Mwanafunzi, tumia vizuri muda wako baada ya shule

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
WANAFUNZI wengi wamekuwa wakitumia vibaya muda wao baada ya masomo. Wengine kwa michezo isiyo na maana, kushinda vijiweni, kutazama televisheni kupitiliza au kuwa bize na mitandao ya kijamii ambayo siku hizi imewateka vijana wengi hata ambao hawana faida nayo.

Ukweli ni kwamba wanafunzi wa aina hii, inawezekana kabisa wakawa wanafahamu au hawafahamu kuwa baada ya muda wa masomo ni muhimu kuwa na muda wa ziada wa kufanya mazoezi zaidi ili kupata uzoefu wa kujibu na kuelezea maswali.

Lakini ni muhimu kuwakumbusha ambao wanafahamu ila hawazingatii kuwa ili kufaulu wanatakiwa wautumie muda wao baada ya masomo ya kawaida shuleni vyema. Kwanza kwa kuwa na ratiba ambayo itawaongoza kila siku wafanye nini!
Jambo la kuzingatia pia katika ratiba hiyo ni kuzipa nafasi shughuli nyingine kufanyika. Kwa mfano muda wa kufanya kazi za nyumbani, michezo, kuzungumza na marafiki na kufuatilia vyombo vya habari. Vyote vinatakiwa kuwa kwenye ratiba na kufanyika kwa muda muafaka.

Kwa waliokuwa hawafahamu juu ya suala hili ni muhimu kufahamu ikiwa ni pamoja na kuandaa ratiba yao vizuri na kuifuata pia.
 
Back
Top Bottom