Jaby'z
JF-Expert Member
- Jan 15, 2013
- 4,300
- 7,624
Thursday, December 29, 2016
MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Isack Macha (25) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa kiume (16), mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Zawadi.
Macha, mkazi wa Kinyerezi Kibaga alihukumiwa kifungo hicho jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Ritha Tarimo. Hakimu Tarimo alisema upande wa mashitaka ulileta mashahidi watano kuthibitisha tuhuma hizo.
Alisema baada ya kupitia ushahidi huo, mahakama imeridhishwa na kwamba mshitakiwa atatakiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kutokana na kitendo hicho.
Katika ushahidi uliotolewa, ilielezwa kuwa mtoto huyo na mshitakiwa walikutana kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook na baada ya kuanza kuwasiliana, walifanikiwa kuonana dukani kwa kaka wa mshitakiwa ambako alimnunulia mtoto huyo suruali yenye gharama ya Sh 25,000 na kuahidiana kuonana.
Ushahidi huo ulieleza kuwa mtoto huyo ndiye aliyetafuta nyumba ya kulala wageni inayojulikana kama Kitas iliyopo Tabata Barakuda na kupewa chumba Februari 10, mwaka huu.
“Mhudumu wa Kitas alipokuja kutoa ushahidi alidai kuwa anamjua mlalamikaji huyo pamoja na baba yake na kwamba siku ya tukio mtoto huyo alimwambia kuwa kuna rafiki yake anahitaji chumba na kumpatia,’’ alisema Hakimu Tarimo.
Pia alisema shahidi huyo alishangaa kuona kwamba mtoto huyo pamoja na mshitakiwa hawatoki ndani ya chumba ndipo alipozunguka dirishani alisikia sauti za miguno ya kimahaba na kugundua kwamba ndio watu hao.
Hata hivyo, mtoto huyo alidai kufanya hivyo kwa kuwa baba na mama yake wametengana hivyo anataka kusaidia familia.
Aidha, kwenye utetezi wa mshitakiwa alikiri kuwepo eneo hilo la tukio na kudai kuwa hakufanya kitendo hicho kwa kuwa mtoto huyo alikuwa na lengo la kumwibia kompyuta mpakato yake.
Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa kuwa vitendo vya ulawiti havikubaliki katika jamii na kwamba kijana huyo ameathirika kisaikolojia.
Mshitakiwa huyo aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ni mwanafunzi na anasumbuliwa na pumu.
Chanzo:Habari Leo