Mchakamchaka wa kuomba kuteuliwa Kugombea Ubunge katika Jimbo la Kigamboni Jijini Dar es salaam zimeanza kupamba moto ambapo leo Katibu wa Idara ya Mambo ya nje ya chama cha Act-Wazalendo Wakili MWANAISHA MNDEME amechukua fomu ya kuomba Chama hicho kumpa ridhaa ya kugombea katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hiyo amesema endapo atapewa ridhaa amesema atahakikisha anakuwa sauti ya Wananchi hususan Wanakigamboni kutokana na changamoto nyingi walizonazo zikiwemo za Miundombinu ambazo zinasababisha maisha yao kuwa ya gharama ya juu.
Aidha amesema atatumia vizuri taaluma yake ya Sheria kushiriki kutunga Sheria zenye tija na zitakazowasaidia Watanzania wote kunufaika na Rasilimali nyingi zilizopo na hivyo kuharakisha Maendeleo yao na ya Taifa.