Mwamuzi wa Pambano la UMUGHAKA na GENTAMYCINE , nipo tayari na nitatenda haki.

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
10,985
28,567
Mambo yanaenda kua mazuri,
Nikiwa mtani wa hawa jamaa kikabila na tena mtani mwandamizi, najitangaza kua mwamuzi wa pambano hilo,
Na napendekeza wapigane mechi mbili yaani moja ipigwe kawe ukwamani au tp kwa mwamposa ili wakimaliza mechi waombewe kabisa,
Mechi ya pili iwe mapinga ili kuwakwepa bodaboda wasimsaidie Umughaka kama atanyukwa,
Maandalizi ya mechi kwanza kitapikwa chakula cha pamoja na wapishi watakua wahaya, waha kazi yao itakua kutafuta kuni na kuchota maji, wanyiramba wao ni kuosha vyombo na warangi kazi yao itakua ni kukaribisha wageni,
Aina ya chakula itakua kuna kichuri, sato wa kuchomwa, ugali wa mtama, na supu ya mbuzi,
Mavazi Umughaka atavaa jezi ya yanga na Gentamycine atavaa jezi ya simba,
Katika pambano hilo hakuna kulia hata ukiumia utavumilia tu hivo hivo,
Nawakaribisha nyote ndugu watazamaji na tarehe itatangazwa rasmi na mwamuzi nipo tayari.
Nitaomba mashabiki wa pande zote muwe wengi maana hawa wajinga wanaweza kunigeuka wakaanza kunitandika mimi refa hivo muwepo kwa tahadhari maana hawaeleweki hawa, wapiganaji wetu,
 
Back
Top Bottom