Mwambieni Zitto ajifunze kutafuna, kutafuniwa kutamponza

Ndata

JF-Expert Member
Mar 2, 2017
226
321
Ni nani asiyefahamu Dr Slaa alikuwa mtafunaji Zitto mmezaji. Yaani Slaa alikuwa akifanya Tafiti yeye Zitto anakuwa speaker tuu ya kusema yale yaliyoandaliwa na Slaa. Huu ulikuwa mkakati wa kuikuza Chadema. Hapa homeboy akavimba kichwa baada ya umaarufu.

Alivyokuja Kafulila, Kafulila akawa anatafuta nitoke vipi ila ghafla akaotea mchongo wa Escrow kama kawaida Spika ikataka kurob ile issue. Huu ukawa mwanzo wa ugomvi kati ya Kafulila na Zitto.

Leo sitaki kujikita zaidi huko ila nataka niangaze zaidi kwenye ujenzi wa chama. Tagusa kidogo Chadema then tamaliza na ACT inayoongozwa na yeye.

Wakati wa Chadema, Zitto ndio mbunge pekee na Kiongozi aliyeshindwa kuikuza Chadema kwenye mkoa na kanda atokayo. Pamoja na umaarufu wake wote hadi anahama Chadema mbunge wa Chadema Kigoma nzima alikua peke yake. Madhara ya kupenda kutafuniwa haya.

Mwaka 2014 wakati ACT inaasisiwa Zitto alikuwa Chadema akisapoti uanzishwaji ACT huku akiendelea kuomba asamehewe Chadema.

Vijana wakaingia mzigoni, wakafight kwa hali na mali chama ikasimama. Baada ya kuona machine imekolea moto huyo akajiunga ACT na kujipa umungu mtu wa Chama. Hakutaka hata kushindana na mtu.

Leo baada ya Maalim kujiunga ACT na kuja pamoja na kundi lake tunaona Zitto kahamishia nguvu Kusini na pemba eti anajenga chama . Kwanini chama asianze kukijenga nyumbani.

Mpaka sasa mbali na Kigoma mjini hata Kaskazini aliyoiongoza kwa miaka kumi hana uhakika wa kupata mbunge hata mkurugenzi wampe Jashia Hamis na Boaz Chuma..

Zitto ni muoga wa kutafuna, kujenga au kuanza from the scratch. Tunafahamu kina Bwege tayari ni wabunge na wenye platform kubwa Kusini ni kwanini yeye kama kiongozi asiwashawishi wenzake waende maeneo ambayo chama hakipo wakijenge. Uoga wa kutafuna na kuzoea kumeza walichotafuna wenzake.

Wale wanaodhani Zitto ni jasiri na shujaa muulizeni kashindwaje kukivusha chama kutoka mjini hadi Kasulu? Muuluzeni ni kwanini anazurura majimbo ambayo yalikuwa na wabunge wa CUF waliokimbilia ACT na sio majimbo ambayo kazi bado kubwa?

Akiwapa jibu mtafahamu kweli ni shujaa au kibogoyo mmeazaji wa kilichotafunwa na wanaume wenye miraba sita.

Picha Afande Sele akiijenga ACT

Cwu @2020
IMG-20200622-WA0008.jpg
 
Unaonekana kama una hoja, lakini mimi kwa hili niko upande wa Zitto kwa sababu ndege mmoja mkononi, ni bora zaidi kuliko 10 mtini.

Tuna miezi kadhaa tu kuelekea uchaguzi mkuu, na kama kuna wabunge wa CUF ambao wamehamia ACT wazalendo, inalipa zaidi kwa Zitto kwa muda huu, kuanza kujiimarisha kwenye majimbo ya watu hawa kwa sababu chances kwamba wabunge hao watashinda tena Ubunge na kuingia Bungeni kwa tiketi ya ACT wazalendo ni kubwa, kuliko aanze kwenda kuanza kuparangana Kasulu na majimbo mengine ambayo hana hata uhakika wa kuyapata, eti kisa tu ni nyumbani kwao. Ni kweli anatakiwa baadaye akakiimarishe chama huko lakini si kwa wakati huu kwa sababu uchaguzi umekaribia muno, atafanya hivyo baada ya uchaguzi mkuu.

