Mwambusi, Yanga ni timu kubwa, kula kwenye VIHOTEL UCHWARA kunakupunguzia heshima yako

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,734
239,355
Nimekuona si mara moja ukipata lunch kwenye kihoteli cha wasomali mtaa wa kongo , kariakoo .

Hiki kihoteli kisichokuwa hata na feni achilia mbali a/c si sawa kwa hadhi yako , hakuna haja ya wewe kocha msaidizi wa Yanga afrika kwenda kubanana na wamachinga kwenye foleni ya wali nyama wa 3500 /, pondamali atakupoteza , mbona yeye hali kwa wasomali ?

Ingekuwa simba tusingeshangaa lakini yanga mbona shida hizo hakuna ? Jiangalie mkuu na ikiwezekana jirekebishe .

.....Itaendelea ikibidi .
 
Mind your business acha umbeya kila mtu na malengo yake ya maisha.
 
Mtoa post anawakilisha tabia zetu za kiafrika (sio wote ila wengi na sio tabia nzuri). Kubadilisha life style mara kwa mara kutokana na kuongezeka kwa kipato. Hayo ni maisha binafsi ya mtu na si ajabu ndio sehemu anazokutana na rafiki zake wa siku nyingi. Kumbuka hata hapo hotelini kuna washabiki wa hiyo timu yake. Sioni tatizo la huyo kocha bali naona tatizo la mtoa post
 
Huijui heshima ya kocha msaidizi wa timu inayoshindana kimataifa wewe , ni lazima kuwepo na gap kati yake na watu wengine , kwanza kujitenga na kadamnasi kutamwepusha na tuhuma za mara kwa mara za kibongo za kuuza timu au kupanga matokeo , ngoja itokee game ya simba na yanga ndio utanielewa .
 
Mtoa post anawakilisha tabia zetu za kiafrika (sio wote ila wengi na sio tabia nzuri). Kubadilisha life style mara kwa mara kutokana na kuongezeka kwa kipato. Hayo ni maisha binafsi ya mtu na si ajabu ndio sehemu anazokutana na rafiki zake wa siku nyingi. Kumbuka hata hapo hotelini kuna washabiki wa hiyo timu yake. Sioni tatizo la huyo kocha bali naona tatizo la mtoa post
Huyu mleta mada ndio wale wanaokula lunch pale samaki samaki samora then usiku anaenda kulala kwake maji matitu..
 
Mtoa post anawakilisha tabia zetu za kiafrika (sio wote ila wengi na sio tabia nzuri). Kubadilisha life style mara kwa mara kutokana na kuongezeka kwa kipato. Hayo ni maisha binafsi ya mtu na si ajabu ndio sehemu anazokutana na rafiki zake wa siku nyingi. Kumbuka hata hapo hotelini kuna washabiki wa hiyo timu yake. Sioni tatizo la huyo kocha bali naona tatizo la mtoa post
Mimi ni Mwanasimba mwenye matarajio ya kuongoza timu , wala sina kolabo yoyote na Yanga , lakini nimesononeka sana kwa huyu shujaa wa timu yenu kumuona mara nyingi akila uswahilini , kama shida ni hela basi alipwe malimbikizo yake , hawa makocha wa yanga na simba wanavumilia mengi sana ambayo wewe huyajui .
 
Mtoa post anawakilisha tabia zetu za kiafrika (sio wote ila wengi na sio tabia nzuri). Kubadilisha life style mara kwa mara kutokana na kuongezeka kwa kipato. Hayo ni maisha binafsi ya mtu na si ajabu ndio sehemu anazokutana na rafiki zake wa siku nyingi. Kumbuka hata hapo hotelini kuna washabiki wa hiyo timu yake. Sioni tatizo la huyo kocha bali naona tatizo la mtoa post
umkute mayor wa jiji humo utasema ndio life aliyochagua?
 
Nilikuwa duka fulani la mpemba maeneo ya Bunju, Dar es Salaam.

Ghafla nikaona basi la Simba SC likisimama na wakashuka wachezaji wakaja dukani kununua Maji ya Kandoro.

Mmoja aliamua kununua maji 6, kaweka kwenye mfuko wa rambo.
Mkuu punguza chumvi,japo nakiri Timu yetu imefulia lakini sii kwaa kiasi hiki...
 
Back
Top Bottom