Mwanafunzi ukitaka kufaulu mitihani fuata mbinu hizi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,743
25,535
Nini Cha Kufanya Mwanafunzi ?

1. Weka lengo maalumu la kusoma kila siku na litimize.
76eea6aa50d3bb919ce762eef21080b4.jpg

2.Uwe na ratiba yako binafsi ya kujisomea nyumbani na ifuate. Hakikisha ukiwa nyumbani una ratiba ya kujisomea na wala sio unapokuwa shuleni tu.

3. Jisomee katika muda unaodhani unafaa zaidi.

4.Tenga muda wa kutosha kwa kila somo.

5.Yapende masomo yako na tena uyafurahie.

6. Jenga tabia ya kuyaombea masomo yako kila siku na kila mara.

7.Uwe na muda mwingi wa kujisomea kila siku, usipoteze muda kwa mambo yasiyo ya lazima kama vile maongezi,mizaha,utani.

8.Penda kuukomboa wakati ,tambua muda ukipita haurudi tena. EFESO 5:15—17.

9. Waheshimu wale wote wanaokulea na kukuhudumia.

10.Uwe na mahali maalumu pa kusomea.

11.Hakikisha mahali pa kusomea , pana mwanga wa kutosha.

12.Tafuta mahali pasipo na kelele za aina yoyote.

13. Jenga tabia ya kufanya mazoezi ya mwili kama vile kucheza mpira, kuruka kamba n.k.

14. Usifanye mambo mengi kwa wakati mmoja. Kwa mfano, mapenzi au anasa za kimwili wakati ungali mwanafunzi. Hivyo ni vikwazo masomoni.

15.Ni vizuri kujihusisha na watu wengine , jambo hili litakufariji kimawazo.

16. Fanya bidii sana katika kusoma ni lazima UTAFAULU. MITHALI 10:4.



NINI CHA KUFANYA UNAPOKUWA SHULENI / CHUONI/DARASANI ?
5f2a26028812eb4c62f24bd1ecd48d99.jpg


1.Ipende shule unayosoma au chuo unachosoma,hata kama watu wengine wanasema maneno mabaya kuhusu shule yako.

2. Soma kazi zako zote za darasani kabla ya kuanza darasa.

3.Fika darasani kwa wakati unaotakiwa ili usikose maagizo.

4.Usikose kipindi bila sababu maalumu.

5.Wasilisha kazi za darasani kwa wakati wake.

6.Epuka kukaa kimya na nyuma ya darasa,bali shiriki katika mazungumzo ya darasani na wenzako.

7.Usiwe mtu wa kukaa tu darasani , uliza na jibu maswali yanapoulizwa.

8.Wakati mwalimu hajafika darasani , pitia yale uliyojifunza kipindi kilichopita.

9. Msikilize mwalimu anapokuwa anafundisha darasani.

10.Baada ya kipindi, pitia yale uliyojifunza.

11.Jijengee tabia njema ya kujizuia katika tamaa za mwili.

12. Jenga uhusiano mzuri kwa walimu wako na kwa wanafunzi wenzako. Ukiwa
na amani moyoni, utasoma na kuelewa. Jistahi na kuwapenda walimu wako.
Ukimpenda mwalimu utaliewa vizuri somo lake. Wapende walimu wanaokufundisha.Tambua ukimchukia mwalimu na somo analokufundisha lazima utalichukia tu.

13.Hudhuria shughuli zote za shule nje ya darasani.

14.Unapokuwa na matatizo kimasomo, mwone mwalimu anayehusika.

15.Jiandae kwa mitihani kila wakati , usingoje mwalimu atangaze kuwa ataleta mitihani ndipo usome.

16.Epuka kuwaonea WIVU na kujilinganisha na wengine kimasomo, bali, jifunze tu siri za mafanikio yao.

17. Jenga tabia ya uvumilivu na kamwe usikate tama wakati ugumu unapoibuka masomoni.

18. Jenga tabia ya kupania kufaulu katika masomo yako.

19. Amini kuwa utafaulu.

20. Amini na wewe unaweza KUFAULU, hata kama mazingira uliyonayo ni magumu. Mfano U—mtoto Yatima , huna ada ,huna fedha za matumizi “Pocket Money” , husomi masomo ya ziada “ TUITION “ unaishi maisha magumu n.k.

21.Chunguza masomo yako ili ujue udhaifu wako uko wapi.

22.Uwe mwanafunzi mdadisi wa mambo kwa walimu na hata kwa wanafunzi wenzako pia.

23. Epuka marafiki wabaya wenye nia ya kukupotosha.

24.Kaa na wale wanaoweza kile usichokiweza.

25. Ni vizuri pia kuwa na mwanafunzi mwenzio wa kujadili naye.


NINI CHA KUFANYA WAKATI WA KUJISOMEA ?

1.SHETANI hapendi ufanikiwe , hivyo kabla ya kuanza kusoma fanya SALA.

2. Epuka kitu chochote kinachoweza kukufanya usisome vizuri.Hakikishaunapoanza kusoma umekaa mahali ambapo pana utulivu na hupati usumbufu usio na sababu za msingi,

3.Kabla hujaanza kujisomea, hakikisha kuwa zana zote muhimu kwa kusomea zipo, mfano vitabu , kalamu n.k.