Zaidi ni kuwa huyu mtu amebahatika kuanzisha chama ambacho kuna uwezekano mkubwa baada ya uchaguzi mkuu 2020, kikawa chama cha pili kwa ukubwa na uwingi wa idadi ya wabunge, kote bara na visiwani, kikiifuatia CCM.

Kwa hili mimi naomba watu wamshauri vizuri Zitto, he is actually in the very right track kwa sasa. Aendelee kufanya kazi huko huko ambako kuna wanachama ambao ni potential kwa ajili ya kuchukua majimbo ya uchaguzi mwaka huu 2020. Naomba sana katika hili watu wasimshauri vibaya au kwa wivu!
 
Hi point, kwanini kashindwa kukuza chama hata kwao kigoma?
Baada ya uchaguzi mkuu 2020, atafanikiwa kukiimarisha Kigoma pia. Watu wanaangalia potential ya chama kwanza halafu ndiyo wanajiunga. Akipata wabunge uchaguzi ujao, itakuwa ni ticket yake pia ya kupata wanachama wengi wapya kutoka majimbo yaliyoko Kigoma. Waha mimi nawajua, hawajiungi na chama eti tu kwa sababu kimeanzishwa na Zitto na anatokea Kigoma, hapana. Kwanza wako smart halafu ukitaka hata ubishi nao pia wanayo karama. They are very smart, chukulia mfano rahisi tu kwa Kafulila
 
Mh zitto ni mmezaji kama wamezaji wengine na vile vile ni MTU wa kiki katika Ahadi zake kumi na tano katika manispaa ya kigoma ujiji hajatekeleza lolote hivyo basi ameshindwa kubeba ndoto za wanakigoma na sasa wanakigoma wamepoteza imani naye kwa kuwa si mkweli
 
Ukiona haufanikiwi kuna sehemu haujapiga hesabu zako sawasawa, Acha anaejielewa afanye yake adhihirishe ukomavu wake ktk siasa.

Ni wabunge wachache wanaweza kugombea majimbo mawili tofaut na wakashinda, yeye ameweza. Na anaweza kugombea jimbo lingine la 3 na akapita.

Kuna wananchi wanawachagua wabunge kwa maslahi ya taifa zima hawajiangalii wao tu. Baadhi ya majimbo hayo yapo Kigoma, Singida, Kilimanjaro na Dar.
 
Ni wivu tu unakusumbua. Hii miaka mitano ya Jiwe siasa ilipigwa lockdown isipokuwa kwa CCM tu au umejisahaulisha?
 
Kumeza haikatazwi,Slaa haijawahi kuwa mtafutaji,Bali alikuwa anavujishiwa habari na walioichoka michosho ya serikali,hata kafulila vivyo hivyo.Kama unataka kujua kuwa Slaa alikuwa mweupe kichwani angalia Yangu amekuwa balozi huko Scandinavia ameisaidia Nini Tanzania?Anazidiwa Hadi na balozi anayewakilisha nchi zetu Korea kusini na Japan.Saizi hata ukiangalia ujengaji wa hoja Slaa Hana kabisa.Sasa huko kutafuna vipi?

Halafu unaposema Zitto anameza hajui kutafuta so kweli,Ana uahawishi mkubwa na hoja kuzidi Dr.Slaa.Hao wabunge wa CUF wanaenda ACT mi sawa na Magufuli anavyochukia wapinzani na kuwapa nyadhifa serikalini, maana yake chama chake hakina hazina ya kutosha kuongoza serikali Sasa kwa Nini asiende upinzani kuiba madini?
 
Back
Top Bottom