Mwanafunzi wa darasa la Sita aozeshwa

Mwanafunzi wa darasa la Sita aozeshwa

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
42,451
Reaction score
50,186
Dar es Salaam
Mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kigezi iliyoko Chanika, wilayani Ilala, Dar es Salaam (jina linahifadhiwa), ameolewa na mkazi wa Mbondole, Halfa Ally (54) ambaye humfungia ndani ili wakazi wa eneo hilo wasimuone.

Mama wa mtoto huyo, alisema jana kuwa alipata taarifa kutoka kwa mdogo wake aliyekuwa akiishi eneo hilo kuwa mwanaye anaishi na mwanaume huyo zaidi ya mwezi mmoja na nusu na huwa anamfungia ndani ili asitoke nje.

Alisema mtoto huyo alikuwa anaishi na baba yake mzazi kwa zaidi ya mwezi mmoja eneo la Kivule, alishangaa kusikia kuwa mwanaye ameolewa na anaishi Mbondole.

"Nakumbuka ilikuwa Oktoba 7, mwaka huu tulitoa taarifa kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa, tulishirikiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi wa mtaa huo ambao tulifika eneo hilo saa moja asubuhi hadi saa 8 mchana na tulifanikiwa kumkamata mtuhumiwa," alisema mama wa mtoto huyo.

Alisema walishangazwa na kitendo cha mwenyekiti wa serikali ya mtaa kumwachia huru mtuhumiwa bila kumchukulia hatua zaidi. "Aliniambia tulimalize tu suala hili kienyeji ila niende duka la dawa nikanunue kipimo cha mimba ili tuangalie kama mtoto atakuwa kapata ujauzito na kama hana aendelee na shule."

Mwenyekiti wa Mtaa huo, Salum Matangula alikiri kutokea kwa tukio hilo na alisema kilichotokea ni mtuhumiwa huyo alikiri mbele ya kikao kuwa alipewa ruhusa na mama mzazi wa mtoto huyo aishi naye.

Alisema kutokana na maelezo ya pande zote, walibaini wote wana makosa ndipo walipomtaka mama huyo aende kwenye duka la dawa ili achukuliwe kipimo cha mimba na baada ya hapo ampeleke mwanafunzi huyo shuleni.

"Niliwaeleza kuwa wote wana makosa, mama alikuwa anadai mwanaye akapime kwanza, nikamruhusu, lakini sijapata majibu hadi leo," alisema Matangula.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kigezi, Joseph Kalungutu alisema mwanafunzi huyo ni mtoro na kipindi cha nyuma alikuwa akihudhuria darasani mara moja moja na lakini kuanzia Septemba, mwaka huu, hajaonekana kabisa shuleni.

"Mahudhurio ya mwanafunzi huyu ni mabaya, kuanzia Mei 14, mwaka huu hakuingia darasani lakini ilipofika Juni alionekana wiki moja, Julai alikuja siku mbili na Agosti aliingia darasani kwa siku nne tu," alisema.

Mwanafunzi huyo alisema waliishi na mwanaume huyo kuanzia Septemba, mwaka huu, baada ya kuchukuliwa nyumbani alikokuwa anaishi na baba yake mzazi eneo la Kivule.

"Alinichukua kama mke wake na kuniambia kuwa ninaenda kwake kumlelea watoto wake watatu ambao walikuwa hawana mlezi," alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema hajapata taarifa hiyo na kuahidi kufuatilia ili mtuhumiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Ally alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo, alisema ni kweli msichana huyo anamfahamu na alikuwa anaishi naye. "Sina cha kukueleza zaidi ya hayo ninachofahamu huyo binti nilikuwa naishi naye," alisema Ally.

Chanzo:Mwananchi


 
Ana miaka mingapi?
kuna baadhi ya jamii hapa nchini ni vigumu sana kuja kubadilika.
 
Ana miaka mingapi?
kuna baadhi ya jamii hapa nchini ni vigumu sana kuja kubadilika.


Haijafahamika umri wake ni miaka mingapi, inasikitisha, yawezekana huyu ni mmoja kati ya wengi wanaoozeshwa kimyakimya ila taarifa hazifiki kwa vyombo husika
 
Wazazi tuweni makini na watoto wetu wa baba akili zao sio nzuri kweli mtoto mdogo hivyo kuozeshwa kwa lizee si umri kama wa baba yake. Duuh inaskitisha jamani
 
Miaka 54 na mtoto ambae hajavunja hata ungo?! ha ....
 
kwakweli ni ajabu, hilo zee nalo hata halioni aibu kuoa mtoto mdogo sawa na mjukuu wake.
wanawake wa umri wake wamejaa tele..... mwisho wa siku kabinti kanaachwa kajane kakiwa bado kadogo pengine na mzigo wa majukumu kibao ya kulea watoto.
muoaji na baba mkwe wote wanastahili adhabu kali.
 
Is there a problem? best friend!

you are not a woman. sasa utajuaje? ningekuuliza wewe ulianza lini na wenzako walianza lini. Grade 6, 12yrs is the mean age, from my experience.

na mama mtu alikubali bintiye akapimwe mimba so obviously alikuwa tayari.

au labda alikubali apimwe akiogopa wakigundua mtoto bado ni kesi kubwa zaidi? i dont know.
 
Kichwa Ndio Mtu mtoto wa darasa la sita vipi unaoa au unamuacha akue ?

Mkuu kwanza nimeshangaa,kuna mtoto wa ndugu yangu niko nae hapa yuko darasa la sita,10 yrs,niliposoma hii mada na kumuangalia huyu mwanangu nimesikitika sana unawezaje kuoa mtoto wa miaka kati ya 10 hadi 12?

Btw jina la huyo muoaji linaashiria ana imani flani ambayo wao huruhusu kuoa mtoto wa kuanzia miaka 6,lakini pia huruhusu kumchezea kimahaba mtoto wa kuanzia siku moja toka amezaliwa na sio dhambi. Rejea kesi mudy na kale kabinti aisha,alikua na miaka 56 akakaoa kana miaka 6.
 
Back
Top Bottom