4. Ni vizuri ukiwa unasoma uwe na SAA , hii itakusaidia kuelewa muda halisi uliosoma.

5. Wakati wa kusoma hakikisha unakuwa na daftari jingine ambalo utakuwa unaandika mambo usiyoyafahamu vizuri .

6. Epuka kusoma hadi usiku sana , utaharibu afya yako .

7. Usisome mambo mengi kwa wakati mmoja.

8. Epuka kusoma ukiwa umejilaza kitandani.

9.Uwe na muda wa kumpuzika kila unapochoka kusoma.

10. Epuka pombe , uvutaji wa sigara ,bangi na madawa ya kulevya. Huharibu ubongo na
kudhoofisha afya.

11.Kila nafasi unayoipata itumie kwa kusoma.

12. Usiendekeze usingizi katika muda wako wa kujisomea.

13. Soma vitabu mbalimbali vinavyohusiana na hicho unachokisoma.


KABLA YA MTIHANI /BEFORE THE EXAMINATION .

1.Kabla ya mtihani ,soma kwa bidii sana usingoje mtihani umekaribia ndipo usome.

2.Soma kwa mpangilio kila siku ili kujiandaa kikamilifu kwa mtihani.

3. Usitumie vilevi vinavyopelekea mtu kupunguza uwezo wake wa kufikiri. Mfano bangi , bia , sigara ,unga wa kulevya.



SIKU YA MTIHANI / DURING THE EXAMINATION.

1. Usiku unaofuatiwa na siku ya mtihani uwe na muda wa kutosha wa
kulala. Usisome hadi usiku wa manane.

2. Siku ya mtihani, usifikirie kushindwa bali uwe na imani kuwa utashinda. Ondoa wasiwasi na mashaka.

3.Wahi kwenye chumba cha mtihani kwani kuchelewa huleta hofu.

4.Chukua vifaa vyote muhimu katika mtihani kama vile kalamu ,penseli na rula.


NDANI YA CHUMBA CHA MTIHANI.

1.Soma maagizo /maelekezo ya mtihani kwa uangalifu sana ,na hakikisha uko makini kwa kile unachotakiwa kufanya kabla ya kujibu swali lolote.

2.Kabla hujaanza kujibu maswalli ,angalia maswali ambayo ni rahisi kwako
kujibu.

3. Jibu maswali rahisi kwanza na kwa haraka ili upate muda wa kutosha kujibu maswali magumu.

4. Usijibu swali bila kuelewa linataka nini.? Jibu utakalojibu litakuwa tofauti na swali.

5.Usiwe na haraka ya kumaliza mtihani kutakufanya usijibu kwa makini.

Asanteni

Cc : Bacary Superior STUNTER CHAI CHUNGU
 
Mkuu kirikou1 funguka zaidi wenzako wapate maujanja
hahaha, kwanza mkuu Mpalestina Mchizi nimemuelewa sana huyo kirikou kwenye dp

Mimi nilikua nakunja ile karatasi ya rim mara tano kwa urefu then naandika kwa mwandiko mdogo nondo zote za somo moja nakua natembea nayo nikiwa kwenye mpira au sehemu yoyote ila isiwe sehemu iliotulia naitoa nakula desa then nairudisha mfukoni naendelea na misheni town :D:D
 
Yeezus Kwanza nikwambie tu me siyo bwege Kama ulivyosema na Nina akili zangu timamu refers to the aim ya mtoa hoia, kaongelea kuhusu usomaji usome kwa kufata misingii ipi , na pia kabla ya kuingia kwenye paper unapaswa kufanya nn.... Na siyo kwamba hivyo vitu sivijui Na hicho ndicho nilichokichukua sasa wewe unakuja unaanza ku quote mtu vibaya siyo vzr kuingia humu hakunifanyi nisifanye mtiani na hujawahi nifanyia paper all in all inaonekana elimu yako bado ndogo acha kuwa na mawazo mgando Kama ww ni msomi jaribu kuwa na fikra chanya
 
Kwanza nikwambie tu me siyo bwege Kama ulivyosema na Nina akili zangu timamu refers to the aim ya mtoa hoia, kaongelea kuhusu usomaji usome kwa kufata misingii ipi , na pia kabla ya kuingia kwenye paper unapaswa kufanya nn.... Na siyo kwamba hivyo vitu sivijui Na hicho ndicho nilichokichukua sasa wewe unakuja unaanza ku quote mtu vibaya siyo vzr kuingia humu hakunifanyi nisifanye mtiani na hujawahi nifanyia paper all in all inaonekana elimu yako bado ndogo acha kuwa na mawazo mgando Kama ww ni msomi jaribu kuwa na fikra chanya
sawa tutakutana hapa mwezi july na madivision yenu 3,4 au zero

Nakuapia kama utapata division two au one nageuka mwanamke mimi .
 
hahaha, kwanza mkuu Mpalestina Mchizi nimemuelewa sana huyo kirikou kwenye dp

Mimi nilikua nakunja ile karatasi ya rim mara tano kwa urefu then naandika kwa mwandiko mdogo nondo zote za somo moja nakua natembea nayo nikiwa kwenye mpira au sehemu yoyote ila isiwe sehemu iliotulia naitoa nakula desa then nairudisha mfukoni naendelea na misheni town :D:D
saf
 
sawa tutakutana hapa mwezi july na madivision yenu 3,4 au zero

Nakuapia kama utapata division two au one nageuka mwanamke mimi .

Division zinasaidiaga nini kwenye maisha, mavyeti hayana kazi ndani.

Uwe na madivision mazuri kama huna connections ni kazi bure
 
Back
Top Bottom