JAMII-ASM
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 1,305
- 524
Tukio la kusikitisha lililompata mwanamama kutoka Canada mwalimu Amanda Furst akiwa nchini Tanzania ni moja ya matukio mengi ya kusikitisha yanayoipa nchi yetu sura isiyofaa na kutufedhehesha sote tunaojiita Watanzania... watu tunaofahamika duniani kwa ukarimu wetu na wapenda amani wa kupigiwa mfano.
Amanda kaishi Afrika kwa zaidi ya miaka kumi akisaidia jamii maskini vijijini kwa kuanzisha miradi ya vituo vya kijamii,vituo vya kulea watoto na uvunaji wa maji ya mvua.Hata kufikia kutunikiwa tuzo ya The Manitoba Red Cross Young Humanitarian of the Year mwaka 2011.
Lakini tarehe 29 Julai ni siku ambayo hatoisahau maishani mwake.
Akiwa Kisesa Tanzania kukamilisha ndoto yake kubwa ya ujenzi wa kituo cha kijamii Hero's Home Community Centre alivamiwa na kijana mmoja muda wa asubuhi akiwa anafanya mazoezi ya jogging.
Kwa mujibu wa maelezo ya Amanda huyu kijana alikuwa anaomba hela...ghafla huyu kijana akamrukia Amanda na kumkaba shingoni na kumvuta pembeni ya barabara na kuanza kumbaka.
Katika jitihada za kujinasua Amanda alipiga kelele kuomba msaada. Huyu kijana akachomoa kisu na kuanza kumkata sehemu za mikononi.Akajaribu kumchoma kisu tumboni..lakini hakuweza.. kwani wanakijiji walishakaribia...na kumfanya kijana huyu akimbie.
Amanda alifanyiwa operesheni tatu za kunusuru mikono yake Daresalaam na Nairobi.
Alipigwa sindano nyingi za kuzuia asipate maambukizi ya ukimwi- anti-viral drugs injections..Alieleza jinsi alivyopata tabu katika matibabu yake..na hasa pale alipokuwa anatibiwa kwa sindano chafu.
Kikubwa alichoeleza ni kukithiri kwa rushwa kwenye vyombo vya utoaji haki Tanzania...kwani mpaka leo mbakaji hajakamatwa. Anasema badala yake wamemkamata na kumuweka ndani rafiki yake na hawataki kumuachia mpaka atoe rushwa.
Licha ya masaibu yote yaliyompata yeye yuko tayari kusamehe... na amepanga kurejea Tanzania kuendeleza shughuli zake za kusaidia jamiii maskini.
Winnipegger attacked in Tanzania; Vows to continue humanitarian work with "incredible" co-workers
Winnipeg teacher returning to Tanzania despite attack