). Tulipofika hapo nikamuambia ok itoe tu maana niliona hana shukurani, nikakata mawasiliano.
Baada ya wiki akanitafuta anahitaji mawasiliano na mimi nikamuambia nakusikiliza, akasema anahitaji tuwe kama zamani nikamuuliza mimba umetoa akasema hapana, nikamwambia hakuna shida( hapa nikiri udhaifu wangu kwa kuwa namhitaji mtoto) ikabidi nikubali.
Sasa basi juzi hii ninapiga simu mchana kutwa hapokei na message hajibu kupatikana usiku nikamuuliza ulikuwa wapi akasema nilikuwa kwenye semina ninamtafutia mtoto mahitaji madogo, nikamuuliza yapi? Akasema hawezi kuniambia kwa kuwa sina hela! Kumuuliza zaidi akaanza kuwaka, kuona hivyo nikamuambia usijali sitakusumbua maana naona uko busy sana, akasema sawa! Baada ya muda akanitumia sms akisema nimemkana mtoto nitamtafuta tu kuwa damu ni nzito kuliko maji, wakati kiuhalisia sijaikana mimba wala kuitilia shaka, ila ni kama ananishurutisha niikane.
Sasa anachukulia udhaifu wangu wa kukosa hela kwa kipindi kifupi kunipelekesha kwa kuwa namhitaji mtoto mtarajiwa, ukizingatia kwamba hajui kuomba kitu kwa ustaarabu na kauli zake ninachoka kabisa niamue nini.
Ushauri wenu wakuu.
Samahani kwa gazeti.