Mwanafunzi aliyeongoza kitaifa matokeo ya kidato cha nne aahidiwa ajira na Benki ya CRDB

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Benki ya CRDB imemfungulia Akaunti ya Scholarship na kumwekea sh. Milioni 5 mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2015, Butogwa Shija na kumwahidi ajira pindi amalizapo masomo.

Hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani leo, ambapo Butogwa alipewa zawadi ili kuwahamasisha watoto wa kike kwamba wanaweza.

Pia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ilimuongezea mwanafunzi huyo kiasi cha shilingi 500,000 lengo likiwa ni kuwahamasisha watoto wa kike ili kuleta haki sawa kwa wote.

Naye Butogwa aliahidi kutumia fursa hiyo vizuri kwa kusoma kwa bidii bila kubweteka na kuwataka wanafunzi wengine kuweka bidii kwenye masomo yao.

Katika hatua nyingine, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Esther Kitoka alisema wametoa sh. milioni 20 zitakazosaidia katika ujenzi wa mabweni kwa watoto wa kike ili kuongeza kasi ya ufaulu kwa wanafunzi
 
Yale yale,aliye nacho huongezewa

Watoto wa private schools wanahaidiwa ajiri mapema

Huku watoto wa kina sisi,pangu pakavu wakizunguka na vyeti mwaka wa tatu huu.

Kibaya zaidi nchi za kiafrika hazijui kutambua na kutumia vipaji vya wasomi wao.

Wanafikiri kumuajiri msomi ndiyo kulisaidia taifa.Inasikitisha

Wenzetu wanarusha Rockets,huku wasomi wetu hata stick za meno hawajui kutengeneza

Hapo napinga,hawahamasishi watoto wa kike,wanaowahamasisha ni watoto wao wa Private schools

Na gape kati ya ukapa na ukwasi linaendelea kutanuka!
 
Duh... Hongera dogo.. huo ni mwanzo mzuri...ila badae ntakuiba
 
Hongera zake.kwakuwa ajira hipo njee namshauli akimaliza form Six asome masomo ya Biashara.BAF ya mzumbe itamfaa
 
Wasingemwambia, sasa hivi ataanza kushoboka kwa wenzake! Nilimuona wakati anahojiwa, uongeaji wake ni wa kasista duu fulani!
Hata hivyo hongera zake, she has to keep her feet on the ground, watu wanapasuaga o level huko juu huwa ni shughuli pevu!
Alafu kwa nini waliofeli hatuwahamSishi?? Hawa ndo wanaoenda kuwa na akili za kujiajiri! Wengi waliojiajiri ni failure wa sekondari!
 
majembe hawaendagi crdb..

dogo kama akimantain ufaulu wake kwa a level na gpa nzuri chuo sizani kama atakubali kwenda crdb na kuacha big 4 proffessional firms zenye ma secondment ya nje ya nchi kibao na mishahara mikubwa kuliko crdb.

yaani aache pwc, kpmg, delloitte, ernst & young aende crdb..

enz zangu za mzumbe university top performers wale ma to wengi BAF walikuwa na scholarship za Zain now Airtel zinaitwa build our nation na field na ajira walishahaidiwa na airtel wakimaliza chuo tu..

ila wote wamekataa kaz za airtel na hata kubaki kifundisha chuo kama tutoria assistant napo walikataa baada ya kupata kpmg, pwc na big 4 zingine..

kichwa gani anaependa kuhesabu na kutunza hela za watu kwa mshahara kiduchu
 
Back
Top Bottom