Leo tarehe 16.6.2024 Katika zunguuka yangu nimefika eneo la majengo karibu na shule ya Secondari Legico Mbeya mjini. Nikakuta kuna umati wa watu nikasogea baada ya kusikia sauti za spika. Nilipofika nikawakuta watu wengi tu, sikutaka kuuliza kuna nn maana macho ninayo masikio ninayo. Nikaona wanakaribishana viongozi wa CCM mara Mwenezi, mara katibu wa tawi mara diwani mara mwenyekiti.
Hapo walikuwapo watu kadhaa walioonekana wamevaa t-shirt zimeandikwa Mwamnyeto Foundation. Alikuwapo Mwamnyeto, Zawadi Mauya, Juma Mgunda masikio yangu yakasikia kwamba Mwamnyeto Foundation wamekuja kutoa msaada Kwa wazee wa kata ya Majengo. Jambo jema.
Lakini kilichonishangaza ni eneo Hilo kutokuwa eneo la kutoa misaada pakawa Sasa ni Tulia kafanya hili, Samia kafanya hili na CCM imefanya hiki. Lengo lilikuwa ni kutoa msaada Kwa wazee hasa kipindi hiki Cha sikukuu au kumtangaza Tulia na Samia?
Mulienda kuwasaidia wazee au kufanya siasa? Halafu eti mnataka na baraka za Mungu ziwashukie Kwa unafiki huo? Mwamnyeto umekuwa sehemu hiyo? Foundation yako ni sehemu ya CCM?
Tuambie tusio upande wa CCM tusikuunge mkono kwa juhudi zako. Mwamnyeto foundation mmeamua kutumika ki-siasa? Au Mimi ndo siyo muelewa?